Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Bunge halina mguso na wananchi ‘out of touch’

with 16 comments

Inasikitisha kwamba Bunge laweza kukaa wiki nzima na kujadili masuala mbalimbali bila kutoa muda kujadili suala la mtikisiko katika sekta Afya. Siku ya kwanza ya Bunge nilisimama kutaka taarifa ya serikali kuhusu mgomo wa madaktari na taarifa hiyo ijadiliwe na Bunge. Spika akalojulisha Bunge kwamba Serikali imempa taarifa na itawasilishwa. Bunge likaahirishwa siku bila kurejea. Kamati ya Uongozi ya Bunge ilipohitaji taarifa ya Serikali, Serikali haikuwa na taarifa. Kwa hiyo walifanya ujanja ujanja kuzuia mjadala wa mgomo wa madaktari.

Leo wabunge kwa mara nyingine wamesimama kutaka mjadala huu wa dharura. Naibu Spika wa Bunge akatumia sababu za kiufundi kuzuia mjadala. Inawezekana wabunge hawakuwaandaa wabunge kusimama kuunga mkono hoja, lakini ni jukumu la Kiti kuona umuhimu na udharura wa mijadala.

Hii inadhihirisha kwamba sasa Bunge kama Mbunge mmoja mmoja au kwa ujumla wake na Taasisi ya Bunge imekosa mguso na Hali ya wananchi (out of touch). Hali hii ni hatari sana. Wananchi wanapoona chombo kinachowawakilisha hakitoi nafasi kwa masuala yanayowagusa, watachukua hatua zao wao wenyewe na hivyo kuhatarisha utulivu wa nchi. Bunge liache shughuli nyingine zote na kutoa fursa ya kupokea taarifa ya serikali kuhusu madai ya Madaktari, kuijadili na kuazimia kwa kuelekeza hatua za kutekelezwa na serikali.

Written by zittokabwe

February 2, 2012 at 12:58 PM

16 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Tufanyeje sasa jamani?

  Francis Kessy

  February 2, 2012 at 1:10 PM

 2. Inasikitisha sana kuona juhudi za mbunge mmoja mmoja haziungwi mkono na bunge zima. Suala la mgomo wa madaktari linaumiza taifa kwa ujumla, wananchi ambao ndo mtaji kwa kila aliye bungeni wanateseka kwa hali hii hasa wakiona wabunge wao wanakaa kimya wakisubiri serikali ndo itoe taarifa, ingetakiwa wabunge waishinikize serikali imalize tatizo hilo mara moja. Naunga mkono juhudi za Mh, Zitto aendelee kuwashawishi wabunge wenzake ili kuokoa maisha ya watanzania.

  Evarist

  February 2, 2012 at 1:31 PM

 3. Hii ni kali wabunge kama wabunge naamini hawana matatizo isipokuwa huyo spika naibu wake na katibu wake hawajui nini maana ya jambo la dharura,Madaktari wamegoma hii ni wiki sasa serikali inashindwa kutoa tamko wananchi wanazidi kutaabika na kufa lakini viongozi wa nchi husika wanafanya mdhaha kwa jambo la hatari kama hili.Hii ni hatari sana kusoma hujui hata kwa kuangalia picha hutambui nini kinaendelea kwenye nchi yako?

  Eliaringa Macha

  February 2, 2012 at 2:30 PM

 4. Ila mkuu zitto usikate tamaa pambana kwa ajili ya wanachi wako sisi tuko pamoja,Watanzania huu ni wakati wa kubadilika na kufanya maamuzi sahihi ona hali ilivyo kwa sasa ni serikali gani inashindwa kufanya juhudi za kumaliza mgomo wa madaktari watu muhimu ambao kazi yao ni kuokoa maisha yetu? Naamini kupitia hili tumeshatambua udhaifu wa serikali tuliyo nayo badala ya kushughulikia masuala nyeti ya kitaifa waziri mkuu na spika wake wanakaa kushangilia rais kuidhinisha posho za wabunge madaktari je???

  Eliaringa Macha

  February 2, 2012 at 2:39 PM

 5. I think imewauma sana ,I call them selfish MP’S coz ime interfere ile sitting allowance waliyokuwa wanaitaka,shame on them…2015 they should never return ,wananchi amkeni…big up comrade Zitto na Dr Hamis mmeonyesha nia…

  Ibrahim

  February 2, 2012 at 6:05 PM

 6. Mh. Zitto tumeona na tunatambua juhudi zako na za Mh. Mnyika katika kushawishi suala la mgomo wa madaktari linajadiliwa bungeni.Wananchi hatujafurahishwa.Tunaomba Chadema kama chama kitafute namna ya kuwaunganisha wananchi ili wailazimishe serikali kuacha mzaha na kutafuta ufumbuzi wa sakata hili la mgomo.

  stanslaus

  February 2, 2012 at 6:26 PM

 7. Sasa wananchi wanateketea kwa kukosa tiba, hakuna Madaktari. Jamani oneni jambo hili ni la dharura! Sisi hatuna uwezo wa kwenda India! Hiyo misuada mingine mnayopitisha itakua ya nani wakati watu wanakufa?
  Tusiangalie madhara ambayo yameshatokea, hayo ni kidogo tu! Yatatokea makubwa zaidi kwasababu tiba iliyocheleweshwa kwa hawa wagonjwa itawaadhiri na labda kuwa sugu matokeo yake ni nini? kifo. Chonde chonde wapeni maadai yao mupate wapiga kura msimu ujao

  Exaud Kisamo

  February 2, 2012 at 10:19 PM

 8. kuna siku tanzania itatosheka na dharau hizi za viongozi wetu wasioambilika. mda utanena, kaka zitto tumia unaibu wako wa kambi rasmi ya upinzani kusisitiza ushawishi wangu kwa wabunge wote wa upinzani kutoka nje ya ukumbi wa bunge, endapo hiyo kauli ya serikali haitajadiliwa bungeni. Tuko nyuma yenu wapenda mabadiliko ya kweli Tanzania.

  juma kiolobele

  February 2, 2012 at 10:22 PM

 9. Mheshimiwa Zitto, usikate.tamaa. Kila uongozi una vipaumbele vyake na labda kwa uongozi uliopo Mgomo wa madaktari si kipaumbele kwao. Niombe tu kwamba watanzania wote tuwe pamoja kuiombea Nchi yetu ili awape viongozi wanaoshikilia dola upeo na huruma ili katika shughuli zao waweke maslahi ya taifa mbele kuliko tumbo zao. Hii ni ajabu!!!

  William Js.

  February 3, 2012 at 10:34 AM

 10. Mheshimiwa Zitto hili shwara linasikitisha sana kwa watanzania wa kawaida kwakuwa wanao kufa ni watanzania wa kawaida na viongozi wanaenda kutibiwa nje ya nchi,tuendelee kuiombea nchi yetu jamani

  Allan Shemahimbo

  February 3, 2012 at 3:28 PM

 11. Mh sababu za kutoka nje kwa wabunge wa chadema huwa za msingi ila hii ilikuwa ni ya msingi zaidi kwani kiti cha spika siku zote hakitoi haki na kikitoa haki huwa ni ya kuonesha jamii na wala siyo kutoka moyoni, maoni yangu kwa hili mlipaswa kumuambia spika hatuko tayari kuenderea na mijadara ili hari watu wanakufa jipangeni sisi tunatoka bungeni mpaka tutakapo pata taarifa
  hii na fananisha kwako kuna msiba kwa jirani kuna harusi tena na mziki juu
  hizi si mila zetu
  nakupa pongezi

  Ally lilangela hamis

  February 4, 2012 at 5:14 AM

 12. Wabunge wanasahau kuwa wao walichaguliwa na wananchi kuwawakilisha. wanaenda bungeni kujiwakilisha wao na maslah binafsi ndo maana hata hawaoni shida wanayopata wananchi kwa kuwa kuna tabaka kubwa kati yetu na wao.

  http://mapenziyangu.wordpress.com/

  vicky

  February 4, 2012 at 7:55 AM

 13. ni kweli kabisa limekosa mvuto na hiyo nyongeza ya posho wanataka ya nini? serikali imesema haina hela ya kuwalipa madaktari sasa hizo za posho wanatoa wapi? pambana mheshimiwa ss tupo nyuma yako. together forever comrade

  hamza minangu

  February 5, 2012 at 8:03 AM

 14. Jamani watanzania tuamke sasa na tujue ni aina gani ya wabunge tulionao, na tunaowahitaji, Mh Zitto na Mh Mnyika ni mfano mzuri wa wabunge tunaowahitaji. Haya mazee yamechoka hata kufukiri, uchaguzi ujao tuhakikishe robotatu ya bunge ni vijana!
  Mh Zitto juhudi zako zinaonekana na tupo nyuma yako endeleza mapambano!

  Ussy Madawili

  February 6, 2012 at 9:21 AM

 15. Adaaaa! Bongo watu waoga sana hivi wanamchi tunashidwa kuandamana c 2 tumngojee mbunge aongee kwani wabunge wengine wanazingua big up full polician{zitto}

  By zamimu

  February 8, 2012 at 9:01 AM

 16. Thanks God.Doctors wanaanza kesho.
  dam ya watz iliyomwagika iko mikononi mwa serikali hasa waziri mkuu pinda

  todo

  February 9, 2012 at 7:49 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: