Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Uonevu unaoendelea, hatuuoni

with 19 comments

Nimeletewa barua pepe hii kutoka kwa Mwana Mama wa Kitanzania ambaye alipendana na mwanaume raia wa Burundi na hatimaye wakaoana. Baadaye mume wake akafukuzwa nchini. Sijui kama alikuwa na makosa au hapana lakini katika nchi yenye kufuata sheria na haki za binaadamu huwezi kutaraji unyanyasi wa namna hii kufanyika. Nimeombwa kufuatilia suala hili na Mtanzania huyu. Ninalifuatilia ili haki itendeke. Naliweka suala hili hapa ili  kuonyesha aina ya uonevu ambao raia wetu hupata bila sisi viongozi kujua au tunajua na kupuuzia.

Kisa chenyewe hiki (kwa maadili sitaweka majina)

Mheshimiwa,naitwa (jina) mzaliwa wa Kigoma ktk Wilaya ya mpya ya Kakonko.Sote pamoja na mume wangu ni wahitimu ktk chuo kikuu cha Dar es salaam ambapo nilichukua PS$PA na mume wangu 

(jina) alichukua sheria.Yapata takriban miaka mitatu tangu apewe PI jambo lililotufanya kutoka Tanzania na kuja kuishi Burundi pasipo maandalizi.Nasikitika kupoteza mwelekeo wangu wa maisha kwa maslahi ya watu binafsi kwani kwa kipindi chote hicho naishi kama mama wa nyumbani wakati nina elimu.

Mheshimiwa,mume wangu alianza kufanyiwa fitina na maafsa uhamiaji na hatimae kupewa PI,sikuwa na jinsi niliamua kumfuata nchini Burundi.Mpaka sasa siwezi kueleza kosa alilotenda mpaka tukaadhibiwa kiasi hicho.Ilikuwa mwezi wa 6 mwaka 2008 nilipomaliza chuo,tulikwenda kwa mara ya kwanza kutembea nchini Burundi tulipofika Mabamba mume wangu aliwekwa chini ya ulinzi kuuliza kosa gani tumetenda tuliambiwa ni amri kutoka juu,tulitii sheria.Cha kushangaza nilianza kukashifiwa na maafsa uhamiaji,”Ulikosa mwanaume wa kukuoa nchini Tanzania mpaka uolewe na Mrundi?”Sijui alichotaka kufanyiwa mume wangu kwani niligombezwa na kuambiwa nirudi nyumbani wnitafahamishwa juu ya kesi yake ila niligoma.Sidhani kama nchi ya Tanzania huadhibu wanaoolewa nje ya nchi,la hasha!Hata hivyo,tunaomba msamaha iwapo kuna lolote baya huenda tulifanya pasipo kukusudia.

Mheshimiwa,natambua kuwa wewe ni mtetezi wa wanyonge na mwana mabadiliko,naomba ufanye jitihada zako afutiwe PI hiyo,si lazima turudi kuishi Tanzania ila tuweze kuwa na uhuru kuja japo kutembea.Naona uchungu kuja nyumbani peke yangu hasa wakati wa matatizo kama msiba.

Kwa kweli mume wangu alipewa arbitrary PI, tar. 12/06/08 aliwekwa mahabusu kibondo nami nilibaki hapo na mtoto tukihaha. Hakupelekwa mahakamani, alitolewa na kupewa PI.

 Samahani kwa kukuchosha,nimejaribu kufupisha

Mwisho

Inawezekana kuna Wanawake wengi sana wa KiTanzania ambao wameolewa na wanaume ambao si raia na wamekutana na manyanyaso ya aina hii. Natamani kuona Taasisi za kutetea Haki za Wanawake zikifika vijijini ili kuona mateso ya aina hii. Kama kuna kosa mtu huyu alifanya ‘due process’ ilipaswa kufuatwa kwa kupelekwa mahakamani, kusomewa mashtaka, kujitetea na kupewa hukumu. Inabidi kufuatilia kesi ya mama huyu mpaka haki ipatikane. Nitawajuza wasomaji wangu juu ya matokeo ya suala hili. Kazi ya kutafuta Haki ya Mama huyu sasa inaanza……….

Written by zittokabwe

November 24, 2011 at 6:06 PM

Posted in Uncategorized

19 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Ukiacha majiji na baadhi ya manispaa tulizo nayo nchini, wilaya nyingi na vijiji vimetengwa sana na watetezi wa haki za binaadamu na hata vyombo vya habari!
  Vyombo vya habari vina deni kubwa sana katika taifa hili kwa maeneo ya vijijini!
  Mbaya sana hata waeneza dini wamepatupa mkono vijijini!
  Najuta mie!

  Shagihilu

  November 24, 2011 at 6:26 PM

 2. Juzi colleague wangu kaenda home affairs kumlipia mke wake[mwana east africa] dependants pass. Kaambiwa ni $ za kimarekani 520 .Baada ya kulalamikia hili na kutaka maelezo zaidi askari uhamiaji [wa kike]akamuuliza kuwa eti alikua naumbea gani wa kukosa mwanamke wa kiTanzania wa kumuoa! Alifanikiwa kuonana na ofisa wa juu zaidi ambaye amlimjibu kwa mkato kua hio ni sheria.Mimi nauliza ni watanzania wangapi wanaweza hio garama? pili kwanini watu walipishwe kwa USD? Kwani hapa ni Marekani?
  Dada huyo anapata taabu cos nadhani sheria ya Tanzania hairuhusu mwanamke wa kiTanzania aolewe na foreigner halafu waishi hapa mume akiwa na dependent pass. Wanaume ambao sio wa Tanzania wanatakiwa wawe na work permit/resident permit na bei yake nadhani unaijua na vilevile hassle ya kuipata!
  Kwa kweli tunahitaji kupitia[revisit/revise] mambo mengi sana kwenye sheria zetu. Zipo nyingi ambazo wenye nguvu au access na dola wanatumia vibaya kunyanyasa ambao ni wanyonge kwao. Inasikitisha sana, pia hio suala lakutoambiwa kosa! Hio ni haki hata ya muuaji aambiwe kosa lake ni nini!.

  dada mTanzania

  November 24, 2011 at 6:48 PM

  • mi nadhani tunatakiwa kuwa makini na hizi issue tusije tukaifanya tanzania ni sehemu ya kukimbilia! mbona nchi nyingine ni ngumu hata kuoana? kwa nini tusifuate mfumo wetu waafrika kuwa ukiolewa unaondoka kwenda kwa mumeo! kwa nini mumeo akuoe aje kwenu?

   Ngoka

   December 14, 2011 at 8:31 AM

 3. Mheshimiwa Zitto Kabwe,
  Awali nakupongeza kwa kuliweka hadharani suala hili na kuonesha utayari wako wa kulifuatilia. Kwa ujumla kuna manyanyaso mengi ya mfano huo ya raia kwa kuwa tu ni amri kutoka juu. Juu ni kwingi, ni juu gani? Ni jeshi la polisi(Mwema)? Ni Rais? Mkuu wa mkoa? Nk.
  Ombi langu kwako ufuatiliaji wa suala hili na matokeo yake yatoe elimu kwa watanzania wengi, kwa maana ya kuyaweka hadharani yanayowezekana.
  Tumshukuru Mungu pia kwa afya yako njema tena, uendelee na ukombozi wa wanyonge. Mungu akubariki.

  Paskal

  November 24, 2011 at 8:16 PM

 4. na mimi pia mkuu, nimekutana na manyanyaso hayo – si vjijini: hapa DSM kwa makao makuu.

  Swahili Street

  November 24, 2011 at 8:31 PM

 5. Jana colleague wangu mmoja alikua ananieleza yaliyomkumba Home Affairs. Kaenda kumlipia mke wake dependants pass[ni member wa EAC] akaambiwa atoe US$520, miaka yote analipa 120. Akagutuka kuuliza askari wa immigration[mwanamke] akamuambia eti na yeye alikua na umbea gani hado kutooa mTanzania, kwani hapa nyumbani kakosa wanawake wa kuoa?
  1 Je hilo ni swali analopasa kukuuliza wewe mteja
  2. Ndio “customer care” ya serikali yetu
  Jamaa yangu huyo akafanikiwa kuonana na afisa wa juu zaidi ili apate kueleweshwa kulikoni hio gharama, afisa yule jibu likawa la mkato kuwa imeshakua sheria, basi. Maswali yangu yanaendelea:-
  3.Kwa mara ya pili points namba 1+2 hapo juu ndio policy ya serikali yetu?
  4. Mtanzania wa kawaida anaweza kumudu gharama hizi? GNP yetu yenyewe ya mwaka yafika hizo dola ngapi? Statistics za 2005 ni US$ 350
  5. Kwa nini mTanzania nilipe kodi/gharama nk kwa serikali yangu kwa fedha za kigeni? Hivi pesa ya Tanzania pale chini si imeandikwa kua ni “Legal tender”? na nchi zote za nje serikali[zenye uchumi uliosimama au fedha zenye thamani kwenye sokowanapokea pesa za nchi sio za kigeni.
  Pia kuhusiana tena na suala hili la uhamiaji na kuonana, eti ninavyoelewa mimi mwanamke wa kiTanzania hana haki ya kuwa na mume ambae si raia , wakaishi wote hapa kwa dhamana ya [mwana]mke yule.Kwani wanawake ni raia nusu? mbona familia nyingi za kiTanzania [baba na watoto]zinalelewa na akina mama? Kwa hio huyo mume lazima awe na Resident permit/work permit ambayo mim na wewe tunafahamu shughuli pevu ya upatikanaji wake!na Bei yake hio ni US$2000 nafikiri kwa hali ya sasa . Kwa mpango huu serikali inatuambia nini sis wananchi[wanawake]?Inabidi tuangalie kwa makini masuala kama haya, issue za uonevu/kutokuwepo na uwazi, usawa na haki zipo nyingi. Na wenye dhamana za hizo ofisi husika lazima waelewe kuwa sisi wananchi ni wateja wao, ndio tuna “waweka mjini” kwa hio tuheshimiane, ni kitu cha bure! Kila mtu atende wajibu wake halali, kwa staili hio tutafika na si vinginevyo.
  Halafu pia serikali yetu ijiulize kwa mwendo huu wanafukuza wananchi wangapi tena wenye uwezo mkubwa wa kuchangia maendeleo na uhai wa nchi yetu?
  Mwisho, naomba nitoe Pole nyingi kwa huyo dada, natumaini tatizo lake litapatiwa ufumbzi ingawa atakua ameshapoteza mengi.

  dizaina (@dizainatweets)

  November 24, 2011 at 9:35 PM

 6. Mh, huyo mama anasikitisha sana,anyway hatujui kilichojificha hapo lakini msaidie kadri uwezavyo tujue nini tatizo.kazi njema

  Mahenge

  November 24, 2011 at 11:50 PM

 7. Inawezekana kuna Wanawake wengi sana wa KiTanzania ambao wameolewa na wanaume ambao si raia na wamekutana na manyanyaso ya aina hii. Natamani kuona Taasisi za kutetea Haki za Wanawake zikifika vijijini ili kuona mateso ya aina hii. Kama kuna kosa mtu huyu alifanya ‘due process’ ilipaswa kufuatwa kwa kupelekwa mahakamani, kusomewa mashtaka, kujitetea na kupewa hukumu. Inabidi kufuatilia kesi ya mama huyu mpaka haki ipatikane. Nitawajuza wasomaji wangu juu ya matokeo ya suala hili. Kazi ya kutafuta Haki ya Mama huyu sasa inaanza……….

  Sugel

  November 25, 2011 at 6:56 AM

 8. INasikitisha kuona manyanyaso ya utaifa tena kwa maslahi ya watu wachache,Mh Zitto tupo pamoja kushughulikia suala hili na mengine yanayoendana na hili,Mungu awape roho ya ujasiri wote wanaonyanyaswa na kuonewa

  Gerrard Kihiyo

  November 25, 2011 at 11:53 AM

 9. Hii inaonyesha jinsi gani watu wa UHAMIAJI walivyo miungu watu. Nadhani ifike mahali sasa hawa watz watambue haki zao na hili wakubwa wanalijua na ndio maana hawataki kuweka somo la Katiba katika mitaala ya elimu kuanzia shule za msingi ni kwa kuogopa wananchi wakijua haki zao basi kuwanyanyasa itakuwa ngumu. Mh. Zitto fuatilia hilo jambo na tafadhali utueleze kila process unayoipitia.
  Barikiwa sana.

  Simon

  November 25, 2011 at 11:56 AM

 10. Hiyo inaonesha kuwa ccm ni tatizo kila mahali.

  Kibona

  November 25, 2011 at 12:12 PM

 11. Kaza mwendo mheshimiwa,tunahitaji watu kama nyie ktk nchi yetu. Mungu akubariki.

  Godwin Muganyizi

  November 25, 2011 at 12:15 PM

 12. Duu! Inatia uchungu sana kuona baadhi ya maofisa wa uhamiaji kufanya kazi zao kibabe. Mh jitahid umsaidie uyo mdada apate haki yake. Uhamiaji ni wanyanyasaji kama walivyo askari wa wanyapori.

  Rumanyika

  November 25, 2011 at 12:48 PM

  • Inasikitisha sana yani tungepata watu kumi kama wewe Mheshimiwa Zitto nchi yetu ingekuwa mstari ulionyooka kaza mwendo hawa wapate haki zao.

   Hadija

   November 25, 2011 at 4:15 PM

 13. Mh. fanya suala la huyo mama ili uwakomboe wakina mama manake wanazidi kukandamizwa na sheria za kuwalinda zipo na kaz yenu kubwa ni kukutea haki za wanyonge…..!

  Malongo

  November 25, 2011 at 3:54 PM

 14. Nami pia nakupongeza sana muheshimiwa kwa kuwaeleza wananchi wako kuwa utalifuatilia suala hili,
  Kwa mkoa wa Kigoma tatizo hili limewakumba wengi Na sijui ni kwanini?tunahitaji huu mchezo mchafu uishie hapo,Pia mashirika binafsi yanayo shughulika na mambo kama haya sijui yanafanya nini hapa nchini?,Endelea kulifuatlia mpaka mwisho.

  Juma

  November 25, 2011 at 4:12 PM

 15. Mh Zitto u are so great kwa haki zetu wakina choka mbaya. Komaa nayo hiyo issue ya huyo dada etu hadi kieleweke. Kama ulivosema ‘due process’ haikufuatwa. Amri kutoka juu maana yake nini jamani??????? Embu kiongozi wangu nisaidie kujua p’se. Msaidie dada etu mungu atakulipa ujira ulio mwema inshaallah. Ubarikiwe Zitto(JEMBE LA KAZI).

  juma kiolobele

  November 25, 2011 at 5:52 PM

 16. Kwa kweli watanzania tumezidi kuwaonea wageni wetu. Hivi PI zinatolewa tu kiholela kama njugu? Mahakama zetu zimedharaulika kiasi hiki? Na kwa nini hao maafisa uhamiaji wasiadhibiwe kama hawawezi kulinda heshima ya nchi yetu kwa kuwatendea vema wageni wasio na hatia? Mheshimiwa Zitto, nakuomba usambaze issue hii ya Mrundi huyo msomi aliyetelekezwa kama mnyama pori na familiya yake kuhaha bila kosa lolote, mpaka kieleweke! Lazima hatua kali zichukuliwe dhidi ya wote waliohusika katika unyama huu. Tena ikibidi Mrundi huyo atafutwe alipo ili apewe fidia maana inaonekana alinyanyaswa pasipo sababu. Mwenyesi Mungu akutangulie katika vita vya kukomesha uonevu.

  John Kimaro K.

  December 15, 2011 at 3:40 PM

 17. Issue hii imeishia wapi?Ama ndo imefisadiwa tayari?

  Neema Hamisi

  June 14, 2012 at 5:49 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: