Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Mchango wangu: Bajeti ya Uchukuzi

with one comment

MHE. KABWE Z. ZITTO:

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru nimekubaliana na Mheshimiwa Raya Ibrahim Hamisi  kwa sababu hajisikii vizuri na ana udhuru kwamba nafasi yangu ya kesho atazungumza yeye na mimi nichukue nafasi ya kuzungumza leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kukushukuru kwa kukubaliana na mabadiliko haya na kunipa fursa ya kuchangia hotuba ya Wizara hii yaani bajeti ya Wizara  ya Uchukuzi. Ni Wizara nyeti sana kama jinsi ambavyo Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu amezungumza na Msemaji Mkuu wa Upinzani na Wabunge wengine wote ambao wamezungumza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi kabla sijaja hapa Bungeni nilipata fursa ya kukutana na Viongozi wakuu wawili wastaafu yaani Mheshimiwa Dr. Salim Ahmed Salim na Mheshimiwa Mzee Joseph Sinde Warioba.  Waliniomba nikutane nao kwa sababu ya jinsi ambavyo wanaona tunavyokwenda na mwenendo wa Bunge.  Lakini hili ni kwa pande zote kwa maana ya Wabunge wa Kambi ya Chama Tawala na Kambi ya Upinzani pamoja na meza kuu ambao wanaongoza vikao vya Bunge. Ujumbe walionipa ni kwamba tuna kazi ya kuendesha nchi, kwa hiyo, tujikite katika kuhakikisha kwamba tunawasemea wananchi, tuna nchi ya kuongoza.

Kwa hiyo, ni vizuri sana Waheshimiwa Wabunge wote kwa pamoja na ndiyo maana nimeona nitumie fursa hii kuweza kutoa ujumbe huu wa wazee hawa kwamba  tuwe makini sana kwa kufahamu kwamba tuna nchi ya kuongoza. Inawezekana kabisa tukawa tunafurahi kutumia jukwaa hili la Bunge kwa ajili ya kujaribu ku-score some political points lakini a day inayopita kurushiana vijembe ni a day inayopita kuendesha nchi yetu. Kwa hiyo, ni vizuri sana wote kwa pamoja haiwezekani kuacha kufanya siasa ndani ya Bunge ni lazima tufanye, lakini over riding goal iwe ni kuendesha nchi yetu kwa pamoja. Huu ndiyo ujumbe ambao wazee wamenipa inawezekana ikawa siupendi mimi mwenyewe lakini wameniomba niuseme na nimeufikisha na ninadhani huko Mzee Joseph S. Warioba  na Dr. Salim Ahmed Salim watakuwa wanafurahi kwamba kina wao ameweza kuufikisha ujumbe waliompa kwa niaba ya Wabunge na wamesisitiza Wabunge vijana. Kwa hiyo, nadhani vijana Wabunge wote wamesikia na nimewaomba wafanye utaratibu  wa kukutana na Wabunge wote vijana waweze kuwapa huo uzoefu na kadhalika ili wapate fursa pia ya kuweza kujua nchi hii inakwenda namna gani.  Nadhani wamekubali na wataweza kukutana na Wabunge wa Kambi zote mbili siyo Wabunge wa CHADEMA peke yake au CCM peke yake. 

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna bajeti ya Wizara ya Uchukuzi ambayo ni pungufu sana na ninapenda nichukue fursa  hii kuwapongeza Wabunge wenzangu wawili wa Kigoma, yaani Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu Mheshimiwa Joseph Serukamba na Mheshimiwa Mhonga Said Ruhwanya Mbunge wa Viti Maalim kutoka Kigoma. Kwa niaba ya Kambi na kwa niaba ya Kamati waliweza kutoa maoni ambayo yamedhihirisha kabisa kwamba iwapo Bunge hili litaidhinisha makadirio haya ya Wizara ya Uchukuzi hatutakuwa tumefanya jambo lolote la maana, kwa sababu hakuna jambo lolote jipya ambalo limo ndani ya bajeti ya Wizara hii. Lakini inawezekana tukamshughulikia sana Waziri lakini hapa nina barua ya Waziri ambayo tarehe 27 Aprili, 2011 amemuandikia  Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa ajili ya kuonyesha concern zake  za udogo wa bajeti ya Wizara yake. Pia akawa ameomba kwamba  kutokana na udogo wa ceiling naiomba Ofisi yako iingilie kati  suala hili kwa kutafuta njia ya kutenga fedha kwa ajili ya sekta ya Reli ambayo miradi yake mingi haitakuwepo kwenye bajeti zilizopita kutokana na TRL kuwa chini ya Management ya RITES. 

Lakini maombi haya ambayo Waziri aliyapeleka kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu hayajafanyiwa kazi yoyote ile na leo tumeletewa bajeti ambayo haiwezi kabisa kutatua tatizo la Reli, haiwezi kabisa kutatu tatizo la usafiri wa anga na hasa ATCL na wala haiwezi kusaidia katika kuendeleza nchi yetu. Ninafikiri na ninakubaliana kabisa na Mheshimiwa Tizeba aliyeanza, baadaye Mheshimiwa Mbowe na Wabunge wengine wote kwamba ni vema tufanye retreat, tuombe Serikali ikakae iangalie upya namna gani ya kuweza kusaidia Wizara hii iweze kupata bajeti ya kutosha. 

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa wa 43 wa hotuba ya Waziri amezungumzia suala la Reli na kama nilivyosema na kama wazungumzaji wote walivyosema, kwamba kimsingi hakuna jipya ambalo linafanywa. Kwa mfano, Waziri anasema kwamba Serikali imezungumza na Benki ya Dunia na ninafahamu hili limekuja baada ya mara ya kwanza Kamati ya Miundombinu kuikataa bajeti baadaye wakasema kwamba Benki ya Dunia wanakuja watatupatia pesa. Lakini wanasema; taratibu za kumpata mtaalamu mwelekezi wa kufanya utafiti kuhusu mahitaji ya Reli ya Kati’.

Reli ya Kati

Mheshimiwa Mwenyekiti,  Nchi hii bado tunafanya utafiti kuhusu mahitaji ya Reli ya Kati? Kweli tunahitaji Benki ya Dunia ije kutupa fedha tumtafute mtaalamu mwelekezi tumlipe atuambie mahitaji ya Reli ya Kati? Hii ni aibu kabisa na ni jambo ambalo wala haliingii akilini. Haiwezekani kwa sababu mahitaji ya Reli ya Kati yanafahamika toka alipojenga Mjerumani  mwaka 1905, leo hatuwezi kukaa kutafuta fedha eti kumtafuta mtaalamu mwelekezi wa Benki ya Dunia lakini tunajua miradi ya Benki ya Dunia. Hata kama kungekuwa na nia njema kabisa na kwamba Benki ya Dunia inakuja itatuwekezea kwenye Reli, Benki ya Dunia tunajua na ninyi Wabunge ni mashahidi wa miradi ya haraka  ya maji kwenye Wilaya zetu jinsi ambayo inachukua miaka na miaka kupata no objection kutoka Benki ya Dunia. Hakuna mradi wowote mkubwa wa infrastructure toka Benki ya Dunia ambao umefanikiwa kwa kiasi kikubwa na inachukua muda mrefu sana.

Sisi Kigoma ile Airport ya Kigoma tumeanza kuitafutia fedha kutoka Benki ya Dunia toka mwaka 2006 mpaka sasa hazijaingia na kila mwaka kwenye bajeti tunaziweka, leo tunaambiwa kwamba Reli ya Kati nayo Benki ya Dunia. Hii  ilikuwa ni statement ya kuwapashapasha kidogo na kuwalainisha watu wa Kamati ya Miundombinu ili waweze at Committee level kuweza kuipitisha bajeti na leo Mwenyekiti amekuja hotuba yake mwanzo mpaka mwisho ni matatizo tu lakini mwisho anasema kwamba tumekubali fedha hii ipitishwe. Kwa  ajili ya nini? kwa ajili ya kufanyia nini?

Waheshimiwa Wabunge ninawaomba na ninaomba nitoe rai kwamba katika jambo hili tuachane kabisa na political ideologies, kabisa!  tusimamie nchi yetu haiwezekani tukaruhusu bajeti ndogo kiasi hiki. Ni lazima tuwape fursa Serikali waende wakakae wafikirie upya waangalie vyanzo vingine, wajue wapi kwa kukopa, wapi pa kukata, wapi kwa kuongeza lakini tupate fedha kwa ajili ya bajeti ya Wizara hii.

ATCL

Mheshimiwa Mwenyekiti, Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani amezungumzia vizuri sana suala la ATCL na kila Mtanzania anaelewa tatizo tulilonalo na ATCL.  Leo hii   Tabora hakuna ndege, ukitaka kwenda Kigoma inabidi upite Mwanza ndiyo uende Kigoma kisha upande  ndege ndogo za ORIC Air na return ticket kwenda Kigoma sasa hivi ni shilingi milioni moja, one million. Mkisema mpitishe bajeti hii kama jinsi ilivyo maana yake ni kwamba mnatuonea sisi watu wa Kigoma na Tabora hamtuonei huruma Watanzania wenzenu. Lakini mkikataa kupitisha bajeti hii ili Serikali iende ikakae ifikirie upe ipate fedha za ATCL mnawaunga mkono na mnawafuta machozi Watanzania wenzenu wa Kigoma na Tabora. Nawaomba mtufute machozi  kwa kuikataa bajeti hii ili Serikali iende ikakae iweze kuangalia ni namna gani tutakavyoweza kupata fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ATCL wanahitaji fedha, Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu ametoa mfano wa Kenya Airways hapa namna ambavyo share capital ya Kenya Airways ilivyo yaani Instructional Investors na kadhalika. Katika mapaendekezo yetu ya bajeti kivuli tulielekeza kwamba kuna watu ambao wanafaidika moja kwa moja na utalii yaani TANAPA na Ngorongoro wapeni up to 60% ya shares waingize capital ili tupate fedha za kuanzia lakini baada ya miaka mitatu wakifanya vizuri tutangaze IPO. Lakini Ethiopia  Wazungu wamemnyima Merets Zanawi pesa za kutengeneza Hydro Power Station  anatengeneza Hydro Power Station kubwa sana lakini wazungu wamemkatalia kwa mambo ya mazingira na kadhalika. Lakini yeye ameamua kuitisha a National Bond an Infrastructure Bond ambayo kila Mu-ethiopia ananunua wamepata fedha mara mbili ya walizokuwa wanazitafuta kwa ajili ya kufungua Hydro Station, washirikisheni Watanzania wawe sehemu ya ownership ya hiki kitu, 60% ya fedha zinazotokana na utalii zinabakia kwenye nchi kama nchi hiyo ina National Carrier, ndiyo maana Kenya wanafaidika na utalii.  Sisi kwa maana hiyo ni kwamba tunabakia na a only a third ya fedha ambazo zinatokana na utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba na Waheshimiwa Wabunge na ninawa-convince suala hili tuweze kwenda nalo vizuri.

Mikopo ya Wachina

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu bandari. Kuna improvement ambazo zimetokea kwenye bandari. Kiwango cha meli kukaa  majini kimepungua sana na tunawashukuru sana kwa hilo na ninawapongeza sana watu wa Mamlaka ya Bandari. Tuna develop base 13 & 14 tumeamua kwenda China kuomba mkopo, sina tatizo hata kidogo  na mikopo kutoka China, hata kidogo. Lakini  naomba nitoe ushauri tu as an economist.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mikopo mingi ya China  gharama yake ni kubwa sana. Sasa hivi kwa sababu ya matatizo ya madeni ya Marekani Wachina wanakimbilia nchi za Afrika, lakini wanatupa mikopo kwa gharama kubwa sana. Kwa mfano,  gharama halisi za kutengeneza base 13&14 katika Bandari ya Dar es Salaam hazizidi dola milioni 340. Mkopo ambao Wachina wanataka kutupa ni wa dola milioni 525, lakini kuna the easiest way ya kwenda kutangaza tender through PPP International Tender watu wa-bid waje watengeneze, wa-own na baadaye wa-transfers kwa Serikali kwa Mamlaka ya Bandari, that is the easiest way wala nchi haiingii kwenye mikopo. Kwa hiyo, ninaomba muangalie hizo options, mikopo ya China, msiende tu kukopa ni ghali sana kwa sababu inaendana na conditionality kwamba tunakupa mkopo lakini Contractor atoke China maana yake ni kwamba hela yote inarudi China. So you have to be very careful katika maamuzi haya.

UDA

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho  suala la UDA. Waheshimiwa Wabunge wamelizungumza sana na ukiangalia unakuta watu wamezungumza  na taarifa zipo tofautitofauti. Lakini nataka niseme jambo moja kwamba  mwaka 1997 UDA ilikuwa listed specified kama Shirika linakwenda kubinafsishwa. Ilitolewa Government notice namba 555 mpaka leo tunavyozungumza Government Notice hiyo haijawahi kufutwa. UDA bado ni specified cooperation na kuna watu wanadhani kwamba hisa za UDA zilizokuwa specified ni zile 49% ya Serikali peke yake, no! Shirika zima la UDA lilikuwa specified. Maamuzi yoyote ya ku-privatise UDA yalipaswa kuwa approves na Consolidated Holdings, kama kuna mtu yeyote  ambaye amenunua hisa za UDA hakuna approval ya Consolidate Holdings ameingia choo cha kike. 

Mheshimiwa Mwenyekiti,  mmetugawia Mamlaka, ndani ya Bunge, kuna Kamati za Bunge. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma kwa mujibu wa Kanuni za Bunge ndiyo mmeipa majukumu ya kufuatilia utekelezaji wa sera ya ubinafsishaji na mimi ndiye Mwenyekiti wa Kamati hiyo.  Alianza kunipa fursa hiyo Mzee Samuel J.  Sitta na baadaye Mama Anne S. Makinda akaendeleza na ninadhani  nitamaliza miaka mitano hii. Kama Mwenyekiti wa Kamati ya Mashirika ya Umma na kwa niaba ya Wajumbe wangu wote as far as we are concern, UDA haijawa privatised kwa sababu taratibu za kisheria hazijafuatwa. Public Operations Act 1992 ya Consolidated Holdings hazijafuatwa na hapa ndiyo matatizo ambayo Mheshimiwa Mbunge mmoja amezungumza ya Ofisi ya TR. Tunawaambia kila siku na tunalalamika, jamani hisa za Serikali ambazo tuna chini ya 51% zinaendeshwa vibaya kwa sababu Ofisi ya TR haina nguvu ya kuweza kuzifuatilia, ndiyo mambo ambayo yametokea kwenye TRA.

Mheshimiwa Eng. Salvatory Naluyaga  Machemli amezungumzia kwamba ni mambo ya CHC, siyo mambo ya CHC hili ni suala la ofisi ya TR kwa muda mrefu imekaa bila kuteua Wajumbe wa Bodi ya UDA. Wajumbe wa Bodi ya UDA walikuwa waliokuwa wanafanya kazi ni wale walioteuliwa na Halmashauri ya Jiji peke yake. Wamekwenda wanauza  wanasema eti wanauza un allotted shares. Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali atanisaidia, un allotted shares ni sehemu ya ownership ya shareholders na siyo mali ya Board Members. So it is wrong kuuza un allotted shares maana yake ni nini?  Serikali inamiliki 51% Jiji, …….

 MHE. KABWE Z. ZITTO:

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

 

Advertisements

Written by zittokabwe

August 4, 2011 at 4:53 PM

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. Nimefurahishwa saaana na mchango wako,ila ujumbe wa MZEE SAS na Warioba imebigusa sana,,,,,,lakin wabunge hawatoifanyia kazi

    Pj

    August 17, 2011 at 7:57 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: