Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

To the Ministers-Nothing to Celebrate, go to work

with 25 comments

Mawaziri, hakuna sherehe, nendeni mkawajibike!

Rais Jakaya Kikwete akitangaza Baraza jipya la Mawaziri, Ikulu jana.

Juhudi za kurejesha misingi ya uwajibikaji katika utumishi wa umma zimeanza kuzaa matunda Baada ya Rais kutekeleza shinikizo la Bunge la kuwafukuza kazi baadhi ya Mawaziri ambao Wizara zao zimetuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma, rushwa na utendaji mbovu. Mawaziri 6 wamefukuzwa kazi baada ya kugoma kujiuzulu wao wenyewe, manaibu Waziri 2 wamefukuzwa pia.

Ndugu George Mkuchika alitakiwa kujiuzulu, akajiuzulu lakini Rais amemrudisha kwenye Baraza kama Waziri wa Utawala Bora. Yeye nampongeza kwani hakuwa na makuu ya kuanza kujitetea kama wengine. Atakuwa ametoa funzo kwa wenzake.

Kwa kawaida wateule hufanya sherehe kwa kuteuliwa kwao. Nitawashangaa watakaofanya sherehe safari hii kwani hakuna cha kufurahia. Nitawashangaa Watakaokwenda kuapa na Maua kwa furaha kwani furaha itakuwa ya muda mfupi tu. Mkutano wa Bunge wa Bajeti ni mwezi ujao tu na Wateule wote watakuwa kikaangoni. Too short honeymoon.

Hakuna cha kusherehekea kwa sababu nchi in changamoto nyingi sana. Changamoto ya kuzalisha umeme wa kutosha na kuusambaza kwa wananchi wengi, changamoto ya kukuza uchumi wa vijijini na kukuza uzalishaji viwandani ili kutengeneza ajira kwa vijana, changamoto ya kuongeza mapato ya Utalii kutoka katika hifadhi zetu na kuvutia watalii zaidi katika nchi yetu.

Nimewapigia simu wateule wengi na kuwaambia, siwapi pongezi Bali nawatakia kazi njema. Nawatakia uwajibikaji mwema. Uwajibikaji ndio msingi wa kupambana na rushwa, uvivu na uzembe.

Kwa Waziri wa Fedha, ambaye mimi ni Waziri Kivuli wake (Kama Kiongozi wa Upinzani Bungeni hataniwajibisha pia), namwambia uteuzi wake ni changamoto kubwa sana katika maisha yake.

Hivi sasa eneo lenye Bajeti kubwa kuliko zote nchini ni huduma kwa Deni la Taifa (services to national debt). Lazima kuangalia upya Deni la Taifa. Hivi sasa Deni la Taifa ukijumlisha na Dhamana za Serikali (government guarantees) limefikia tshs 22trn mpaka Desemba 2011. Nimewahi kutaka ukaguzi Maalumu katika ‘account’ ya Deni la Taifa. Linarejea wigo huu. Tunalipa takribani 1.9trn tshs kwa mwaka kuhudumia Deni la Taifa. Zaidi ya Bajeti ya miumbombinu, Afya, Maji, Umeme nk.

Mfumuko wa Bei, misamaha ya kodi na kodi zinazozuia watanzania kujiajiri ni changamoto kubwa sana Wizara ya Fedha lazima ihangaike nayo.

Usimamizi wa Mashirika ya Umma kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina na hasa usimamizi wa Hisa za Serikali katika kampuni binafsi ni masuala yanayohitaji masuluhisho sasa na sio baadaye.

Kwa Mwalimu wangu Dkt. Mwakyembe, utakumbukwa kwa Jambo moja tu. RELI. ‘make our Railway system work‘. Hutakuwa na ‘legacy’ nyingine isipokuwa Reli maaana Bandari bila Reli ni sawa na Bure.

Tunatumia zaidi ya tshs 300bn kwa mwaka kukarabati barabara wakati tunahitaji tshs 200bn kukarabati Reli iweze kusafirisha mzigo kwenda Bandarini na kutoka Bandarini.

Ndio maana nasema hakuna Jambo la kusherehekea maana wajibu mliopewa na Rais ni mtihani mkubwa kwenu katika kulitumikia Taifa letu. Msipowajibika, mtakumbwa na fagio la chuma!

Mkisha kula kiapo, kimbieni kazini. Nothing to celebrate. Hit the ground running.

ZZK

Dar-es-Salaam

Jumamosi, Mei 5 2012

25 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. operation uwajibikaji imezaa matunda

  todo

  May 5, 2012 at 1:38 PM

 2. Safi sana kamanda kwa mawazo yako ya kujenga tz.,nakuomba twende tuijenge manyovu make ntabaliba hana mpya kama kilotsi

  Sjmgombozi

  May 5, 2012 at 1:41 PM

 3. SAFI SANA MHESHIMIWA ZUBERI ZITTO KABWE KWA UJUMBE HUO KWA MAWAZIRI WETU WAPYA KWANI HUU SI MDA WA KUSHEREKEA KWA KUTEULIWA BALI NI MDA WA KUTAFAKARI NAMNA WATAKAVYOFANYA KAZI KWA UFANISI.

  JALIWA

  May 5, 2012 at 1:55 PM

 4. Mchango wako katika kufichua maovu na kuikosoa serikali hautakaa upotee katika historia,Zitto nakutakia maisha marefu na Mungu akupe afya na ujasiri wa kukemea mabaya.

  Abdallah Kileo

  May 5, 2012 at 2:05 PM

 5. this is realy gud Brother Zitto… Huu si muda wa sherehe bali ni muda wa kuwajibika kwa ajili ya Watz

  david

  May 5, 2012 at 2:07 PM

 6. tTunahitaji viongozi wa aina ya zitto,magufuli na wachache sana sijawataja

  Daudi Masyi

  May 5, 2012 at 2:54 PM

 7. Well said Mh.Zitto,ni wakati wao kutenda,na tuone wanatenda vile tunavyotegemea,watanzania tunahali ngumu katika kila kitu.

  Barani

  May 5, 2012 at 3:03 PM

 8. Tunakuombea sana kwa mungu zitto wewe ni mbunge wakweli,

  JACOB

  May 5, 2012 at 3:08 PM

 9. safi san msh zito kabwe!

  hobidan

  May 5, 2012 at 4:51 PM

 10. Ujumbe imara kutoka kwa mtu imara unaleta matumaini makubwa kwa vijana na vizazi vijavyo! Ni tumaini langu kwamba uwajibikaji utapewa tafsiri sahii na kila mtu atajua maana halisi si kwa viongozi tu, ila kwa kila mmoja wetu sehemu alipo. Unawajibikaje nyumbani kwako, mtaani kwako, kazini kwako, na zaidi ya yote, unawajibikaje kuwaajibisha wasiowajibika.

  Kila la kheri Zitto! Mungu awalinde na awape nguvu zaidi

  Sam Muro

  May 5, 2012 at 4:57 PM

 11. ….well said Mheshimiwa Zitto Kabwe….the way you have conducted your opposition is something to desire…with intellect, pride, honesty, straightforwardness and without fear of repercussions, a true man of the people. We salute you….

 12. kweli kabisa unachosema mheshimiwa zitto. una maono ya mbali sana

  fortunatha

  May 5, 2012 at 6:10 PM

 13. ur 100% true big up! right thought

  Thomas Macha

  May 5, 2012 at 6:52 PM

 14. Very true brother, we real appreciate your work , this is the result of your work in national assembly!

  Simon Mwambagi

  May 5, 2012 at 7:46 PM

 15. Nice

  Brian

  May 5, 2012 at 8:20 PM

 16. PAMOJA KAKA ZITTO KATIKA MAPAMBANO HAYA..YA KUIKOMBOA TENA NCHI YETU!

  mohamed mwabumba

  May 5, 2012 at 11:09 PM

 17. Mheshimiwa Zitto suala lililobaki na nakupa kama deni ni kuhakikisha majimbo yote ya Kigoma tunachukua, maana sioni ugumu wowote cha msingi ni kutuandalia vijana ambao unaona twaweza kuwa amana ya kubeba majimbo yetu. tumechoka na ccm

  Rwigwa Aman

  May 5, 2012 at 11:35 PM

 18. Safi sana muheshimiwa Zitto ninachojua ulichofanya ni 1%ya yale unayotakiwa kwa sasa hamna haja ya malumbano nendeni vijijini kuhimarisha chama ninaamini 2015 asilimia 99% ya kinachohitajika kufanya kitatimia

  NAMKANDA

  May 6, 2012 at 7:55 AM

 19. Kati ya awamu ambazo wabunge wamefanya kazi yao, awamu hii mmefanya vyema sana. Mkutano wa Saba mmeandika historia. Nguvu na akili hizi mlizozitumia ziendelezwe, zisikome kwa mawaziri wote ili isije ikajengeka dhana kwamba kulikuwa na MAWAZIRI mliowalenga. Kila wizara muichokonoe, hakuna kumwamini waziri yeyote, kila atakayeboronga apewe kibano kikali, HESHIMA YA NCHI itakuwepo kwani tutaachana na bla bla za bungeni. Ilikuwa inanikera sana kuona swali lililojibiwa miaka mitano iliyopita, hadi sasa linaendelea kujibiwa vile vile kwa kuwaliwaza wabunge kama vile watoto. Sasa wabunge mkatae na muunde kikosi cha kufuatilia majibu ya mawaziri kwa maswali wanayoulizwa bungeni ili iwe njia ya kuwaumbua na kuwawajibisha waliozoea kujibu kwa mazoea. Hongereni sana wabunge.

  Stella

  May 6, 2012 at 12:52 PM

 20. Ulichosema ni 100% safi sana. It is high time leaders remember that they are in these positions to SERVE the people and not to be SERVED privileges on a platter by virtue of their positons….there is no reason at all that our beautiful endowed country should be poor!!!! can business and politics mix?

  sauda

  May 6, 2012 at 1:13 PM

 21. Kisu kilichotumika kuwachinjia mawaziri waliopigwa chini ,kinolewe makali zaidi kwa wale watakaofanya mchezo kipindi kijacho,ni lazima tuwateketeze mafisadi wote.

  Matandiko

  May 8, 2012 at 11:54 AM

 22. JAMANI WAONEE HURUMA WATANZANIA WANAOKOSA MLOWA KILA SIKU, WANOKOSA SHS 2,5000/= ZA MATIBABU KATIKA HOSPITALI/ZAHANATI ZA SERIKALI, WAIOWEZA KUMUDI ADA YA WATOTO WAO, WAKASHINDWA KUENDELEA NA SHULE, NK.

  Dominico Kabyemera

  May 9, 2012 at 11:38 PM

 23. Sina mengi leo sema nimefurahi kujiunga kwenye .com yako pia na twitter so expect comment nyingi saana now am going to facebook pia

  mwisho mwampamba

  May 10, 2012 at 9:53 PM

 24. Naomba niseme haya machache! Japo unastahili sifa kwa kusababisha naona hatutakuwa tumefanya chochote kwa kufukuzisha watu serikalini iwe ngazi yeyote ile mchezo utakuwa wa toa kitu weka kitu gemu lile lile! Tuige wenzetu tena hasa wachina manake kuwafukuza sio fundisho kwani wanabaki na milundo ya pesa mfukoni na majumba na magari ya kifahari huku wakituachia madeni mengi pamoja na miradi ikiteketea! Dawa ni kuwafungulia mashtaka kwa uwizi wakuaminiwa , kutumia madaraka kwa ubinafsi ,na kutowajibika kadarakani ! Wananchi tuandamane tukidai wafunguliwe mashataka pia wakiwa washtakiwa mali zinyaganwe zoooote na ikiwezekana wasipewe dhamana kwani tulishawapa dhamana ya madaraka wakachezea nakupuzia ! Na hatma yake wafungwe maisha ama kunyongwa kabisa ndio itakuwa fundisho kwa wengine kwani zaidi ya kutumia madaraka vibaya , kupotesha jamii, kujilimbikizia mali pia wanakesi ya kujibu ya mauaji kwani makosa yao yote yamesababisha vifo visivyo vya idadi ! Watu wamekufa njaa kwa kukosa chakula, matibabu hovyo ama hakuna kabisa mahospitalini, ajali shauri ya usafiri mbovu pamoja na njia zenyewe ikiwa ni majini,barabarani , angani, relini na kosa kubwa zaidi ni elimu duni inasababisha ufukara wa akili amabayo imetusababisha tushindwe hata kujikoa wenyewe shauri hatujui chakufanya!

  mwisho mwampamba

  May 10, 2012 at 10:11 PM

 25. tna huu si wakati wa kupongezana kabisa nchi inaelekea kubaya kilichoppo ni kazi tu

  matandiko

  June 10, 2012 at 10:40 AM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: