Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

SUALA LA POSHO ZA VIKAO: WAZIRI MKUU-ANAPASWA KUCHUKUA HATUA MBILI, AFUKUZWE AU AJIUZULU!

with 6 comments

Kwanza nasikitika kuwa Waziri Mkuu amerejesha suala la posho za vikao kwenye mjadala ilhali lilimalizwa baada ya Bungekupitisha Mpango wa maendeleo wa miaka 5.  Kitendo cha Waziri Mkuu kulilia posho kinaonyesha jinsi asivyo tayari kusimamia na kutetea sera za serikali anayoongozwa. Anapaswa kuchukua hatua mbili, ama afukuzwe kazi kwa kwenda kinyume na maamuzi ya kisera ya serikali yaliyopitishwa na baraza la mawaziri na Bunge, au ajiuzulu. Hatuwezi kuvumilia viongozi wanaokwenda kinyume na sera za serikali.

Waziri Mkuu: Mizengo Pinda

Written by zittokabwe

June 19, 2011 at 6:12 PM

6 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. BIG UP MH ZITTO, natoa ombi langu kuwa muangalie uwezekano wa kumwajibisha PM haraka iwezekanavyo ama kwa mujibu wa kanuni za kudumu za bunge toleo la 07 ama uwezo wenu kama kambi rasmi ya upinzani. WE are together! I’m JUMA KAMBAJECK.

  JUMA KAMBAJECK

  June 19, 2011 at 7:53 PM

 2. jambo hili likiwezekana itakuwa heri sana kwetu siye wananchi tunaofuatiliwa kwa karibu mdahalo huu, tupo pamoja katika hili!

  aidan mmari

  June 20, 2011 at 8:44 AM

 3. huyu ndo munayemwita mtoto wa mkulima anayeonekana kusahau kuwa watotowa wakulima wanahitaji hiyo fedha ili wapatiwe maendeleo!

  Budix

  June 20, 2011 at 9:16 AM

 4. Hata mimi kiuhalisia nilishangaa siku ile alivyoamua kujitosa na kupigilia msumari wa mwisho kama serikali kuonesha ulipaji wa posho kwa wabunge kuwa lazima uendelee,Kustaajabu kwangu ni kwasababu yeye ni waziri mkuu na kiongozi wa shughuli zote za seriakali bungeni na mwenye kauli ya mwisho bungeni kuhusu msimamo wa serikali kwa jambo fulani.

  Lakini pia mbali hapo yeye anajiita mtoto wa mkulima,sasa swali anapateje ujasiri wa kujjita jina hilo na wakati asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima na wamepigika sana vijijini,na wakati huo yeye anatetea posho za wabunge zisizo na tija kwa serikali yenye wananchi masikini? Wananchi waliompitsha bila kupingwa pale jimboni kwake walijisikiaje waliposikia majibu kama yale yakitoka kinywani mwake siku ile.

  Hakika,anapaswa kuachia Ngazi mara moja kwani anaonekana hana msimamo hata kidogo zaidi kupelekwa kama mnyama tena aliekatwa kichwa

  Ntegeye,Alex P.

  June 20, 2011 at 12:23 PM

 5. Mh mimi kabsa nakupongeza kwa kazi nzito unayoifanya ya kutetea wananchi wako,kama sheria inaruhusu waziri mkuu apate adhabu kulingana na kosa alilofanya basi haina budi kwa yeye kupata adhabu iyo,na mwendelee na moyo na nguvu hizohizo pingeni mpaka mwisho cc 2shawachoka kila muda ahadi zisizotekelezeka tangu uhuru wanaimba maisha bora kumbe hakuna lolote

  Andrew Mosha

  June 22, 2011 at 2:08 PM

 6. Gud!

  oxygen

  January 26, 2012 at 10:36 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: