Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

PRESS RELEASE: On Government Austerity Measures-Cut Re-current Expenditure Not Development Expenditure

with 15 comments

PRESS RELEASE

MPANGO WA SERIKALI KUPUNGUZA MATUMIZI

Punguza Matumizi ya Posho SIYO Matumizi ya Reli, Barabara, Elimu na Afya

Mwezi Disemba mwaka 2011 Waziri wa Fedha na Uchumi alimwandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) kumwahidi mambo yepi Serikali ya Tanzania itafanya ili kurekebisha Bajeti yake. Utaratibu huu hufanyika kila mwaka kupitia mpango unaoitwa ‘Policy Support Instrument (PSI). Katika barua hiyo Waziri wa Fedha wa Tanzania ameahidi kwamba Serikali itafanya juhudi kupunguza matumizi ili kuweza kupunguza uwiano wa nakisi ya Bajeti na Pato la Taifa (fiscal deficit to GDP ratio) kutoka asilimia 7.2 mpaka asilimia 6.6 ya Pato la Taifa.

Waziri wa Fedha na Uchumi ameiambia IMF kwamba ifikapo mwisho wa Mwezi Disemba mwaka 2011 (wiki mbili zilizopita) Baraza la Mawaziri la Tanzania limefikia maamuzi ya kupunguza nakisi ya Bajeti kwa kiwango kilichotajwa. Maeneo yanayotajwa ni Pamoja na Miradi ya Maendeleo ambapo jumla ya miradi yenye thamani ya Tshs 157bn itakatwa. Waziri
wa Fedha ametaja miradi hiyo katika Ukarabati na Ujenzi wa Miundombinu.

Kambi ya Upinzani Bungeni inapinga kuondolewa kwa miradi ya maendeleo ili kupunguza matumizi ya Serikali. Kimsingi wakati kama huu ambapo hali ya uchumi ni mbaya na vijana wengi vijijini na mijini hawana ajira tunasisitiza umuhimu wa kutumia zaidi kwenye miradi ya maendeleo.

Punguza matumizi ya kawaida

Kambi ya Upinzani Bungeni inarejea wito wake kwa Serikali kupunguza matumizi ya kawaida ili kupata fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo. Haiwezekani kamwe tukawa Taifa huru iwapo miradi yetu yote ya maendeleo inafadhiliwa na wahisani. Kiwango kidogo tulichokiweka katika Bajeti ya mwaka huu ndicho hicho sasa kinakatwa na hivyo miradi yote ya maendeleo kubakia kwa wahisani ama kwa mikopo au misaada. Kiwango cha Tshs 203bn sawa na 0.5% ya Pato la Taifa ambacho Serikali imeahidi kupunguza ni kidogo mno na kinalenga kuumiza watumishi wa kada ya chini ya Serikali na sio viongozi wakubwa. Bajeti ya Mafunzo inayoenda kukatwa itaumiza Manesi na Walimu au watumishi wanaoongeza ujuzi ili kuboresha kazi zao. Serikali ikate matumizi yote yasiyo ya lazima na hasa posho (360bn), ipunguze matumizi ya magari na yale yasiyo na uhitaji yapigwe mnada na viongozi wote isipokuwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika na Jaji Mkuu washushwe madaraja ya kusafiria kwenye ndege. Safari zote ambazo hazina mahusiano na miradi ya maendeleo zipigwe marufuku kwa muda wote wa miezi sita ya Bajeti iliyobakia.

Serikali ihakikishe matumizi katika Sekta ya Elimu na Afya hayakatwi kabisa ili kuhakikisha tunalinda mafanikio kiduchu ya upanuzi wa sekta hizi na kuongeza uwezo wa Serikali kutoa huduma bora kwa wananchi hasa wa vijijini.

Matumizi ya Maendeleo yasiguswe, yaongezwe

Tayari imeonekana kwamba katika kipindi chote cha nusu ya Bajeti Halmashauri za Wilaya hazijapata fedha za maendeleo. Mfano Halmashauri ya Wilaya Kigoma imepata asilimia 0.3 tu ya Bajeti ya Maendeleo ilhali Halmashauri ya Mji wa Mpanda imepata asilimia 4 tu. Ni dhahiri miradi ya maendeleo kwa maeneo mengi ya vijijini itakwama kwani ni wazi kabisa kwamba Halmashauri hazipati fedha zote za Bajeti ya Maendeleo. Serikali itambue kwamba miradi ya maendeleo sio anasa bali ndio vyanzo vya baadaye vya mapato ya serikali. Miradi ya maendeleo hutoa ajira kwa wananchi na hivyo kuwapunguzia umasikini wa kipato. Jumla ya Tshs 157bn zinazotakiwa kukatwa zisikatwe bali ziongezwe ili kupata fedha za kurekebisha miundombinu kama Reli ya Kati.Kwa mfano Reli ya Kati inahitaji Tshs 200bn katika kipindi cha miaka 3 ili iweze kusafirisha mizigo tani 1.5m kwa mwaka kila siku na kuzalisha faida.

Ongeza Mapato ya Ndani

Inashangaza kwamba katika mpango wa Serikali kupunguza nakisi ya Bajeti mkazo umewekwa kwenye kuondoa miradi ya maendeleo badala ya kuongeza mapato. Nakisi hupunguzwa ama kwa kupunguza matumizi au kwa kuongeza Mapato. Serikali katika Taarifa yake kwa IMF imeibua njia moja tu ya kuongeza mapato, kodi ya mapato kutoka Kampuni ya Geita Goldmine. Huu ni uvivu wa kufikiri.

Serikali imeambiwa mara kadhaa suala la kuanza kutumika kwa sheria mpya ya madini kwa Kampuni za Madini zilizokuwapo. Makusanyo ya Mrahaba peke yake kwa sheria mpya, kiwango kipya na kanuni mpya ya kukokotoa ingeongeza mrahaba mpaka Tshs 203bn kutoka Tshs 99bn za sasa. Kwanini Serikali ianvuta miguu katika kutekeleza hili? Waziri wa Nishati na Madini aliahidi Bungeni kwamba mazungumzo na Kampuni za Madini yanaisha Mwezi Septemba. Mbona Serikali imekuwa BUBU katika hili?

Serikali iliahidi kuangalia suala la mauzo ya mali za makampuni zilizoko Tanzania na kodi ambayo tunapaswa kukusanya, Serikali imekuwa kimya kabisa katika suala hili. Marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa kuondoa msamaha kwenye ‘deemed capital goods yangeongeza mapato ya Serikali kwa kiwango kikubwa na kupunguza mzigo wa
misamaha ya Kodi.

Uwajibikaji kwa Bunge

Inashangaza zaidi kwamba sasa imekuwa ni mtindo kwa Serikali kutoa ‘commitments’ muhimu za kibajeti kwa Shirika la IMF badala ya wananchi kupitia Bunge. Bunge limepitisha Bajeti, mapitio yeyote ya Bajeti yanapaswa kuidhinishwa na Bunge. Bila kufanya hivyo maana ya Bunge kupitisha Bajeti inakuwa haina mantiki na uhuru wa Taifa letu unakuwa haupo kwetu.

Umuhimu wa Bunge kutunga haraka Sheria ya Ofisi ya Bajeti ya Bunge (Parliamentary Budget Act) sasa unaonekana waziwazi. Muswada umewasilishwa Bungeni na Wabunge binafsi kutaka kuundwa kwa mfumo wa kuisimamia Serikali katika Bajeti. Ofisi ya Spika wa Bunge ihakikishe muswada huu unachapishwa katika Gazeti la Serikali mara moja ili usomwe kwa mara ya kwanza katika mkutano wa Sita wa Bunge na kutungwa kuwa sheria katika mkutano wa Saba.

Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali ilete mpango wa kupunguza matumizi Bungeni ili ujadiliwe na kuidhinishwa na Bunge kabla ya kuanza kutumika. Vinginevyo Mpango wa Serikali kwa IMF utakuwa ni kudharau wananchi na kuuza uhuru wetu kwa Shirika la Fedha la Kimataifa. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema mwishoni mwa miaka ya Sabini ‘toka lini Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limekuwa Wizara ya Fedha ya Kimataifa (International Ministry of Finance)?’

Kabwe Zuberi Zitto, Mb

Waziri Kivuli Fedha na Uchumi

Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni (NKUB)

Dar es Salaam, 10 Januari 2012.

15 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Big up Kiongozi.

  sharuvembo

  January 10, 2012 at 5:11 PM

 2. Kazi ni moja kuangalia uhalisia na si itikadi,kimsingi kaka yangu zito ni mzalendo CCM KUBALIN UKWEL VINGINEVYO MNATUUA

  Darison andrew

  January 10, 2012 at 5:11 PM

 3. Kaka Zitto Kabwe, Nakupongeza kwa kazi nzuri inayoendelea kufanywa na kambi ya upinzani bungeni,ingawa Serikali imekuwa kikwazo kwa maendeleo ya nchi.Ninacho penda kukueleza hapa ni kwamba,licha ya juhudi zote hizo za kuifunza serikali utaratibu wa kufanya kazi, jitahidini kuongeza nguvu kazi na sio kuipunguza.Ninamaana punguzeni tofauti kati yenu wawakilishi wa wananchi na vyama vyenu hasa katika mambo ya katiba zenu ili msifukuzane bali kuitumia nafasi iliyopo kutekeleza tuliyo waamini kwayo.Napenda kukukumbusha kuwa muda unakuja tutakapo hitaji breakdown kama hii kwa ajili ya kuweka viongozi wa juu kabisa Serikalini, hasa Rais.
  Salamu kwa wapenda maendeleo wenzangu Tanzania.

  Justin

  January 10, 2012 at 5:16 PM

 4. Nakubaliana na hoja za NKUB. Serikali lazima iwajibike kwa wananchi wake.

  danwelwel

  January 10, 2012 at 5:22 PM

 5. Big up mh ZITTO, Inafurahisha jinsi ulivyo “ACTIVE”

  Juma Kambajeck

  January 10, 2012 at 5:29 PM

 6. Shame on govt,

  Nuru

  January 10, 2012 at 5:32 PM

 7. Hongera Mheshimwa,tukipata walau vijana kama 10 tu bungen kama ww.tutafika mbali,Mungu akupe moyo huo huo wa kizalendo.Endelea kuwaumbua,tuko pamoja kamanda.

  Milka Richard

  January 10, 2012 at 7:43 PM

 8. ok lets pray 2 GOD

  Noel Ernest

  January 10, 2012 at 7:56 PM

 9. Mh. Zitto hoja zako ni za msingi sana na zina mashiko. Binafsi nimejifunza tangu nilipoanza kufuatilia siasa ya Taifa kwamba, utofauti wa itikadi si dhambi bali dhambi inakuja pale unapotumia utofauti wa itikadi kupinga hoja ambazo zina maslai kwa watanzania walio wengi. Ukweli ubakie ukweli ila tusibadili ukweli kwa maslai ya kisiasa. Mh. Zitto kwa nafasi yako ya ubunge na Waziri Kivuli wa fedha na uchumi. Hizi hoja zisiishie kwenye mitandao ya kijamii. Mimi ninaamini Mh. Jakaya na Mh. Mkulo ni waelewa sana na wasikivu. Zungumza nao na uwaeleze kiunagaubaga hoja zako ili hatimaye watanzania tuweze kunufaika. Huu sio wakati wa kulumbana kisiasa. Malumbano ya kisiasa yameisha kilichobaki ni kujenga taifa. Ishaurini serikali kwa utaratibu mzuri bila kejeli wala maandamano. Nguvu ya umma imepitwa na wakati tunachohitaji ni nguvu za hoja kama hizi unazotoa Mh. Zitto. Hongera sana.

  Jabiri Omari

  January 10, 2012 at 9:10 PM

 10. Hii ni serikali sikivu kweli? Kama wanavyo dai wao au hawajui maana ya neno sikivu

  Ally lilangela hamis

  January 11, 2012 at 7:14 AM

 11. Tatizo ni wivu,Wazo katoa nani kama ni mpinzani serekali ailifanyii kazi lakini kama ni mtu wao atakama ni pumba wanaliangaikia.Naamini hipo siku serikali hii itajuta,I believe it.

  Mtalii TZd

  January 11, 2012 at 10:58 AM

 12. […] Punguza Matumizi ya Posho SIYO Matumizi ya Reli, Barabara, Elimu na Afya PRESS RELEASE: On Government Austerity Measures-Cut Re-current Expenditure Not Development Expenditu… PRESS RELEASEMPANGO WA SERIKALI KUPUNGUZA MATUMIZIPunguza Matumizi ya Posho SIYO Matumizi ya Reli, […]

 13. swali kwa Mbuge wetu wa Karagwe; fedha zilizopelekwa anajua kiasi gani. bw Gosibert blandesi anaiua karagwe

  kamugisha

  January 11, 2012 at 6:56 PM

  • blandes is nothing if at all people of that place you do not work up and fight for change things are adamant
   I know him very well so what you have to do you people from karagwe is to stand for change but postive either I happened to be from karagwe once in my life however now am in other place other than krg
   I am with you

   Darison andrew

   January 14, 2012 at 10:54 AM

 14. Hichi ni kichwa laiti serikali ingekuwa inaweza kuchukua mawazo ya wapinzani tungefika mbali

  Rumi

  January 12, 2012 at 11:35 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: