HOTUBA YA WAZIRI KIVULI WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012
Dondoo/Highlights
Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma
Mashirika ya Umma mia tatu sitini (360) yalibainishwa (specified) kwa ajili ya ubinafsishaji mpaka Disemba 2009
Kati ya Mashirika hayo, Mia Tatu Thelathini na Moja (331) yamebinafsishwa na ishirini na tisa (29) yalikuwa katika hatua
mbalimbali za kubinafsishwa
Mapato la serikali kutokana na ubinafsishaji huo yalikuwa Shilingi billion 482. Hii maana yake ni wastani wa shilingi 1.5 bilioni kwa kila Shirika lililouzwa
Huu ni wakati mwafaka wa kufanya tathmini ya kina juu ya sera utekelezaji wa Sera ya Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma (Public Inquiry on Privatisation)
Ubinafsishaji pamoja na uwekezaji kwa ujumla haujaweza kutanzua tatizo la ajira ambalo linawakumba vijana wengi
Mashirika mengi ya umma yaliyobinafsishwa wawekezaji wameshindwa kutekeleza mambo/masharti waliyokubaliana na serikali hii ikiwa ni pamoja na wao kufanya mambo mengine kinyume na makubaliano kwa mfano Kiwanda cha Urafiki Dar es Salaam ambapo mwekezaji kutoka China amekuwa akiuza baadhi ya mashine kama vyuma chakavu
Usimamizi wa Mashirika ya Umma
Serikali imetenga shilingi bilioni 35.7 zikiwa fedha za kulipia madeni na mahitaji ya dharura kwa Mashirika ya Umma
Serikali imetenga shilingi bilioni 26.4 kwa ajili ya kulipa fidia kwa mikataba mbalimbali ambayo serikali imeingia
Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR-Treasury Registrar) imekuwa dhaifu mno katika kusimamia mali za serikali Katika Mashirika. *Mifano miwili ya namna hisa za Serikali zilivyouzwa itasaidia kuonyesha hali hii. Kampuni ya Oryx ilikuwa inamilikiwa na Serikali kwa asilimia hamsini mpaka mwaka 2004. Mwaka 2004, kupitia ofisi ya TR serikali iliuza hisa zake ambazo ni asilimia 50% kwa bei ya kutupa kwa thamani ya dola 2.5 milioni. Hivi sasa Oryx ni moja ya Kampuni inayofanya vizuri sana katika sekta ya Mafuta lakini hatuna umiliki tena na pesa kiduchu tulizopata zimekwishatumika!
*pia serikali ilikuwa na hisa katika kampuni ya simu za mkononi ya Mobitel ambayo kwa sasa inajulikana kama “tigo”. Katika hatua ya kushangaza na haina maelezo kabisa Serikali imeuza hisa zake asilimia kumi na sita (16%) kwa thamani ya dola 1.3 milioni mwaka 2006 na kwa sasa kampuni hiyo ni ya kigeni kwa asilimia mia moja jambo ambalo ni kunyume na sheria. Kampuni za Simu zatakiwa kumilikiwa na Watanzania kwa sio chini ya Asilimia 35. Asilimia 16 ya hisa Tigo leo thamani yake ni zaidi yakumi ya bei tuliyouza mwaka 2006.
Ofisi ya Msajili wa hazina (TR) ifumuliwe na ianzishwe ofisi ya Mashirika ya Umma ambayo itakuwa ni kama Wakala wa
Serikali chini ya Wizara ya Fedha ikiwa ni chombo huru chenye kusimamia Mashirika yote ya Umma (Office of Public Enterprises– OPE))
Mashirika yaliyo katika Sekta nyeti kwa umma yasibinafsishwe tena na badala yake yaendelee kumilikiwa na Serikali kwa
kuweka Menejimenti mahiri na kuwa na lengo la kuorodhesha hisa zao katika Soko la Hisa la Dar es Salaam ili kumilikisha
wananchi na kuweka uwazi katika uendeshaji.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania/National Bureau of Statistics-NBS
Mapendekezo ya kuboresha utendaji wa Ofisi ya Takwimu
Taarifa mbali mbali za takwimu zitolewe kwa uwazi ikiwahusisha wanahabari na wataalamu wa kada mbalimbali kama vile wachumi na kuwepo mjadala wa wazi kuhusiana na taarifa hiyo
Kuwa na uhisiano wa moja kwa moja wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa na ngazi za mikoa, halmashauri za wilaya, kata na vijiji
kurahisha upatikanaji wa takwimu ili zisaidie katika kupanga mipango ya maendeleo.
Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA
Kambi ya upinzani tunaitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania kuanza mara moja kufanya utafiti wa namna bora ya kutoza kodi ya faida kwenye dhahabu (windfall tax) ili kuongeza mapato ya serikali kwa sababu wawekezaji wanapata faida mara dufu kwa sasa kwa sababu ya ongezeko hilo la bei.
Deni La Taifa
Deni la taifa liliongezeka kwa asilimia 38% kutoka trilioni 7.6 mwaka 2008 mpaka Tshs 10.5 trilioni mwaka 2009/2010,
hadi kufikia mwisho wa mwezi Aprili 2011 kwa mujibu wa tamko la hali ya kifedha la Benki Kuu ya Tanzania la Juni 2011, deni la taifa lilikuwa dola za kimarekani milioni 11,455.4 sawa na shilingi trilioni 17.1 ambapo asilimia 80 ya deni hilo ni deni la nje
Wakati wenzetu wanakopa ili kuongeza uzalishaji (capital investments), sisi tunakopa kwa matumizi ya kawaida
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
Kuna kuna mifuko mitano ya hifadhi ya jamii nchini yenye jumla ya wanachama 1,073,441
Kati ya hao Shirika la NSSF lina wanachama 506,218 (47%), Shirika la PSPF lina wanachama 289,046 (27%), Shirika la PPF lina wanachama 160,068 (15%), Shirika la LAPF lina wanachama 73,833 (7%) na Shirika la GEPF ambalo lina wanachama 35,279 (4%)
Idadi hii ya wanachama katika Mifuko yote ni sawa na asilimia 2.5 ya idadi ya watu waliopo nchini na ni asilimia 4.7 ya nguvu kazi yote iliyo katika sekta rasmi ya ajira
Mifuko hii imewekeza katika vitega uchumi vyenye thamani ya shilingi trilioni 2.8, ambayo ni takribani asilimia 8.7 ya Pato la Taifa kwa bei za sasa. NSSF inaongoza kwa kuwa na uwekezaji wenye thamani ya
shilingi trilioni 1.03 (38%), PSPF inafuatiwa kwa kufanya uwekezaji wenye thamani ya shilingi bilioni 751 (27%), PPF uwekezaji wenye thamani ya shilingi bilioni 670 (24%), LAPF shilingi bilioni 206 (7%) na GEPF shilingi bilioni 82 (3%)
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni bado inasisitiza ushauri wake kuwa Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii ihamishiwe Wizara ya Kazi na Ajira kama Wizara inayohusika na ‘social security’. Hata Mdhibiti wa Mifuko (SSRA) yupo chini ya Wizara ya Kazi.
Hakuna sababu ya kuwa na utitiri wa mifuko mingi kama ilivyo sasa. Ipunguzwe na kubakia na mifuko miwili tu, mmoja wa wafanyakazi walio aktika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi na mwingine kwa wafanyakazi wa sekta ya umma.
NSSF na PPF iunganishwe kuwa mfuko mmoja kwa ajili ya sekta binafsi na isiyo rasmi na PSPF, LAPF na GEPF iunganishwe na kushughulika na wafanyakazi wa Sekta ya Umma
Huduma Kwa Wastaafu kwa Ujumla
Madeni ya PSPF ya michango ya kabla ya Julai 1999
watumishi wa umma wanaolipwa na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wanapostaafu hulipwa mafao yao tangu kipindi walipoanza kazi, japo wao wameanza kuchangia kuanzia Julai 1999. Kipindi cha Julai 1999 kurudi nyuma ni deni ambalo serikali inapaswa kuulipa Mfuko huu wa PSPF. Kwa bahati mbaya deni hili lilikuwa halilipwi kwa kipindi chote tangu Mfuko uanzishwe hiyo Julai 1999, na limeendelea kukua na kuwa deni kubwa sana sasa; takriban Shs 3,380 Billioni.
Nyongeza ya kiwango cha Pensheni ya kila mwezi kwa wastaafu
Masuala ya Jumla
Miundo Kandamizi kwa Watumishi wa kada ya Uhasibu Serikalini
Uwajibikaji ndio suluhisho kubwa kwa matatizo ya rushwa, hongo, ubadhirifu na ufisadi
Kambi ya Upinzani tutaendelea kuwa jicho la watanzania dhidi ya watawala, ninawataka Mawaziri Vivuli wote wafuatilie kwa karibu sana utendaji wa Mawziri katika maeneo yao ili kuhakikisha kuwa bajeti hii inatekelezwa kwa faida ya mwananchi wa kawaida.
kp t up bro we hv trust on u!
matilda
August 25, 2011 at 5:33 PM
Great Article I totally agree with it if we reduce hiyo mifuko to two of them then we will have large capital outlay and we can invest in development programs effectively
Oscar
August 25, 2011 at 5:36 PM
yes Zitto moja ya faida muhimu ya uwekezaji ni kutoa ajira lakini ni kweli tanzania wawekezaji hawajatatua hilo tatizo na vijana wengi waliopata nafasi wananyonywa na hao wanaojiita wawekezaji,wakati vijana wengi elimu nzuri na uwezo wa kudeliver wanao,maslahi yao ni ya chini sana kulinganisha na hao wenzao wanaowaleta ambao hata elimu yao ni ya kubabaisha. inauma sana.wenzetu india wana policies kali sana za uwekezaji baada ya kunyonywa kwa muda. kuna hitaji kubwa la kuweka na kufuatilia sera zenye maslahi kwetu,sisi sio dampo wala shamba lisilo na mwenyewe,ni taifa lenye watu timamu na tunahitaji viongozi wetu watambue hivyo na wajitambue wajibu wao.kama walikua wamelala wakifikiri tumekufa,sasa waamke wachakarike.
Heid
August 25, 2011 at 6:23 PM
kimcngi CHADEMA ndio tegemeo le2 manake kwayanayotokea ss hv ndan ya ccm hayawezi kulekebisha pac nakuingia chama kingine madalakani nahilo litawezekana km mkiamua kuwekeza siasa zenu vijijini ambako ndio ngome kuu ya ccm kwasababu huko wa2 hawana uelewa.
DADY MICHAEL JOHN
August 26, 2011 at 1:46 AM
TZ Kazi ipo.
Johndavid Mwakitalu
August 26, 2011 at 4:00 AM
kwa kweli unanikosha.endelea hvo hvo kaka kwa kweli naamini siku moja na sisi tutafika mahala tuwe nchi iliyoendelea kama nchi zingine zilizoendelea
Gabriel
August 26, 2011 at 8:38 AM
Hakika CHADEMA ndio chama pekee kilichobakia kutetea wanyonge, ccm wao na matajiri,mafisa,wala rushwa ndio watu wao. Chadema nawashauri muanzishe matawi mengi zaidi iwezekanavyo ili kufikia 2015 muwe na base imara. Tuko pamoja daima.
william Jotham
August 26, 2011 at 10:47 AM
kiukweli hotuba ni nzuri sana,jambo la msingi kwa serikali yetu wapokee na kutekeleza mapendekezo haya yanatia moyo sana hongera sana waziri kivuli keep it up to change our nation
yahaya mohamedi
August 26, 2011 at 12:35 PM
safi mheshimiwa waziri tena ww sio waziri kivuli kwa hoja hizo ww ni wazir kamili kabisa since kuna utofauti mkubwa wa kihoja na aliyempendeza president
hamza
August 26, 2011 at 2:02 PM
Ninakupongeza bro!big up
Clement manyatta
August 26, 2011 at 3:00 PM
it was great Article but I was espect you to promp more sources where the govt could generate more revenue especially in green economy
R.Komu
August 27, 2011 at 6:57 PM
Mh Zitto kazi yako tunaiona yaan wewe ni waziri kivuli lakni unamfunika huyu part 2 wako kwa kiwango kikubwa sana., vijana tunajiandaa kukupeleka Ikulu mzee maana tumeona unatufaa….CHADEMA FOREVER……………….
emmanuel mushi
August 29, 2011 at 11:28 AM