Msimamo wangu: Kupandisha posho za wabunge ni ukichaa na kutojali Hali ya Nchi
Nimeshtushwa sana na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa Wabunge. Nimeshtushwa zaidi kwamba Posho hizi zimeanza kulipwa katika mkutano wa Bunge uliopita kabla hata Rais hajaamua maana maslahi yote ya Wabunge huamuliwa na Rais Baada ya kupokea mapendekezo ya Bunge kupitia Tume ya Bunge.
Wabunge wote watambue kwamba kuamua kujipandishia posho zao bila kuzingatia Hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida ni usaliti usio na mfano. Mbunge yeyote ambaye anabariki Jambo hili au anaishi hewani haoni tabunza wananchi au ni mwizi tu na anaona Ubunge ni Kama nafasi ya kujitajirisha binafsi.
Kwa Wabunge wa Chadema, wajue uamuzi kuhusu posho ni uamuzi wa chama na ni uamuzi wa kisera. Mbunge yeyote wa Chadema anayepokea posho za vikao anakwenda kinyume na maamuzi ya sera za chama tulizoahidi wananchi wakati wa uchaguzi. Nimemwomba Katibu Mkuu wa chama kuitisha kikao maalumu cha Kamati Kuu ya chama kujadili suala hili.
Toka tarehe 8 juni mwaka 2011 nilikataa kupokea posho za vikao. Popote ninapohudhuria vikao huomba Risiti ya fedha ninazokataa. Baadhi ya Wabunge Kama Januari Makamba wamekataa posho na hata kwenye semina ya kamati ya nishati alikataa na tumeona kwenye vyombo vya habari jina lake likiwa limekatwa ilhali viongozi wakubwa kabisa wamechukua posho. Nampongeza kijana mwenzangu kwa uzalendo huu. Nawataka wabunge wengine wenye Moyo wa dhati kukataa sio tu ongezeko hili la posho Bali posho yote ya vikao. Kwa nini mbunge akubali kulipwa kwa kukaa?
Tazama nchi hii, juzi serikali ilipokea Msaada wa tshs 20bn kwa ajili ya Sensa ya mwakani wakati wabunge wanalipwa 28bn Kama posho za kukaa tu.
Tanzania inaagiza gesi ya matumizi ya nyumbani kutoka nje kwa kutumia mamilioni ya dola za kimarekani. Kuwanda cha kutengeneza LPG kinagharimu tshs 35bn tu, Wabunge peek Yao kwa mwaka wanatumia 28bn kwa posho za kukaa tu achilia mbali mishahara na marupurupu mengine.
Ipo siku Watanzania watatupiga mawe kwa usaliti huu dhidi yao.
****
June 10, 2011-Barua: Posho za Vikao
Update: Posho za Vikao- Majibu ya Ofisi ya BUNGE na Uamuzi Wangu (June 11, 2011)
June 19, 2011- SUALA LA POSHO ZA VIKAO: WAZIRI MKUU-ANAPASWA KUCHUKUA HATUA MBILI, AFUKUZWE AU AJIUZULU!
October 10, 2011-#1 Say NO to Posho!
October 14,2011-#2 Say NO to posho!
Natafuta neno zaidi ya ukichaa lakini silipati: yaani Tumeshindwa kulipa madeni ya wazee, tumeshindwa kutoa mikopo kwenye vyuo vya elimu ya juu, tumeshindwa kuzibiti ongezeko la watoto wa mitaani, tumeshindwa kutoa ajira kwa vijana, Tumeshindwa kuwapatia wanafunzi wa shule za msingi japo mlo mmoja kwa siku, kwa kigezo cha serikali haina fedha….. Hii ni dharau kubwa sana kwa wabunge kuongezewa posho wakati kuna wafanyakaziwa muhimu kuliko wabunge, Walimu, madaktari, police, hawa nao vipi? Acheni kucheza na kodi za Watanzania kwakutaka kuwanyamazisha wabunge.
kilewo
November 28, 2011 at 10:39 AM
Nawapongeza sana vijana wenzangu, Kabwe na Januari kama hayo uliyo andika ni YA KWELI, ni suala la Uabunuasi na Umangi meza wa Viongtgozi wetu, kama kweli Miposho hiyo inaongezwa na bado wabunge ambao ni wawakilishi wetu wana pokea na kutia kinywani, ili hali Wananchi wa tanzania wengine wanaishi chini ya dola moja, aibu gani hii. Haya kama hayo hayatoshi, posho zote hizo za nini kama si ulafi wakati kuna mwananchi analipwa shilingi elfu sabini 70,000/= kwa mwezi,
ONYO: hawa wananchi wasio nacho, tena wanao waangalia na kushuhudia jinsi mnavyo tanua na kuneemeka na familia zenu huku mitaani kwa jasho lao. Kuna siku hizo gharama mtazirejesha kwa nguvu za umma tu. Ni kweli wabunge mnahitaji posho ya kutosha, lakini sio kwa muda huu, na kwa hali ya Tanzania ya leo hii, subirini watanzania nao wafike mahali ambapo watasema kweli maisha bora ya mtanzania yanaonekana.
HOFU: Hofu yangu ni kuwa Tanzania hii wananchi kamwe hawataingia vitani kwa sababu za Kiidini au za Kisiasa, bali itakuwa vita kubwa kati ya WALIONACHO na WASIONACHO, sijui muamuzi atakuwa nani, maana wenye nacho hawazidi 2% ya Watanzania wote,
RAI: Rai yangu, kwa viongozi jaribuni kutumia busara kubwa katika kutumia na kugawa RASILIMALI ya watanzania kwa haki na usawa sahihi.
Mungu Ibariki Tanzania
Angolile Rayson
November 28, 2011 at 11:17 AM
[…] kabwe atabili ipo siko watanzania watawapiga mawe wabunge akiwemo yeye. Msimamo wangu: Kupandisha posho za wabunge ni ukichaa na kutojali Hali ya Nchi by zittokabwe Nimeshtushwa sana na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa Wabunge. […]
News Alert: Zitto kabwe atabili ipo siko watanzania watawapiga mawe wabunge akiwemo yeye.
November 28, 2011 at 2:06 PM
[…] kabwe atabili ipo siko watanzania watawapiga mawe wabunge akiwemo yeye. Msimamo wangu: Kupandisha posho za wabunge ni ukichaa na kutojali Hali ya Nchi by zittokabwe Nimeshtushwa sana na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa Wabunge. […]
Zitto kabwe atabili ipo siko watanzania watawapiga mawe wabunge akiwemo yeye.
November 28, 2011 at 2:14 PM
sio muda mrefu asante mbunge Zitto kwa kuling`amua hili
Howard
November 29, 2011 at 12:40 PM
[…] kabwe atabili ipo siko watanzania watawapiga mawe wabunge akiwemo yeye. Msimamo wangu: Kupandisha posho za wabunge ni ukichaa na kutojali Hali ya Nchi by zittokabwe Nimeshtushwa sana na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa Wabunge. […]
Zitto kabwe atabili ipo siko watanzania watawapiga mawe wabunge akiwemo yeye.
November 28, 2011 at 2:14 PM
[…] kabwe atabili ipo siko watanzania watawapiga mawe wabunge akiwemo yeye Msimamo wangu: Kupandisha posho za wabunge ni ukichaa na kutojali Hali ya Nchi by zittokabwe Nimeshtushwa sana na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa Wabunge. […]
Posho za wabunge zapanda kwa 154% kimyakimya! - Page 6
November 28, 2011 at 3:08 PM
Tatizo la watanzia wengi tumezidi ubinafsi. Yaani wabunge wameamua kufanya bunge sehemu ya biashara na si sehemu ya kuwailisha wananchi. We are tired of them..
budida86
November 28, 2011 at 4:23 PM
Hii funga kazi! Wabunge walio wengi wa CCM wametudhihirishia tumewachagua ili wawe wanawakilisha na kupitisha miswada yenye manufaa kwao tu, hawajali kama wananchi tunasambaziwa maji, umeme, elimu, afya, huduma za jamii wala miundo mbinu, wametuthihirishia cha kwanza kabisa bungeni ni matumbo yao, na sio maslahi kwa wananchi wala taifa.
Cha kusikitisha ianonekana ni Mh Kabwe na wengineo wawili watatu tu wasiokubali huu UROHO WA KJINUFAISHA NA PESA YA MLALAHOI!
Sie tunasubiri hio 2015, BASI!
MbongoHalisi
November 28, 2011 at 7:01 PM
Mimi nilishitukia pale tu walipo kataa kodi kwenye posho na wewe mh zitto ulipinga lakini warafi walikataa akiwemo mrafi serukamba siyo kwamba hatuoni mnayo yafanya ipo siku yenu nilikusikiliza kwa makini siku ile ya mdahalo bbc wewe na nkamia hawa jamaa wanatuibia sana wazo kwako tutafutie ushahidi sipendi na wewe useme umeskia ili tujadili kitu ambacho ni kweli na source ukiwa wewe bravo tuko pamoja mkuu
Ally lilangela hamis
November 28, 2011 at 10:21 PM
Na kama ni kweli hata jairo mumemuonea na nakubariana na jamaa kuwa munatumia rungu yenu kuumiza watu wengine kwa vile hawana uwezo wa kujitetea jairo muacheni afanye kazi na hata hatutaki kamati zenu za kinafiki(waziri mkuu alipokea posho za jairo) fikisha na hilo bungeni na ulisimamie ninakukubali sana na nitakukumbusha kwa hili
Ally lilangela hamis
November 28, 2011 at 10:28 PM
Ni msimamo mzuri mheshimiwa, kwa vile wewe ni sauti ya wanyonge, naomba kilio chetu kisike kupitia wewe na vijana kama Januari Makamba. Hakika Nchi imefikia pabaya, kila mtu anaangalia tumbo lake. Wapo watanzania wengi wasio na uhakika wa mlo moja kwa siku. Alafu waheshimiwa wanajiongezea miposho kwa ajli ya kwenda kulala Bungeni, rejea Wasira, Mzee wa ToT, na wengine ambao kamera imetufikishia. Hii sio haki hata kidogo.
Paskal
November 29, 2011 at 1:23 AM
[…] Zitto Kabwe VN:F [1.9.11_1134]please wait…Rating: 0.0/10 (0 votes cast)VN:F [1.9.11_1134]Rating: 0 (from 0 […]
Kupanda kwa Posho, haya ndiyo maoni ya Zitto Kabwe. | Dullonet Tanzania :: Just Call It Solution for News and Information.
November 29, 2011 at 8:26 AM
tanzania tunaubinafsi sana watu hawaangali shida za wengine hii dunia tunapita tuu kila kitu utakiacha so jalini shida za wengine haswa walimu muwepe kipaumbele zaidi.
NOELA
December 7, 2011 at 9:11 AM
binafsi nadhani posho hizi ni asante ya serikali kwa wabunge kwa kupitisha mswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba.hivyo hata zitakapoondolewa watakuwa wameshalipwa asante yao.
rizy winklif
December 14, 2011 at 8:54 AM