Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Sekeseke La Mafuta Mchango wangu Bungeni

with 11 comments

MHE. KABWE Z. ZITTO: 

Mheshimiwa Spika, katika hali ya kawaida tumezoea kuona wafanyakazi wakigoma kudai maslahi yao pale ambapo wanapoona maslahi yao hayatekelezwi na waajiri.  Wanaita industrial action.  Hatujawahi kuona kwa muda mrefu wafanya biashara wakifanya industrial action na tulipoamua ku-liberalize kufungua uchumi wetu kuwa uchumi wa soko tulitoa haki kwa wafanya biashara kufanya kazi kwa mujibu wa soko.  Lakini kamwe hatukuondoa uwajibikaji wa Serikali. 

Bado responsibility ya Serikali kulinda raia wake ilibakia  ni jukumu la Serikali.  Wafanya biashara kwa kutumia cartel yao wameamua kukiuka maagizo ya chombo cha Serikali.  Hatupaswi kuwa na maneno matamu ya aina yoyote dhidi yao.  Ni lazima ionekane kuna Serikali.  Ni lazima ionekane kuna dola.  Ni lazima ionekane kuna uwajibikaji ambao vyombo vya Serikali inafanya kulinda raia.  Sheria ya EWURA imetoa nafasi, imetoa hadhi ya EWURA kulinda walaji na imesisitiza kulinda walaji wa hali ya chini.  Kifungu cha 6(B) cha Sheria ya UWURA.

Leo wananchi wetu Dar es Salaam na miji mingine ya nchi wanahangaika.  Hawawezi kwenda makazini kwenda kufanya kazi za kuzalisha mali.  Wakienda kwenye madala dala hivi sasa nasikia daladala zimepandisha bei.   Kule Kigoma leo ni siku ya nne hakuna umeme.  Kwa sababu hakuna mafuta. Wafanya biashara wa mafuta wanai-hold nchi, hatuwezi kukubali.  Kama nilivyosema in a democracy wafanya biashara wana haki zao kama wafanya biashara.  Lakini Serikali ina majukumu yake na wajibu wake kama Serikali.

Naiomba na ninapenda nilishawishi Bunge, kwamba EWURA leo wa-order wafanya biashara wote wa mafuta wa-release mafuta.  Atakayepinga anyang’anywe leseni mara moja.  Natoa ujumbe kwa wananchi wetu inawezekana maamuzi haya yakawa yakawaletea shida.  Haitakuwa mara ya kwanza wananchi wetu wanapata shida.  Tulikwenda vitani kupiga na Nduli Iddi Amini hatukuwa na uwezo, hatukuwa na vifaa kama alivyokuwa navyo yeye.  Hatukuwa na wakubwa wanaotuunga mkono kama alivyokuwa anaungwa mkono yeye.  Wafanya biashara binafsi walitoa magari yao. Wanajeshi na mgambo walikuwa mobilized tukaenda vitani tukampiga Nduli tukamtoa na tukamtoa Uganda.  

Mtapata shida wananchi lakini ni lazima tutoe fursa ya kufanya inforcement ya Sheria zetu.  Nawaomba Waheshimiwa Wabunge, wafanyabiashara ya mafuta wana maneno matamu sana, watakuambia kuhusu profit margins zao lakini muwaulize wakati tumeamua bei ya mafuta ya taa ipande the next day walipandisha bei.  Hawakutueleza masuala ya profit margins  zao.  Hawawezi kutueleza sasa masuala ya profit margins. 

Sheria imeshatoka EWURA wana kazi ya ku-enforce na sijasikia kama wafanya biashara wamefuta  wamekata rufaa, sijasikia kama Tume ya Ushindani imekaa kuangalia rufaa ambayo wafanya biashara ambao wamefutwa. Wanataka kutuonyesha ubabe wao.  Wanataka kutumia jeuri yao ya fedha.  Watanzania siku zote ni maskini jeuri.  Leo mafuta yatoke.  EWURA wa-oder mafuta yatoke.   Ikifika saa 12 jioni wafanya biashara wamegoma wanyang’anywe leseni mara moja.   Jeshi la Wanajeshi liingie wafungue vituo, wafungue ma-godown mafuta yatoke watu wetu wapate mafuta.  

Wachumi, Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha, wakae waangalie hilo suala la profit margin la wafanya biashara wakati raia wanapata mafuta.  Hatuwezi kukaa hapa tunajadiliana mambo ya nchi kuna watu wachache wamekaa wanaamua kutokana na maslahi yao ya kibiashara.  Hatuwezi kukubali hata siku moja. 

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa naomba nichangie na ninaomba Bunge lako tukufu likubaliane nami EWURA wafanye kazi hiyo na tuwape nguvu EWURA, vijana wetu wanapokuwa kazini tusiwakatishe tamaa. Tusiwaone EWURA ni wakosaji wakati wanatekeleza maagizo ya Bunge.  Ni sawa sawa na askari wako yuko jeshini kuna matatizo unaanza kumlaumu.  Tuwalaumu baadaye, tuwape nguvu EWURA wafanye enforcement mafuta yapatikane, twende wananchi wetu wafanye kazi kama jinsi inavyotakiwa.  Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. 

 

Advertisements

Written by zittokabwe

August 10, 2011 at 5:43 PM

11 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. bro ya really ma role model,kip it up!

  alfred jacob.

  August 10, 2011 at 5:59 PM

 2. Zitto wauza mafuta wengine mpo nao humohumo BUNGEN

  Pj

  August 10, 2011 at 6:20 PM

 3. kama ewura ilikaa na wafanyabiashara ya mafuta wakakubaliana bei mpya, then kesho wakageuka. hapo pana kitu kinafichika, kwa nguvu gani, kitu gani kinachowatia kiburi kufanya mgomo kushindana na gov? inakuwa vp wakuu wa nchi na wahusika wengine wapo silent hadi bunge liingilie kati? sijui upande wa sheria ukoje hapo haswa ktk uwajibikaji, naomba ufafanuzi kdg ktk sheria inavyoelekeza

  Alan

  August 10, 2011 at 6:26 PM

 4. Kwa kweli Mh. Zitto hayo ndio matarajio ya wananchi wengi,mbunge wanayemchagua awatetee kwa nguvu zake zote c makofi 2

  MOSES MWANJA

  August 10, 2011 at 7:09 PM

 5. Kukiri kwamba mlipandisha mafuta ya taa,imeniuma sana.Tukirudi kwenye mjadala,kwanza haya n matoke ya haki za mtu mojamoja bila kuzingatia haki za wengi ndo mana watu wachache(wafnybiashar) wanagoma kuathiri wananchi.Pili,serikali lazima iwe na mkono ktk soko.tatizo hapa nyumbani ni kucheka na wafanyabshra wa mafuta,lazima waonjeshwe STATE POWER.Lazima wajue hii ni state.

  Idd Thovu

  August 10, 2011 at 7:09 PM

 6. Hongera sana zitto kwa mchango wako mzuri sana juu ya mambo mbali mbali ya nchi, toka nimeanza kukuona wewe na wabunge wa chadema mkitoa michango mbali mbali inayogusa maslahi ya nchi napata faraje sana kuwa sikumoja tutafika na kama rais Obama alivyosema usiku ule wa tarehe 4 november 2008 wakati katangazwa mshindi wa urais wa marekan kuwa “the road will be long, the climb will be steep, we may not get there in one day or iven in one tearm, bt americans there is no day that am hopefull like today! We shall get there. Hata mimi naamin through you folks Tanzania shall get there na niwatie moyo kwa kusema kuwa msikata tamaa

  salvatory okumu

  August 10, 2011 at 7:34 PM

 7. kaka kwa hilo ninakupa heko bunge linaonekana kuipunguzia nguvu yake kwa vijana 2nao ona mbali we shall make a changes but lets be only the part of changes

  charles nilla

  August 11, 2011 at 7:16 AM

 8. Kaka Zitto tunashukuru sana kwa kuons kilio chetu kwan kwa sasa yunauziwa mafuta kwa sh 3500.

  Godsonn

  August 11, 2011 at 9:15 AM

 9. Pole na asante kwa kutetea haki za wengi

  Michael mwachumu

  August 11, 2011 at 9:50 AM

 10. SAFI SANA WANATAKIWA ZIONGOZI KAMA WEWE NAONA SASA MAMBO MAZURI BUNGENI. SAFI KAKA ONGEZA BIDII.

  faraja mohamed

  August 11, 2011 at 4:03 PM

 11. Safi sana mheshimiwa Zitto. Wa Tz wanyonge tuko nyuma yako asante kwa kututetea.

  Ombeni Charles

  August 20, 2011 at 12:03 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: