Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Maana ya matokeo Arumeru Mashariki

with 12 comments

Matokeo ya Arumeru na kata za Mwanza, Songea na Mbeya ni mwanzo wa safari ya mwisho ya CCM na kwamba wanaondolewa madarakani kwa sababu wananchi wamekasirishwa, hasira ambazo fedha haiwezi kununua. Hasira ambayo matusi hayawezi kuifuta. Hasira ambayo vitisho havifui dafu. Hasira ya kutaka huduma bora. Hasira ya kuchoka na umasikini na kufukarishwa. Hasira ya kuchoshwa na ufisadi.

Mhe Mwenyekiti Freeman Mbowe na Mhe Joshua Nassari

Mnamo tarehe 11 Machi mwaka huu 2012 nikiwa ndani ya ndege natokea Arumeru kuzindua kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenda Kirumba Mwanza kuzindua kampeni za Udiwani katika kata ya Kirumba, niliandika makala kuhusu nini kitaamua mshindi katika uchaguzi ule. Nilianza makala yangu ile kwa kusema haya
“Uchaguzi wa Ubunge Arumeru Mashariki ni kipimo cha namna wananchi mnavyoridhika na watawala, namna mnavyoridhika na mgawo wa Ardhi na namna mnavyoridhika na mgawanyo wa Maji katika Wilaya yenu”.

Haya maneno ilikuwa ni nukuu ya sehemu ya hotuba niliyotoa wakati namkaribisha Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe kuzindua rasmi kampeni zetu.
Ardhi ilikuwa ajenda kubwa sana. Washindani wetu wa CCM wakaona hatari ya hoja ya Ardhi na kuanza kutoa ahadi mbalimbali za kumaliza kero ya Ardhi. Hawakuaminika. Wananchi walisema, hawa wamemaliza miaka 50 bila kutatua kero hii, watawezaje kupata suluhisho sasa. Wakakataa. Hawakuichagua CCM na badala yake wakamchagua kwa kura nyingi sana ndugu Joshua Nassari, kijana wa miaka 26 tu kuwa Mbunge wa Jimbo Lao. Katika makala ile nilieleza wazi kwamba
“Uchaguzi wa Arumeru ni uchaguzi kati ya kuwa na Ardhi au kuendelea kutokuwa nayo. Ni uchaguzi muhimu kwa watu wa Meru. Wasio na Ardhi watamchagua mgombea atakayesimamia mgawo wa Ardhi unaozingatia haki. Mgombea huyo ni mgombea wa CHADEMA ndugu Joshua Nassari. Sasa Nassari lazima aibebe ajenda Ardhi. Hana namna ni lazima awe sauti ya wananchi masikini waliofukarishwa na mfumo mbovu wa kugawa Ardhi ulioanzishwa wakati wa ukoloni na kuendelezwa chini ya Uongozi wa CCM.
Ushindi wa CHADEMA katika uchaguzi wa Arumeru ni ishara ya dhahiri kabisa kwamba siku za CCM kuongoza Taifa letu zinahesabika. Ukilinganisha nguvu ya rasilimali watu na fedha ambayo CCM waliiweka huko Meru kulinganisha na CHADEMA unaona dhahiri kabisa kuwa fedha sio kigezo cha kushinda uchaguzi. Wananchi sasa wanataka masuala Yao yashughulikiwe. Hii pia imejionyesha katika chaguzi za Madiwani.

CCM imepoteza nusu ya viti vya Udiwani vilivyokuwa vinagombewa. Katanza Lizaboni Songea, Kiwira Mbeya na Kirumba Mwanza zote zimeenda CHADEMA. Kata ya Msambweni Tanga imeenda CUF. CCM walipata kata katika Wilaya ya Bagamoyo, Bariadi na Temeke. Pia walipata kata katika manispaa ya Dodoma.

Huu ni uchaguzi wa kwanza wa Madiwani ambao CCM imepoteza nusu ya viti vilivyokuwa vinagombewa toka mfumo wa vyama vingine uanze. Arumeru imekuwa jimbo la kwanza CCM kulipoteza kwa chama cha upinzani Tangu mwaka 1997 ambapo CCM walipoteza jimbo la Magu kwa chama cha UDP. Kwa CHADEMA hili ni jimbo la kwanza kulichukua kutoka CCM katika uchaguzi mdogo toka ianzishwe mwaka 1992. Itakumbukwa kwamba mwaka 2008 CHADEMA ilishinda jimbo la Tarime kwa kulirejesha maana kilikuwa linashikiliwa nacho.

People's power

Hivyo ni dhahiri kabisa kwamba siku za CCM kuwa madarakani zinahesabika. Ushindi wa Arumeru na Udiwani katika kata mbalimbali umeleta mageuzi makubwa ya kisaikolojia kwa wananchi kuliko hata ushindi wa Tarime. Ni wazi kabisa kuwa ushindi huu utafutiwa na mikutano wa kunadi chama katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Kusini na ile ya Magharibi ambapo CHADEMA haijafanya operesheni.

Kushindwa kwa CCM Arumeru pia kutal eta mpasuko zaidi ndani ya CCM na kuunganisha nguvu za wanasiasa ndani ya CHADEMA. Wakati CCM itakuwa inanyoosheana vidole kutafuta mchawi na hata wengine kufurahia kushindwa kwao (wakiamini ni kushindwa mmoja wa mahasimu wao), CHADEMA itakuwa inashikana mikono na kuimarisha mshikamano ili hatimaye kuchukua Dola ifikapo mwaka 2015.

Jambo moja la dhahiri unaliona Baada ya uchaguzi wa Arumeru. Sasa ukipanda Basi kutoka Moshi kwenda Arusha, utopita ngome ya Chadema tu. Moshi mjini, Hai, Arumeru Mashariki na Arusha Mjini. Kwa waliomsoma Rais Museveni katika kitabu chake cha Sowing the Mustered seed, akitumia njia za Frelimo katika ukombozi, eneo hili sasa ni Liberated Zone. Ukanda uliokombolewa.

Lengo langu ni kuonyesha kuwa hii ndio safari ya mwisho ya CCM na kwamba wanaondolewa madarakani kwa sababu wananchi wamekasirishwa, hasira ambazo fedha haiwezi kununua. Hasira ambayo matusi hayawezi kuifuta. Hasira ambayo vitisho havifui dafu. Hasira ya kutaka huduma bora. Hasira ya kuchoka na umasikini na kufukarishwa. Hasira ya kuchoshwa na ufisadi.

 

Advertisements

Written by zittokabwe

April 5, 2012 at 11:36 AM

Posted in Uncategorized

12 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Kurudiwa uchaguzi Arusha mjini kutazidisha mpasuko ndani ya CCM na itakuwa jukwaa muhimu kwa CDM kujiimarisha….kama CDM itamruhusu Lema kugombea tena nnaamini ataweka rekodi ya kuwa mbunge aliyeapishwa mara mbili ndani ya miaka mitano…People’s Power!!!

  hkiboka

  April 5, 2012 at 12:03 PM

 2. Habari kaka
  mimi sitoi Comment ila napenda kutaka kuuliza, hivi mmemchukulia hatua gani ndugu Livingstone Lusinde kwa matusi aliyoyatoa??? me naomba tuandamane na ikiwezekana na yeye anyang’anywe ubunge katika jimbo lake. maana mtu mzima mwenye akili timamu huwezi kuongea upuuzi kama ule infront of the people.
  pls pls lets act on this
  Deborah kutoka Mbeya.

  Deborah Sangu

  April 5, 2012 at 12:05 PM

  • NAMI MAWAZO YANGU NI KAMA YA DEBORAH. KAMA WANA CCM WALIMSHITAKI LEMA, KWA NINI WANA CHADEMA WENYE USHAIDI WA KUTOSHA WASIMSHITAKI LUSINDE. BAADHI YETU TUNAANZA KUCHOSHWA NA USHINDANI WA MATUSI. ARUMERU MASHARIKI ILIZIDI MIPAKA KWA MATUSI.

   DOMINICO

   Dominico Kabyemera

   April 11, 2012 at 11:45 AM

 3. well said zitto, asante sana…. Hata wafanyeje..Arusha mjin tunalirudisha na tunaendela na safari..Monduli, karatu tayari, mbulu tayari… Road to Liberation inazidi kushika kasi….

  Denis

  April 5, 2012 at 12:53 PM

 4. Ni kweli muheshimiwa. Bado tunaamini ukombozi wetu u mikononi mwetu.

  Anatory Amosi Ng'wigulu

  April 5, 2012 at 1:03 PM

 5. That is right brother!unaweza kutueleza uhalali wa hukumu ya mh.lema?

  Robert l mollel

  April 5, 2012 at 1:06 PM

 6. Kaka samahani,nijuze,kisheria ndugu yangu Lema kisheria anaruhusiwa kugombea tena Arusha mjini?

  Mcharo

  April 5, 2012 at 4:39 PM

 7. mwisho wa mabepari na waujumu uchumi wa nchi umefika hatuwezi kulala huku hakizetu zamsingi zikipotea kwenye mikono ya wachache.

  Juael mfinanga

  April 5, 2012 at 10:37 PM

 8. CCM hatutasita kuwapongeza hata mtakapochukua nchi. Japo mnaonyesha kuanza kutanda vijiwingu vya mvua, lakini ni mvua ya manyunyu tu. Kazi bado mnayo CDM, maana sisi tumeweka mizizi shirikishi hasa kwenye matawi ya CHAMA na hususani maeneo ya vijjini ambako hawana mwamko wa siasa hizi za ushindani wa kushika dola. Ushauri wangu kwenu ni kwamba: Kwanza, sasa elekezeni nguvu huku tuliko cc. Pili fungueni matawi kadiri iwezekanavyo hasa yale maeneo yetu makongwe na yenye wazito. Mimi niwatakieni kila kheri na mkitaka kutubwaga tena Arusha mjini basi msisite kumrejesha tena Bw. Lema. Nina uhakika mkimweka huyo basi….CC, itakuwa kush nei.

  Stanley

  April 9, 2012 at 11:43 AM

 9. KABLA YA UCHAGUZI WA ARUMERU MASHARIKI KUFANYIKA NILIWAHI KUANDIKA STATUS KUPITIA FACEBOOK KWA JINA LANGU LA DENISWOOD NIKASEMA MANENO HAYA JOSHUA NASSARI TUMAINI JIPYA LA WANA ARUMERU MASHARIKI NASHUKURU MUNGU KWANI WOTE WALIOCOMMENTS WALINIELEWA NA MWISHO WA SIKU WANA ARUMERI WAKAMCHAGUA JOSHUA NASSARI KIJANA ALIYETUKANWA SANA NA KUKASHIFIWA NA WABUNGE WA CCM NAAMINI SAUTI YA WATU WENGI NI SAUTI YA MUNGU NA NDIO MAANA NASARI AKASHINDA, NA CCM WAMEANZA KUWEWESEKA KWA KUINGILIA UHURU WA MAHAKAMA NA KUMFANYA JAJI GABRIELI MWAKIBARILA KUTENGUA UBUNGE WA GODBLESS LEMA LAKINI NAAMINI TUTASHINDA RUFAA NA LEMA ATASHINDA TENA,HII NI PICHA INAYOWAAMBIA CCM WAJIANDAE KUWA CHAMA CHA UPINZANI

  KINDLY
  LUHUNGA DENIS M

  LUHUNGA DENIS M

  April 9, 2012 at 7:38 PM

 10. Kamanda Zitto Kabwe ninafurahia kazi zako na maongezi yako, Hasa kuhusu Ajira nchini Tanzania. kwa mara ya kwanza moyo wangu umetoka kwenye CCM kuingia kwenye Chadema ndio wenye uchungu na wananchi wa Tanzania bila kujijali wao wenyewe kwanza, Mie inaniuma Mzee wangu ametoka kwenye kijiji cha Masaki huko Kisarawe, katika vijiji vimesahauliwa na Serikali na watu wao pia wenyewe basi vya Kisarawe hapa Tanzania ndio kabisa Maji kila siku hakuna na wananchi wenyewe ndio wanajitahidi na upatikanaji Maji hakuna Mbunge aliofanyia Kazi Maji wala Ajira wala Elimu Uzaramuni kila siku vijana wana Fail kisa wanasema Wazaramo hawapendi kusoma hiyo sio sababu wangekuwa wanatilia nguvu watasoma tu, mie naomba Chadema pia tuache kuongelea Mikoa mikubwa Kama Arusha,Mbeya tuwakumbuke na kuwafungua akili sehemu kama za Kisarawe pia nitashukuru Mada za matatizo yakule yakianza kufunguliwa wazi kwenye Twitter na vyombo vya habari iwe Aibu kubwa kwa CCM huwadanganya sana kule. InshaAllah CCM itakuwa haipo tena kwenye madaraka vijana wanapotea kwenye Elimu na kuendekeza sana Matangazo ya Ulevi uigaji vitu ambavyo havina msingi kama viongozi wakiendekeza Ufisadi unategemea watoto watasoma? nao watataka Pesa za haraka kwa vibaya. Kulwa.

  Kulwa

  April 10, 2012 at 4:56 PM

 11. Unafahamu kwamba wana-CCM waliamini kwa kila kitu (i.e. akili, ubabe wao, pesa zao, matusi yao yoote, nk. nk.) kuwa uchaguzi wa Arumeru Mashariki wangelipita…!!!

  Sylvester George

  April 12, 2012 at 3:06 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: