Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Mahojiano ya Zitto Mlimani Tv(Keki ya Taifa) kuhusu Posho za Wabunge

with 4 comments

Mahojiano MlimaniTV Part 1

Mahojiano MlimaniTV Part 2

Mahojiano MlimaniTV Part 3

Mahojiano MlimaniTV Part 4

Written by zittokabwe

December 17, 2011 at 10:52 AM

4 Responses

Subscribe to comments with RSS.

  1. Salaam sana Mh, Kabwe.
    Ni sasa hivi nimemaliza kusikiliza video hii ya keki ya taifa. Mimi ni msomaji wa blog yako na pia nimekuwa nikiandikia email nyingi japo sipati majibu lakini nina imani kuwa huwa unazisoma pamoja na kuwa na majukumu mengi kitaifa. Umemalizia kwa kusema kuwa tusikate tamaa na tuwe na matumaini na taifa letu. Binafsi, sijakata tamaa na taifa letu ila hili la kuwa na matumaini nimeishiwa kabisa kwa sababu zifuatazo.
    1) Tumeshuhudia ufisadi wa kila aina katika kipindi hiki cha miaka 10 hadi 15 ya mfumo wa vyama vingi. Mabilioni ya pesa za umma yanapotea, watanzania wanazidi kuumia kila kukicha, taifa lipo katika giza, ajira kwa vijana imekuwa ndoto na hakuna hatua madhubuti zimechukuliwa dhidi ya wahusika katika mambo haya. Taifa linaongozwa na sheria, sheria zipo ili zitekelezwe dhidi ya waharifu n.k. Unaposema watanzania tuwe na matumaini na taifa letu (viongozi wetu) una maana gani? Mfumo uliopo, viongozi waliopo hawapo madarakani kukidhi haja za wananchi. Tume ngapi zimeundwa kuchunguza ubadhilifu na ripoti zimewekwa wazi ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika wote. Nikukumbushe wahusika wa EPA hasa kagoda mbona wanapeta mitaani, Richmond, ripoti ya Jairo juzi nayo imewekwa uvunguni na hakuna nia ya dhati kuwaadhibu na utekelezaji hatuuoni. Kwanini tuwe na matumaini na viongozi ambao wapo katika mfumo wa kulindana na ni hawa hawa ambao tulikuwa nao katika miaka 50 ya uhuru iliyopita na ni hao hao ambao tunaingia nao katika miaka 50 mingine ijayo.
    2) Kila mwaka CAG amekuwa akiwasilisha ripoti bungeni juu ya ukaguzi wa mahesabu ya serikali na matumizi yake. Lakini kila mwaka kumekuwa na ufushaji wa pesa za umma, ninyi kama chombo cha kuisimamia serikali mmetetea vipi watanzania wanyonge wanaoendelea kuteseka kwa sababu ya wacheche wanaofikiri kwa kutumia tumbo? Hatutaki mambo haya yasemwe kwa maneno tunataka pia maneno yenu yaendane na vitendo. Je, kesho utakuwa tayari kulishawishi bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais kwa kitendo cha kuficha majina ya wote waliorudisha pesa zilizokwapuliwa BOT kupitia EPA? Kilichofanyika ni wizi na wezi wamerudisha na kwa mujibu wa sheria za nchi wezi hawa ni lazima wafikishwe mahakamani lakini Rais ameamua kuweka majina ya watu hawa kuwa top secret. Ni nini kifanyike ili wezi hawa ( ambao ndiyo mapapa wa EPA na mapapa wa Richmond) wafikishwa mbele ya sheria kwa sababu wanajulikana kwa majina.
    Nimalizie kwa kusema kuwa Tanzania ni nchi ambayo imejaliwa tunu nyingi lakini ni ninyi viongozi mnaotufanya watanzania tuwe katika shida zilizopo kwa kuwa nia ya kuwatumika watanzania haipo na hatuna sababu ya kuwa na matumaini na taifa letu iwapo mfumo ni ule ule kwa manufaaa ya wale wale. There is no tomorrow if we continue on the current path “haya ni maneno ye Mh. Tundu Lissu.
    Asante Sana,
    Gent.
    Belgium

    Joshua Bukuru

    December 17, 2011 at 7:41 PM

  2. Salaam sana Mh, Kabwe.
    Ni sasa hivi nimemaliza kusikiliza video hii ya keki ya taifa. Mimi ni msomaji wa blog yako na pia nimekuwa nikiandikia email nyingi japo sipati majibu lakini nina imani kuwa huwa unazisoma pamoja na kuwa na majukumu mengi kitaifa. Umemalizia kwa kusema kuwa tusikate tamaa na tuwe na matumaini na taifa letu. Binafsi, sijakata tamaa na taifa letu ila hili la kuwa na matumaini nimeishiwa kabisa kwa sababu zifuatazo.
    1) Tumeshuhudia ufisadi wa kila aina katika kipindi hiki cha miaka 10 hadi 15 ya mfumo wa vyama vingi. Mabilioni ya pesa za umma yanapotea, watanzania wanazidi kuumia kila kukicha, taifa lipo katika giza, ajira kwa vijana imekuwa ndoto na hakuna hatua madhubuti zimechukuliwa dhidi ya wahusika katika mambo haya. Taifa linaongozwa na sheria, sheria zipo ili zitekelezwe dhidi ya waharifu n.k. Unaposema watanzania tuwe na matumaini na taifa letu (viongozi wetu) una maana gani? Mfumo uliopo, viongozi waliopo hawapo madarakani kukidhi haja za wananchi. Tume ngapi zimeundwa kuchunguza ubadhilifu na ripoti zimewekwa wazi ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika wote. Nikukumbushe wahusika wa EPA hasa kagoda mbona wanapeta mitaani, Richmond, ripoti ya Jairo juzi nayo imewekwa uvunguni na hakuna nia ya dhati kuwaadhibu na utekelezaji hatuuoni. Kwanini tuwe na matumaini na viongozi ambao wapo katika mfumo wa kulindana na ni hawa hawa ambao tulikuwa nao katika miaka 50 ya uhuru iliyopita na ni hao hao ambao tunaingia nao katika miaka 50 mingine ijayo.
    2) Kila mwaka CAG amekuwa akiwasilisha ripoti bungeni juu ya ukaguzi wa mahesabu ya serikali na matumizi yake. Lakini kila mwaka kumekuwa na ufushaji wa pesa za umma, ninyi kama chombo cha kuisimamia serikali mmetetea vipi watanzania wanyonge wanaoendelea kuteseka kwa sababu ya wacheche wanaofikiri kwa kutumia tumbo? Hatutaki mambo haya yasemwe kwa maneno tunataka pia maneno yenu yaendane na vitendo. Je, kesho utakuwa tayari kulishawishi bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais kwa kitendo cha kuficha majina ya wote waliorudisha pesa zilizokwapuliwa BOT kupitia EPA? Kilichofanyika ni wizi na wezi wamerudisha na kwa mujibu wa sheria za nchi wezi hawa ni lazima wafikishwe mahakamani lakini Rais ameamua kuweka majina ya watu hawa kuwa top secret. Ni nini kifanyike ili wezi hawa ( ambao ndiyo mapapa wa EPA na mapapa wa Richmond) wafikishwa mbele ya sheria kwa sababu wanajulikana kwa majina.
    Nimalizie kwa kusema kuwa Tanzania ni nchi ambayo imejaliwa tunu nyingi lakini ni ninyi viongozi mnaotufanya watanzania tuwe katika shida zilizopo kwa kuwa nia ya kuwatumika watanzania haipo na hatuna sababu ya kuwa na matumaini na taifa letu iwapo mfumo ni ule ule kwa manufaaa ya wale wale. “There is no tomorrow if we continue on the current path, haya ni maneno yake Mh. Tundu Lissu”.

    Asante Sana,
    Gent.
    Belgium

    Joshua Bukuru

    December 17, 2011 at 7:45 PM

  3. Hi Zitto,
    Umeongelea juu ya suala la trade deficit na madhara yake katika maisha ya watu ya kila siku, kuporomoka kwa shilingi yetu na impact ya balance of payment kwa taifa. Lakini hutuelezi ni jitihada zipi zimefanywa na serikali katika kupambana na deficit hii, mikakati ambayo imewekwa na serikali kuhakikisha shilingi yetu inapanda thamani na hatua gani zimechukuliwa na ninyi viongozi kupambana na inflation ambayo inazidi kuyawekwa maisha ya watanzania katika hali ngumu zaidi.
    Nikumbushie wakati Kikwete anaingia madarakani, aliingia na kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania, akaaminiwa na mamilioni ya wabongo na akakabidhiwa hatamu za kuingoza nchi. Matarajio ya wengi ni kwamba ndugu huyu amewasaliti watanzania na badala yake yamekuwa maisha bora kwa kila fisadi na maisha magumu kwa kila mtanzania. Najua utajitetea kuwa jukumu hili ni la CCM na ilani yao ya uchaguzi ambayo haikutekelezwa lakini je ninyi kama opposition mlikuja na mikakati gani katika kuinua hali ya watanzania? Why are we importing than what we export to the world market? Sera zetu za biashara hasa juu ya export and import zinasemaje na zina kasoro zipi na zimerekebishwaje?
    Kwa tunu tulizonazo, tanzania hatuwezi kuwa begger, tatizo ni utilization ya tunu hizi na hapa ndipo matatizo yanapoanzia kwa kuwa factors of production zetu zipo idle na serikali hili hailioni hata kidogo. Mimi nadhani wewe kama waziri kivuli wa fedha na uchumi unayo duty ya kuja na plan mbadala ya vipi tuiokoe shilingi yetu, ni vipi tutoke kwenye trade deficit twended kwenye trade surplus, ni vipi tupambane na unemployment kwa vijana na mwisho inflation. Huwezi kutuambia kuwa uchumi unakuwa kwa asilimia 7 kwa mwaka wakati huo huo employment; economic growth should reflect job creation. Sijui ni data zipi ninyi mnazitumia katika kufanya analysis. Lakini ukienda kwenye IMF na worldbank mambo ni tofauti na maelezo ya serikali, sasa nani anasema ukweli?. Akudanganyaye huyo hakuthamini hata kidogo. Huu ndio ukweli kwa serikali yetu.
    Ni hilo kwa leo

    Joshua Bukuru

    December 18, 2011 at 10:13 AM

  4. kaka yote tisa kumi mi napenda kujuwa hivi ni kwanini hii mifuko ya hifadh ya jamii inashindwa kutoa mikopo ya biashara kwa wanachama wake amboyo itaweza kuwaongezea kipato wakatoka kweny huu umasikin badala yake wanakopesha kwa mtajiri wachache ndiyo wanaonufaika na hizo pesa za wavuja jasho wengi wao hawana zamana ya kuweka kwny mabeki lakini kwny hii waoniwanachama na wana michango yao wakiwa kopesha mikopo ya biashara hawa wakawa nakipato halali cha zaidi na mshahara huko ndo kujenga maisha ya baadaye

    Alan

    December 21, 2011 at 11:59 PM

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: