Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Ripoti/Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge(“Ripoti ya Jairo”)

with 13 comments

TAARIFA YA KAMATI TEULE YA BUNGE ILIYOUNDWA KUCHUNGUZA UHALALI WA UTARATIBU WA WIZARA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA KUPITISHA BAJETI BUNGENI

(Eng. Ramo Matala Makani, Mb.)
MWENYEKITI
KAMATI TEULE YA BUNGE
Novemba, 2011

View this document on Scribd

 

 

13 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Nchi imegubikwa na vitendo vya kilaghai, na kulindana. Vyombo husika havifanyi kazi yake, na mishahara wanapokea-ambayo ni kodi zetu wananchi. Hapa nazungumzia TAKUKURU na wengine wa namna hiyo. Utaratibu wa kutumia kamati za bunge kufichua uozo ni effective na mzuri, lakini unaongeza gharama, kwani wanafanya kazi ambayo ilipaswa kufanywa na taasisi zenye watu wanaopokea mishahara ili kufanya kazi hizo.

  Tuurejee nyuma, tufikiri zaidi.

  Arnold Temba

  November 21, 2011 at 9:43 AM

  • Naunga mkono maelezo yako.Tatizo wanaolipwa mshahara kwa kazi hiyo hawapo huru wanafanya kazi kwa maelekezo ya kuficha ukweli

   oscar elia

   November 21, 2011 at 6:34 PM

  • Kaka Arnold ulichosema ni ukweli mtupu! Ni kweli kuwa kamati za bunge zinafanya kazi nzuri na tunaikubali lakini zinaongeza gharama zisizo za lazima kwa nchi/watanzania/walipa kodi yaani sisi! Anayenisikitisha zaidi ni CAG hasa kwa report yake ya kwanza ambayo ali prove kuwa hapakuwa na any fund mismanagement kwenye hiyo wizara. Nimepata mshangao kuona majibu yake kwa kamati hii ambayo yanapingana na dondoo zilizotumiwa kumrudisha Jairo ofisini na katibu mkuu kabla kamati haijaundwa. Jamani usanii na kulindana kumezidi mpaka professional zinawekwa pembeni watu wanaweka maslahi binafi na kichama yanawekwa mbele. Watu kama CAG ni professionals lakini washachakachuliwa!!

   MOG

   November 21, 2011 at 9:53 PM

 2. Baada ya kusoma yote haya nimebaki na swali moja tuu kichwani WATANZANIA TUTAFIKA KWELI NA KAMA TUTAFANIKIWA KUFIKA NI LINI HILO LITATOKEA? Viongozi wetu wameshiriki na kuwa wadau wa mbele katika kudhoofisha kama si kuua demokrasia na kuendeleza ufisadi ulio wa wazi bila hata ya kuwa na uoga wowote. Karne ya Sayansi na Teknolojia sisi tunaingia na Ulaghai, Ubabaishaji na Ufisadi huku taasisi zote za kudhibiti halii hiyo zikiwa macho bila ya kuweka pingamizi lolote. Huu ni MSIBA.

  idris

  November 21, 2011 at 10:21 AM

  • Nyerere – nchi iliyotikiswa haiwezi fika, na ikiwa itafika haitakuwa salama!

   Makaveli

   November 21, 2011 at 2:46 PM

 3. jembe la ukwel linapiga harakati za kwel

  wiston mogha

  November 21, 2011 at 10:49 AM

 4. ILA IPO CKU MWENYEZI MUNGU ATASHUSHA HUKUMU YAKE KWA HAWA VIONGOZI WE2,SERIKALI YE2 IMEKUWA NI YA KUJUANA SANA.

  Idrisa

  November 21, 2011 at 11:00 AM

  • Ndg yangu Idrisa sitaki kusema natofautiana na wewe ila nisisitize kwamba Mwenyezi Mungu tayari amekwisha toa hukumu kwa viongozi wasiowaadilifu, serikali na CCM kwa ujumla. Japokuwa hilo halionekani kwa macho ya kawaida, ukiwa makini utaona ipo kila dalili ya wazi kwamba Mungu ashatoa hukumu kwa viongozi hawa, serikali pamoja na chama chao. Mnyukano ulio ndani ya chama chao, uelewa tulio nao wa-Tanzania leo na jinsi ambavyo uovu wa serikali unabainika kila kukicha pasipo serikali na chama kuchukua hatua dhidi ya waovu na maovu yao ni baadhi ya dalili za hukumu.

   Utekelezaji wa hukumu hii uko mikononi mwetu sisi Watanzania. Wengi wetu tunajua mda si mrefu hukumu hii itatekelezwa. Hata hivyo dalili zinaonyesha bayana kuwa utekelezaji wa hukumu hii hautatokea bila garama (sitaki kusema ni garama gani!) ambazo hazina budi kutimizwa.

   Kila nikikaa chini nikaanza kutafakari nchi yetu inakopelekwa nasikitika sana. Ninapokutana na bibi zetu au vikongwe popote pale, mara zote machozi yananilenga. Bibi hawa, pamoja na shida zote na umaskini mkubwa walionao, amani imekuwa ndo kitu pekee kilichokuwa kinawapa faraja. Hata kama wakilala njaa, bado uwepo wa amani uliwapa faraja. Lakini inavyoonekana amani itapotea mda si mrefu-kila mtu ni mashahidi juu ya hili.

   Inasikitisha sana pale unapoona viongozi wetu, ambao tuliwaamini kuwa watatuongoza vizuri na kwa namna ya kuitunza hii tunu adimu aliyotujalia Mwenyezi Mungu, wanaposhindwa kuzisoma dalili hizi, na hasahasa sababu zilizonyuma ya dalili hizi kuelekea kuvunjika kwa amani yetu Watanzania. Napata wasiwasi kuona viongozi wetu wanashindwa kujikita kwenye hoja za msingi (kama katiba na nyingine nyingi) na badala yake wanaamini kwamba jeshi la polisi (pengine na majeshi mengine) yanatosha kulinda amani yetu. Wamepotoka.

   Naililia Tanzania yangu…

   Riami

   November 22, 2011 at 10:39 AM

 5. Tanzania yenye neema ya kila aina kama vile rasilimali,utulivu na amani.Naililia Tanzania,Nakupenda Tanzania.

  Laban Muttamwega

  November 21, 2011 at 11:54 AM

 6. Kisha kwa mshangao mkubwa hamtaona rais akitekeleza maagizo ya bunge na wabungewote mtanyamaza kimya.

  Jimmy Kalugendo

  November 21, 2011 at 1:56 PM

 7. Uti wa mgongo wa hii nchi kwa sasa ni rushwa,sio kilimo

  Dastan Kweka

  November 21, 2011 at 9:03 PM

 8. kwavile uchunguzi umekamilika hawa wote washtakiwe na wafungwe! na mafixadi wote wauawe kwani kunahaxara gani wakiea wote mbona Nyamongo vijana wamekufa??

  Oscar Baruti

  November 22, 2011 at 3:54 PM

 9. Kuna MENGI yakuwasiliana na kupeana katika kujengeana uwezo . je? tunaweza kupata Emails za Mh. ZITTO KABWE,Mh. SILAHA ,Mh. MBOWE , Mh. MDEE , Mh. MNYIKA na Wabunge wengine wa kuweza kuwa tayali kubadirishana nao mawazo?

  FISHERS UNION ORGANISATION - FUO

  April 14, 2012 at 6:38 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: