Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Ufanyike Uthibitisho huru (independent verification ) Mradi wa Gati 13 na 14 Bandari ya Dar

with one comment

Ufanyike Uthibitisho huru (independent verification ) Mradi wa Gati 13 na 14 Bandari ya Dar

Mwaka jana nilipokuwa nachangia hoja ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi nilisema maneno haya

“Mheshimiwa Mwenyekiti, mikopo mingi ya China  gharama yake ni kubwa sana. Sasa hivi kwa sababu ya matatizo ya madeni ya Marekani Wachina wanakimbilia nchi za Afrika, lakini wanatupa mikopo kwa gharama kubwa sana.

Kwa mfano,  gharama halisi za kutengeneza berth 13&14 katika Bandari ya Dar es Salaam hazizidi dola milioni 340. Mkopo ambao Wachina wanataka kutupa ni wa dola milioni 525, lakini kuna the easiest way ya kwenda kutangaza tender through PPP International Tender watu wa-bid waje watengeneze, wa-own na baadaye wa-transfers kwa Serikali kwa Mamlaka ya Bandari, that is the easiest way wala nchi haiingii kwenye mikopo.

Kwa hiyo, ninaomba muangalie hizo options, mikopo ya China, msiende tu kukopa ni ghali sana kwa sababu inaendana na conditionality kwamba tunakupa mkopo lakini Contractor atoke China maana yake ni kwamba hela yote inarudi China. So you have to be very careful katika maamuzi haya” mwisho wa kunukuu.

Jana kamati ya Bunge ya Miundombinu ilitoa hoja kwamba Serikali iendelee na mkopo wa kutoka China wa USD 525m ili kujenga magati hayo.
Mbunge wa Ubungo ndugu John Mnyika Leo alilitaka Bunge kufanya marekebisho ya mapendekezo ya Kamati ili kufanya uchunguzi huru (independent verification ) kuhusiana na gharama hizo za Ujenzi.
Uamuzi huu utaokoa fedha nyingi sana za Umma kwani itafanya Mamlaka ya Bandari na Taifa kuwa na uhakika wa dhati wa gharama.

Nini ilivyo sasa?
Kampuni ambayo inapendekezwa kupewa kazi ya Ujenzi ndiyo iliyofanya upembuzi yakinifu. Kampuni hiyo hiyo pia ndio ilikwenda kutafuta Mkopo kutoka Exim Bank China.
Je, tuna uhakika gani kwamba Kampuni hii ilipandisha gharama za Mradi huu kwani wao ndio walikuwa Mhandisi Mshauri wa kufanya feasibility study, Kampuni hiyo hiyo ndiyo ilitafuta Mkopo na Kampuni hiyo hiyo ndio inapendekezwa kuwa mjenzi.

Hoja ya Mnyika imepitishwa Kwa kuungwa mkono na Wabunge wengi sana. Tumetenda Haki.

Advertisements

Written by zittokabwe

April 21, 2012 at 6:01 PM

Posted in Uncategorized

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. Mheshimiwa Zitto, kazi unayoifanya watanzania wengi tunakuunga mkono na kukuombea kwa Mungu akupe nguvu na ujasiri wa kuuzungumzia umma wa wanyonge wa Tanzania. Mimi naomba nitoe ushauri wangu kuhusiana na jinsi kamati yako (POAC) inavyosimamia mashirika ya umma. Ninachokiona ni kuwa kamati hii inafanyakazi kwa kutegemea (1) umakini na uzalendo wa wajumbe na (2) umakini na uchapakazi wa CAG. Namaanisha kuwa kamati yako haina independent way ya kusimamia mashirika ya umma (kuna mashirika ya umma yanafanya vibaya mno – mfano chuo cha uhasibu Arusha) lakini kwa kuwa CAG ametoa ripoti safi na kamati yako imelisifia shirika hili la umma. Duniani kote imedhihirika kuwa kusimamia mashirika au taasisi kwa kuangalia tu mehesabu ya fedha haitoshi (kuna makampuni mengi Ulaya yalifilisika wakati taarifa za ukaguzi wa mahesabu zilionyesha kuwa ni safi). Nashauri kuwa, kwa kuwa mahesabu ya fedha yanaonyesha mapato na matumizi yanayotokana na utekelezaji wa mpango mkakati wa shirika husika, kamati yako itake: (1) kila shirika kuleta mpango mkakati na budgeti kwenye kamati yako (2) wakati wa kupitia mahesabu ya fedha, bodi ileta physical performance- utekelezaji wa mpango mkakati kivitendo.

    Raymond Muro

    May 6, 2012 at 12:34 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: