Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Walipa Kodi 15 Wakubwa Tanzania (Tanzania Top 15 Tax payers) & the missing household names

with 39 comments

Kutoka Hotuba ya Waziri Mkuu 26.08.2011 – Makampuni yanayoogoza kwa kulipa kodi

Note: (Highlights)

Only one Mining company (the smallest ie Resolute Mining), only one telecom company(Airtel Tanzania).

Household names like MeTL, Bakhresa/Azam, IPP, VodaCom, Coca cola, Pepsi(SABCO), Serengeti Breweries, Barrick Gold, AngloGold Ashanti not seen. No oil marketing companies pia.

One can conclude that, TBL is the most profitable company in Tanzania, NMB is the most profitable Bank.

 A public debate is needed.

Here under is the an extract from the Prime Minister speech;

Mheshimiwa Spika,

1. Nitumie nafasi hii kuwapongeza baadhi ya Walipakodi Wakubwa kwa Serikali na ambao wamefanya vizuri kati ya kipindi cha mwaka 2005 na 2011. Kwa kipindi hicho, Makampuni yaliyoongoza kwa kulipa kodi ni pamoja na:

i.              Tanzania Breweries Ltd. (Shilingi Bilioni 165.4);

ii.            National Microfinance Bank (Shilingi Bilioni 108.6);

iii.           Tanzania Cigarette Company (Shilingi Bilioni 92.1);

iv.            National Bank of Commerce (Shilingi Bilioni 89.9);

v.            CRDB Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 79.2);

vi.           Tanzania Ports Authority (Shilingi Bilioni 76.8);

vii.          Tanzania Portland Cement (Shilingi Bilioni 73.4);

viii.        Airtel (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 63.6);

ix.           Tanga Cement Company Ltd. (Shilingi Bilioni 43.6);

x.            Standard Chartered Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 40.0);

xi.           Citibank (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 35.7);

xii.          Resolute (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 32.1);

xiii.        Tanzania International Container Terminal Services (Shilingi Bilioni 25.9);

xiv.         Tanzania Distillers Ltd. (Shilingi Bilioni 13.4); na

xv.          Group Five International (PTY) Ltd. (Shilingi Bilioni 9.5).

2.  Napenda kutoa rai kwa Makampuni yote Nchini kuiga mfano huu mzuri. Wito wangu kwa Makampuni, Wafanyabiashara Wakubwa kwa Wadogo na Wananchi wote ni kuongeza juhudi katika kufanya biashara zao ili zizalishe kwa wingi na kupata faida kubwa zaidi. Faida kubwa itachangia katika kuongeza Mapato ya Serikali kwa njia ya Kodi na hivyo kusaidia kukuza uchumi, kuongeza Pato la Taifa na la Mwananchi mmoja mmoja na kuondoa Umaskini. Niwadhihirishieni kwamba, Serikali inatambua umuhimu wao kwa maendeleo ya Nchi yetu na itahakikisha inaongeza juhudi zake za kuweka Mazingira Wezeshi kwa Makampuni hayo kufanya shughuli zao vizuri ili kuwezesha kulipa Kodi kwa mujibu wa Sheria.

Written by zittokabwe

August 26, 2011 at 8:29 PM

39 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Mi nafikiri ku Conclude kuwa “TBL, NMB etc are more Profitable” badala yake inaonesha jinsi gani Serikali kupitia TRA isivyo makini katika ‘Tax Adminstering’ iweje makampuni makubwa ya madini na baadhi ya traders wasimepo katika List huu unaweza kuwa ushahidi tosha ukosefu mkubwa wa umakini katikakukusnya kodi hivyo kuendelea kupata mapato madogo kwa taifa letu, kwa mtindo huuuu hatuwezi kufikia Vision ya Tanzania kuwa na Uchumi wa kati ifikapo 2025 utabaki kuwa ni ndoto kama kodi ambayo ni kiini cha Public Finance itapuuzwa kiasi hiki.
  My Suggested Solution
  Kubadili mfumo wa kuogopana , watu wawajibike ipasvyo na watu wapew elim ya uzalendo ya kuwa nauchungu wa nchi yao, Tanzania inaendelezwa na Watanzania Wenyewe na si vinginivye ni kuanza kusimamia rasirimali zetu na kukusanya kodi among Others. I
  Baada ya kusema hayo naomba kuwasilisha

  Finias Dogeje

  August 26, 2011 at 8:59 PM

 2. Jamani 2mekwisha waalimu kila mwezi kodi makampuni makubwa wala!!

  Salome Magesse

  August 26, 2011 at 9:02 PM

 3. maskini ya Mungu naskitika sana kuona hata GGM sio miongoni mwa walipa kodi wakubwa hii inaonyesha jinsi taifa linavyopoteza mapato mengi,kiukweli inasikitisha kwa waziri mkuu kuthubutu kuutangazia umma jambo kama hilo huu ni uthibitisho kuwa serikali ya CCM ni legelege

  Prosper mallya sharpville

  August 26, 2011 at 9:04 PM

 4. Ni vema ikajulikana, kwanini kampun hizi kuu za uchimbaji madini zenye habari zinazogonga vichwa vya watu kila mara kwann hazipo kati list hii GGM na kampuni ya barrick kwa migodi ya siku nying kama kmcl, kwanini hawalipi kodi? Kwa uapnde mwingine serikali inafaidika na kodi ya wafanyakazi wa kitanzania wafanyao kazi katika migodi hiyo tu bili mwekezaji mwenyewe kulipa kodi, nini faida yake? Mbona pia mishahara ya wafanyakazi hao haiboreshwi kufikia kiwango kidhi, utofauti wa mishahara ya wageni na wazawa ni tofaut sana pia wageni wengi wamechukua nafasi zinazowafaa wageni, ni lini sekta hii ya madini itakuwa mkombozi kwa mtanzania na taifa kwa ujumla??

  Mayeye

  August 26, 2011 at 9:11 PM

 5. Safi sana
  MH. Mbunge
  ZITTO KABWE
  kwa kutufungua masikio
  pamoja na mabilioni yote hayo
  lakini za maisha ya WATANZANIA ni hatari tupu
  hivi sasa naenda kulala kakini mkononi nina TSHS 1500/= tu
  na nina watu watano wanaonitegemea
  je itakuwaje?
  Tusaidie

  Dominicus Mchilo

  August 26, 2011 at 9:12 PM

 6. Ajira zinazo wafaa wenyeji

  Mayeye

  August 26, 2011 at 9:14 PM

 7. this ia serious mweshimiwa zittto. kampuni kubwa kama vodacom, inazidiwa na airtel, au resolute kulipa kodi kubwa kuzidi, barrick am really puzzled, as an economist, have tried to use my small knowledge of econometrics its does not it make sense, but ur in the committee please open my mind.

  will feel desperate if i wont get a favorable answer.

  Thank you
  Erick

  Erick Ifunya (@eifunya)

  August 26, 2011 at 9:23 PM

 8. Serikali yetu itabidi ifanye jitihada za dhati kubaini vyanzo vya mapata vingine, tanzania ni watu laki tisa (900,000) kati ya milion 40 ndio walipao kodi, wenzetu kenya walipakodi ni takriban milion 10. Vitambulisho vya uraia wa taifa vishughurikiwe kila mtanzania mwenye umri wa miaka 18 abainike na afatiliwe, hii itajenga ile hali ya kufanya kazi kwa bidii.

  Misamaha ya kodi ipungunzwe then mikataba migodini iangaliwe vyema!

  Suitbert

  August 26, 2011 at 9:25 PM

  • hapa umenena, unajua Tanzania inajengwa ni sisi wenyewe sasa kukaa unanyoosha kidole kila siku ipo siku nawe utanyooshewa. Kila mtu play part yake. Lets be solution thinkers and implementers. Sasa kama Laki 9 ndio walipa kodi je wanaotegemea kuhudumiwa ni wangapi? Anae saidia makampuni kukwepa kulipa kodi ni nani?Mimi nadhani ni mtanzania kama wewe na mimi.
   So jamani tuwajibike na sio kuwa bingwa wa kunyoosha vidole tu.
   Ahsante

   Ally Nchahaga (@anchahaga)

   August 28, 2011 at 6:49 AM

 9. Serikali yetu itabidi ifanye jitihada za dhati kubaini vyanzo vya mapata vingine, tanzania ni watu laki tisa (900,000) kati ya milion 40 ndio walipao kodi, wenzetu kenya walipakodi ni takriban milion 10. Vitambulisho vya uraia wa taifa vishughurikiwe kila mtanzania mwenye umri wa miaka 18 abainike na afatiliwe, hii itajenga ile hali ya kufanya kazi kwa bidii.

  Misamaha ya kodi ipungunzwe then mikataba migodini iangaliwe vyema! Serikali ipunguze mizaha ktk mipango ya maendeleo!

  Suitbert Maro

  August 26, 2011 at 9:26 PM

 10. Ama kweli kwa mwenendo huu mustakbali wa amani yetu uko mashakani, nasema hivi kwa sababu katika mazingira haya ambapo makampuni makubwa nchini kama ya madini ambayo yanatupa mrabaha wa asilimia 3 katika kile wanachokivuna leo hawalipi kodi? Bakhressa kampuni ambayo mtanzania huwezi kupitisha siku bila kununua bidhaa toka katika makampuni yake naye halipi kodi? Hii inadhihirisha namna ambavyo maafisa wa TRA wanavyochuma pato haramu kupitia hongo na rushwa ili kuyasaidia kiujanjaujanja makampuni haya yasilipe kodi. Ajabu na kweli hata Vodacom kampuni ambayo kwa taarifa za chini ya carpet iliweza kuanzisha mtandao nchini DRC baada ya kuvuna mabilioni ya fedha kutoka kwa masikini wa nchi hii katika kile walichokiita VODA MILIONEA nao wanakwepa kodi? KATIKA HILI NI BUDI KUWE NA MJADALA WA KITAIFA KUHUSU HAWA JAMAA JASHO LETU WALIPELEKA WAPI? la sivyo pengo la walionacho na wasionacho litaongezeka na mwishoe Mungu atuepushie LAZIMA nchi itaingia katika machafuko

  SAIDI MSONGA

  August 26, 2011 at 9:37 PM

 11. MH ZITTO, Sisi watanzania tunaomba ninyi wanaharakati wa kweli hususani CHADEMA muandae haraka mjadala wa Kitaifa kuhusu hili kama mlivyofanya kwenye KATIBA Haiwezekani METL, IPP,SSB/AZAM, MIC,VODACOM, BARICK, TOTAL,OILCOM,LAKEOIL,BP nk wazidiwe malipo ya kodi na TCC. Tusikubali kamwe! Nasubiri jibu. JUMA KAMBAJECK

  JUMA KAMBAJECK

  August 26, 2011 at 9:46 PM

  • If yo contribute high to ccm burget when you are i n tax holiday then you get tax exemption to your business, thats how it is

   ndebile

   August 29, 2011 at 3:17 PM

 12. Mzee we ni kichwa ila me nilitegemea wale tuliowauzia wanyama (twiga) pamoja na wale wanaotaka kubomoa jengo la court of appeal ndo waongoze kwa kupay tax kumbe teh…teh…teh,

  Chambo isaack

  August 26, 2011 at 10:32 PM

 13. jamani naona hata aibu kusema mimi mtz

  Swago

  August 26, 2011 at 10:47 PM

 14. I am really shocked! I do not know what to say! Nahisi kuna watu wakubwa wanafaidika na haya mambo yanayoendelea! Thank you for sharing Zitto!

  Mercy Byera

  August 26, 2011 at 11:13 PM

 15. kwa kweli nashindwa kuelewa viongozi wa nchi hii wanafanya nini! haihitaji kwenda shule kujua kuna ukwepaji mkubwa wa kodi tena wa wazi,taarifa nlizonazo mby cement ni cha pili kwa uzalishaji wa cement nchini sasa 2waulize wakusanyaji wa kodi hyo cement inayozalishwa huwa inamwagwa ndo mana haitozwi kodi. sitaki kuamini watanzania wanavuta sana sigara kuliko kunywa vinywaji vya SBC au COCA,ni suala lililo wazi vodacom ni mtandao unaoongoza kwa wa2 ku2mia huduma zake lakin eti kodi yao haifiki kwa airtel!! huu ni utani ambao hatuwezi kuuvumilia tena!! watanzania tumechoka!! Mh Pinda shame on you and your government.

  Ramadhani Rashid

  August 27, 2011 at 1:47 AM

 16. Kweli ni jinsi gani inaonesha serikali ya ccm haiko makini na si sikivu kama wasemavyo yaan huu ndio udhaifu wao katika kukusanya kodi?kazi yao ni kukata kodi kubwa kwa wazalendo huku wagen wakifaidi nchi yetu jaman hakika taifa halijui lielekeapo
  Asante

  Saul

  saul mpock

  August 27, 2011 at 2:02 AM

 17. Siyo kwamba haya makampuni hayalipi kodi
  bali pana mazingira ya RUSHWA hapo
  watumishi wenye dhamana ya kukusanya kodi wanachukua chao mapema

  Dominicus Mchilo

  August 27, 2011 at 3:48 AM

 18. hapo ndo ujue kuwa kuna watu hawafuatiliwi kwenye ulipaji wa kodi mana hamna kweli mining company hata moja kwani hizo zote zina exempt kwa kila kitu?

  Innocent

  August 27, 2011 at 10:57 AM

 19. MH.ZUBERI K.Z,kwanza ahsante kwa kutufungua,ila ninakushauri 2015 ugombee URAIS kwa tiketi ya chama chako,kwasbb unasifa zote,unaakili sana.big up!

  Salum Said

  August 27, 2011 at 3:09 PM

 20. Hivi kulipa kodi watu wanapewa hongera? Mimi nilizania ni wajibu wa kila mtu na mfanya biashara kulipa kodi kutokana na % uliyopata?

  Badala ya hongera ingekua tunataka tuone vitabu vyao ijulikane walivyorecord mapsto yao. Kampuni zinatengeneza hela lakini hazionyeshi kila kitu na zinaachiwa tu. That is just so sad.

  Ndio maana watu wanasema Tanzania ni ngumu kupata kibali kufanya biashara kama wewe si raia lakini once umepata kibali nenda na gunia la kupark hela. It to make money and so easy to take that money out of the country without paying a penny.

  Sara

  August 27, 2011 at 6:07 PM

 21. Let’s be serious ina maana artel imetengeneza hela nyingi kuliko hii company nyingine ya simu? Niliona hiyo co. Ilifanya patry dodoma na viongozi walikua wanasakata rumba nikajiuliza at what cost?
  For profit company inakwenda kufanya party kwa legal makers ili iweje? Mwisho wa yote wale wasiokula na kipofu ndio wanalipa kodi kihalali na kupongezwa hadharani. Hao wengine wanapingezwa huko kwenye party.

  Na sisi wananchi tuipende nchi yetu ningekua bongo ningenunua huduma kwa hayo makampuni yaliyotajwa hapo. Kila mtu ajifanya hivyo labda watajufunza. Unazania hao wakwepa kulipa kodi wanajali kuwa praised on public or not. As long they’re making money, don’t pay tax, don’t get procuted,they don’t care.

  I thought avoid paying tax is a crime. I guess not in Tanzania.

  Kenny

  August 27, 2011 at 6:27 PM

 22. Good. Kumbe tuna makampuni mengi yanayoiba tu na kwenda zake. Hilo naomba wabunge na wengine tuliowapa jukumu hilo mlifuatilie.

  Mimi kama mwananchi mlipa kodi ambaye mshahara wangu unakatwa kodi kila mwezi, NATANGAZA MGOMO WA KUNUNUA AMA KUTUMIA HUDUMA ZA MAKAMPUNI YASIYOLIPA KODI. Over.

  Godfrey

  August 27, 2011 at 7:23 PM

 23. Ni kweli hilo usemalo je macampuni ya madini yako wapi?ambayo kwa kiasi kikubwa yangepaswa kuongoza katika ulipaji wa kodi kwa hakika nchi hii bado iko katika majaribio tangu uhuru kwan mfano mzuri ni leo muitikadi wa ccm bwana Nape alipo dhihirisha katika mdahalo kuwa hakuna aanzae kwa hatua mia lazima moja iaanze sasa ni 50 yrs ya uhuru bado tuko katika majaribio iwe elimu,afya,siasa nk japo kltk siasa mfumo tulio nao walau ndo unaonekana sasa kutufikisha hapa tulipo hata kugundua haya yaliyo chimbiwa kapuni muda mrefu,tena Ruhanjo abanwe nae azungumze hiyo kawaida ya kuchangia pesa ili ipitishwe zinatumika wapi?hii ni hatari sana watanzania

  SI KWELI HII

  August 27, 2011 at 11:56 PM

 24. Mi nadhani haya makampuni yange tengwa katika makundi matatu, makampuni makubwa, ya kati na madogo alafu iyo list ya makampuni yanayo ongoza kwa kulipa kodi yange listiwa 15 kwa kila group. Na wananchi tuyatumie katika kufanyanayo biashara, nikimaanisha anayekwepa kulipa kodi bidhaa zake zisinunuliwe pia hauwezi kulipambanisha kampuni kubwa na dogo katika kulipa kodi.

  Anosigwe

  August 28, 2011 at 10:34 AM

 25. Wapi VODACOM TANZANIA LIMITED wenye subscriber wengi kuliko Airtel,either TRA wazembe au VODA wenyewe wanatoa tarifa potofu za mauzo kwania ya kutuibia watanzania. Mimi sisemi kuhusu madini kwani hawa ni wezi tuliongia mkataba wa kuiba tukiwa tunajua wachache kwa manufaa yetu binafsi

  Patrick Mwakifuna

  August 28, 2011 at 2:44 PM

  • Vodacom is party of ccm therefoere they got tax exemption due to high contribution to ccm burget

   ndebile

   August 29, 2011 at 3:14 PM

 26. Muheshimiwa zitto, mimi natamani kuishitaki serikal ya Tanzania kwa wafadhiri ili waisusie budget yake tegemezi, pia niishitaki serikali kwa kushindwa kutekereza wajibu wake kwa kuwapatia huduma za msingi kama umeme(14%), maji, afya na elimu kwa kisingizio cha kukosa pesa huku TRA wakishindwa kukusanya kodi stahili toka kwa makampuni tajiri kama vodacom, bakresa,ggm, makampuni ya kuchimba na kusambaza gas na mengine mengi lazima wote tukubari kuna uzembe

  Isack

  September 1, 2011 at 7:10 PM

 27. nafurahishwa na jinsi mr Kabwe unavyofanya kazi zako, too bad hatujafahamu kutumia rasilimali watu. Mawazo yangu juu ya hii mada, nafikiri kuna weakness technical, nikiwa na maana TRA bado hawajawa na system nzuri ya kukusanya kodi, wataalamu wenye maadili ya kazi, siasa kuingiliana na utendaji wa taasisi ama mashirika ya kiserikali, mgawanyo mbovu wa kazi, kuwa na viongozi wenye maslahi ya kibiashara, na hili ni kubwa mno. Viongozi wetu wengi ndiyo wafanyabiashara wakubwa, wanahisa kwenye makampuni mengi, achilia mbali kwa yale makampuni yaliyo nje ya soko la hisa, wameekeza pesa nyingi. Hii inatupeleka hadi kwenye mikataba mibovu, si kweli kwamba hawajui wanachofanya, kwa mtazamo wa kawaida utafahamu kwamba hapa kuna share waliyonayo, wafanyabiashara si watu wenye utu, ni faida tu, hawawezi kuruhusu kampuni zao na za maswahiba wao zilimwe kodi ya haki kwa mujibu wa sheria.
  Nafahamu viongozi wetu kama Kabwe hamjachoka na hamtachoka na vikwazo mnavyovipata, kwaniaba ya wapenda maendeleo wa nchi hii napenda kuwafahamisha daima tupo pamoja nanyi. SAFARI NDEFU HUANZA NA ATUA YA KWANZA. chairman mao

  musa

  September 2, 2011 at 11:43 AM

 28. Hali hii haiwezi badilika iwapo hatutafikia mahali pa kusema bila hofu na kutenda bila aibu. Kwa sasa nafikiri hata hawa waliolipa bado kwangu hainishawishi, kwa uzembe wa TRA na wahusika tuliowapa jukumu, hapo ni ushindanishwaji wa watu wanaoamua wenyewe nini cha kutuonesha na nini cha kugawana. Wizi uliopo ni mkubwa, umaskini uliopo ni wa kukatisha tamaa. Tafadhali Mjadala wa Kitaifa sasa

  gotwaz

  September 2, 2011 at 3:20 PM

 29. Kod zenyewe wanazfisad,kuna haja ya kulipa??

  Pj

  September 3, 2011 at 8:02 AM

 30. Kuna tatizo mahali katika swala zima la ukusanyaji kodi vipi kuhusu kampuni za utalii maana nazo zinaongoza kuchangia pato la taifa sizioni kwenye listi,kama Rushwa itaendelea hii itabaki maskini!

  Adolf Ben-Gurion

  September 5, 2011 at 5:29 AM

 31. Ni vizuri,Lakini sijaona kundi la wafanyakazi maana PAYEE tunayolipa ni kubwa sana

  Bavon

  September 16, 2011 at 12:25 PM

 32. Watu kama Rostam wanaotajwa leo kuwa ni matajiri na kampuni yake ya Vodacom wako wapi katika kulipa kodi? Yusuf Manji na kampuni yake ya Quality Group yuko wapi katika orodha hii? Ama kwanini MetL hawamo katika orodha hii. Watanzania tutafakari sana!!

  Peter Jacob Awamu

  December 15, 2012 at 3:43 PM

 33. Tunaibiwa mchana kweupe

  Musa Twaha Kitonge

  February 17, 2013 at 12:15 PM

  • Kama makampuni yoter na wafanyibiashara wote wangelipa kodi vizuri na kwa mujibu wa sheria, Tanzania ingekuwa na mafanikio makubwa kiuchumi, lakini leo uchumi unabaki mikononi mwa watu na makampuni binafsi

   Vedasto Msungu

   May 29, 2013 at 11:04 AM

 34. Safi sana chanzo cha mapato tz

  Kadama pawa

  April 21, 2016 at 4:40 AM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: