Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Update: Posho za Vikao- Majibu ya Ofisi ya BUNGE na Uamuzi Wangu

with 16 comments

MAJIBU YA OFISI YA BUNGE

View this document on Scribd

 

UAMUZI WANGU-MAJIBU KWA OFISI YA BUNGE

View this document on Scribd

Written by zittokabwe

June 11, 2011 at 8:31 AM

16 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Ofisi ya Katibu wa Bunge inaonesha udhaifu katika maamuzi yake. Kimantiki mh Zitto hukukataa kupokea posho ILA ULIELEKEZA POSHO ZIPELEKWE KDI ili dhana kuwa POSHO HIZO ZIWASAIDIE WANANCHI WA KAWAIDA LITIMIE.

  Saidi Msonga

  June 11, 2011 at 9:03 AM

 2. safi sana. uamuzi wa kizalendo. mfano bora wa kuigwa

  william mmari

  June 11, 2011 at 9:04 AM

 3. Zito huo ni uamuzi uliosukumwa na nia ya dhati ya kuwatumikia Watanzania na si kuchumia tumbo kama walivyo wengi wa waheshimiwa walioko Bungeni wengine hata uwezo wa kujadili hoja hawana wamebebwa na wamebweteka wakila pesa za wavuja jasho bila aibu naomba kitu kimoja muhakikishe KATIBA MPYA kabla ya uchaguzi ujao tuwanyoe kisha waadhibiwe kwa udhalimu wa kwa kweli wananchi wamechoka kuishi kitumwa katika nchi yenye neema.

  ALUTACONTINUA………..

  Thabit Molly

  June 11, 2011 at 9:17 AM

 4. kaka wamekugomea? wameona utapata umaarufu

  sosy diwani

  June 11, 2011 at 9:35 AM

 5. Hakika juhudi zako Mh.Zitto ni za msingi sana,lakini nakwazwa na ofisi ya katibu wa Bunge kusema generally kuwa kwa mujibu wa sheria,sheria ipi na kifungu kipi? Ikumbukwe wazi bunge ni mhimiri ambao wananchi hatutegemei kuwa na majibu ya jumla kama hilo,Naamini kwa mkakati huu uliounzisha Mh.mbunge tutafika pale tunapotaka mkoa wetu ufike na Taifa kwa ujumla,Mungu aibariki kazi ya mikono yako Mh.mbunge,tupo nyuma yako tangu sasa mpaka kielewke.
  Long live Mh.Zitto Z.Kabwe

  Fredie Mayeye

  June 11, 2011 at 9:45 AM

 6. Mfano mzuri mh. KABWE, (CHADEMA) na wengine watutoe kwenye nadhalie tuingie kwenye vitendo.

  sandahillary

  June 11, 2011 at 11:08 AM

 7. Hapa sasa ndugu yangu zitto una mtihani kabisa. Au uziache au uzichuke wewe mwenyewe na kuzipeleka kule ulikokusudia.
  Kuiacha posho kutakusaidia kusimamia hoja yako kwa nini hukuhitaji kuchukua posho hii dhalimu.

  Jimmy

  June 11, 2011 at 11:59 AM

 8. kaka hongera sana nadhani kwa sasa wamepatikana hawana pa kukimbilia si ushabiki bali umekuwa muwazi na mkweli hongera sana kwa hilo mkubwa naamini tukipata wabunge 200 wa aina hiyo nchi yetu itajengwa tu

  revocatus balenga

  June 11, 2011 at 12:33 PM

 9. pia mh mkumbushe na Selukamba atujali walau kgm mjini kaka ,mana hali unaijua hizo posho aongezee katka mfuko huo walau tujikombowe sasa na pia kama taifa

  revocatus balenga

  June 11, 2011 at 12:38 PM

 10. Tunayo kazi kubwa hadi kufikia hatua ambapo kutakuwa na usawa nchini. Nimesoma barua kutoka ofisi ya Bunge, nimesoma pia maoni ya waziri wa fedha na uchumi (Mhe. Mkulo). Pengine majibu ya ofisi ya bunge yana uoga ndani yake kwa kuogopa kivuli cha wapenda sera ya kulipana posho (kwa maoni yangu). Nimesikitika zaidi baada ya kusoma waziri akiliita pendekezo hili kama “unafiki”. Nikajiuliza, kwa hoja yake ni dhaifu kwa vile, katika jamii, vitu vingi huanzishwa na jamii hiyo hiyo yawe mabaya ama mazuri. Lakini ndani ya jamii hiyo hiyo na kutoka kwa wale wale waliopitisha maazimio hayo hayo, endapo itatokea uchambuzi wa kubaini ubaya wa jambo fulani, basi kutoa mapendekezo ya kuondoa jambo linaloleta hasara kwa jamii si “unafiki” hata kidogo. Hivyo, mhe. Mkulo hapa ameonyesha kukosa uvumilivu wa kiuchambuzi ambao, hakika ungempa nafasi nzuri ya kutoa tamko linalofanana na nafasi yake (inayostahili kuwa na heshima yake).

  Kimsingi, kwa maoni yangu, hoja ya kuondoa posho za vikao inafaida kubwa kwa jamii yetu kuliko faida tunazozipata wachache wenye stahili za kupata posho hizo. Nitoe mfano, mimi ni mtumishi wa umma ambaye kimsingi nimekuwa (ikitokea) naagizwa kuhudhuria vikao mbalimbali nikiwa ofisi na pengine nje ya ofisi yangu. Kwa vikao nje ya ofisi anayenipeleka ni dereva, na hakika kama kuna posho, uzoefu nilionao ni kwamba, huwa hakuna posho za madereva hata kidogo. Hivyo, binafsi limekuwa likinitesa sana katika fikira zangu kuona mimi na wengine tunapata nafasi hiyo ya pato la ziada ya mishara wakati wengine (madereva na wengine wengi) wakiikosa. Kwa sababu ya kuwa na mtazamo huo wa huruma na usawa kwa wengine, kimsingi nimekuwa nagawana na dereva wangu ikitokea kupokea posho. Hata hivyo, hakika nakiri madhara makubwa yatokanayo na posho hizo hasa kuanzia katika suala zima kwamba, posho hizo huharibu ratiba ya utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya afisa ndani ya ofisi yake. Sisi ni wanadamu na kwa vyovyote vile, ubinadamu wetu (udhaifu) utatuvuta tu kufikiria kuandaa vikao ambavyo, hakika vina nia ya kujenga mazingira ya kulipana posho.

  Ushauri wangu kwa Serikali, na kwa sasa Bunge, basi waondoe mfumo wa posho za vikao na badala yake kuwe na majadiliano muafaka yatakayoongeza mishahara ya watumishi (kama tatizo na sababu ya kuwepo posho ni mishahara ya chini/midogo). Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tumeongeza muda wa watumishi kuwepo ofisini, lakini pia tutakuwa tumeondoa uwezekano wa kuongezeka kwa pengo kati ya watumishi wa umma linalosababishwa na posho kubagua watumishi. Na hakika kumekuwa na matukio mengi ndani ya ofisi ninayofanyia kazi kutokea mivutano na chuki kwa sababu kundi fulani halipati haki ya vikao na kujisikia kutengwa ama kuona kwa nini siyo wao. Hivyo, ni chanzo cha chuki na kwa sababu hiyo, wakubwa maofisini hutafuna namna nyingine ya jinsi ya kuwalipa kundi hilo ambalo huwa liko nje ya mfumo wa posho za vikao. Na kwa kufanya hivyo, malipo hayo kama posho za vikao, hutumia fedha za walipakodi iliyopangiwa kufanya kazi fulani kwenye bajeti na hatimaye fedha nyingi hupotea na kushindwa kutekeleza kazi zilizopangiwa kwenye bajeti bungeni. Zaidi katika pendekezo hilo la kuondoa posho za vikao, naomba wadau wote waondoe siasa ndani yake na hakika lijadiliwe kwa ufasaha (maana naamini wakijipa nafasi hiyo) na hasara nyingi zitokanazo na posho hizo zitaonekana kwa vile zi wazi kabisa.

  Nakumbusha pia kwamba, hakuna jambo katika dunia hii laweza kuanzishwa na zaidi ya mtu mmoja (only one man initiates an idea for the interest of the society, either at household or national levels). Chochote tukifanyacho leo hata siku zilizopita, wazo lake lilitoka kwa mtu mmoja na baadaye kwa kujengewa hoja likasikilizwa na hatimaye kwa mchakato mrefu linafikia hatua ya kutekelezwa. Hivyo, waziri Mkulo na wengine wengi, wasijaribu hata kidogo kuona ni vibaya eti mhe. Zitto kupitia chama chake ama vinginevyo kupendekeza wazo la kuondoa posho za vikao. Tujiulize maswali, kwani, kama taifa tunaelekea wapi? Na je, matarajio yetu kama taifa yatashindikana/kucheleweshwa kama tutaondoa posho za vikao? Nini madhara ambayo tungeyaepuka yatokanayo na posho za vikao kwa watumishi wa umma? Kwa uelewa wangu ni kwamba, Sera yeyote hupitishwa kwa njia ya michakato ambapo ili Sera hiyo iwe na manufaa, watu wapewe nafasi kujadili kwa kuchangia hoja zao (ikiwa ni njia moja). Lakini njia ya pili lazima iangalie “legitimacy”, kwamba, Sera husika haikiuki haki za jamii (walipa kodi)? Na katika hilo la posho njia hii ya pili ina nguvu zaidi. Kwa vile kwanza katika kutekeleza mfumo wa posho za vikao tunaleta matabaka ya kipato, punguza muda wa kufanya kazi wa watumishi, kujenga chuki kati ya watumishi, tumia kodi vibaya, kujenga mazingira ya wizi, na kubwa zaidi tunapunguza mchango katika pato la jumla la uchumi wa nchi. Tuanze kuchukua hatua leo!

  Chonza, E. D.

  June 11, 2011 at 12:47 PM

  • Mdau hapo juu umeongea yote ambayo, nilitamani niyaongee, ila kuongezea, ni kuwa ni viongozi wengi ni waonga wa kusimama kwenye ukweli.
   Kumbuka usemi wawa J.F Kennedy na pia Martin Luther King Jr
   “The hottest places in hell are reserved for those who in times of great moral crisis maintain their neutrality”.
   Ni viongozi wachache sana wenye uwezo wa kusimamia kauli ya haki, Hongera Zitto kwa hili.

   mtu

   June 11, 2011 at 3:44 PM

 11. Binafsi nimefarijika sana na ile tu hamu ya Mh Zitto kuwa na wazo kama hilo kwa wale wanaoona kama ni unafiki hasa Mh Mkullo ni kwakuwa tu wanadhani kila hoja inayotolewa na Mpinzani ni hoja dhaifu ama haifai hata kama iko kwa maslahi ya Taifa……………………!! Mh Zitto big up sana ! Nimekukubali sana !

  Hamis

  June 11, 2011 at 5:23 PM

 12. Safi hapa tuache uachama tuangalie maendeleo ya watanzania tukiwemo na sisi.jamani watanzania tuamke na kuwaunga mkono hawa ndugu zetu wapate moyo wa kuendelea kututetea na kuvumbua yale ambayo ccm wameyakalia na kwa manufaa yao binafsi,hivi ni haki kweli mtu alipwe mshahara kwa kazi yake ya ubunge then alipwe posho ktk vikao wakati ni wajibu?huo ni ufujaji wa pesa kwa makusudi kabisa naomba tuondoe imani ya kwamba kila anachosema mpinzani ni uongo au ni uchochezi maana katika akili za kawaida huwezi hili jambo,safi sana mh. Zitto asanteni sana chadema hiyo ndio democrasia mungu awalipe na awabariki katika hili

  Martine/Hafidh

  June 16, 2011 at 12:17 PM

 13. Safi hapa tuache uchama tuangalie maendeleo ya watanzania tukiwemo na sisi.jamani watanzania tuamke na kuwaunga mkono hawa ndugu zetu wapate moyo wa kuendelea kututetea na kuvumbua yale ambayo ccm wameyakalia na kwa manufaa yao binafsi,hivi ni haki kweli mtu alipwe mshahara kwa kazi yake ya ubunge then alipwe posho ktk vikao wakati ni wajibu?huo ni ufujaji wa pesa kwa makusudi kabisa naomba tuondoe imani ya kwamba kila anachosema mpinzani ni uongo au ni uchochezi maana katika akili za kawaida huwezi hili jambo,safi sana mh. Zitto asanteni sana chadema hiyo ndio democrasia mungu awalipe na awabariki katika hili

  Martine/Hafidh

  June 16, 2011 at 12:27 PM

  • Kiukweli zitto swala la posho bungeni halina tija kabisa maana tukiangalia namna wabunge wanavyofanyiwa au rank ya mishahara na marupurupu yao na wafanyakazi wengine kama walimu hakuna uwiano hata kidogo.hivyo swala la kuachia posho na fedha hizo zifanyie kazi nyingine sio jambo la kuamua ni LAZIMA kwa wabunge wote ili kuleta tija na kujari wananchi zaidi wanaweka hapo mjengoni.

   Swala za kusema unataka umaarufu wa kugombea urais 2015 hizo ni sera za MAJI TAKA ZA CCM hakuna kitu kingine zaidi kama wabunge wa CCM na serikali yao wakiendelea na msimami wao wa kupinga swala hilo kwa kutumia wingi wao basi CHADEMA hakuna budi kwenda kuwashiki kwa wananchi kwa kutumia njia ileile ya MAANDAMANO YA AMANI.

   Huo ndio mtazamo wangu

   Ntegeye,Alex P.

   June 20, 2011 at 12:10 PM

   • Kwa mtazamo tofauti kidogo na walio wengi, nadhani ni vizuri Mh Zitto upokee tu hizo posho na uzipeleke huko ulikokusudia kama Katibu wa bunge alivyelekeza. Hiyo itasaidia kuzipata na kuzitumia kama zilivyokusudiwa. Ukizira haitotusaidia. Tuna matatizo mengi na yanazihitaji hizo pesa na nyingine nyingi. Suala la kupelekwa Moja kwa moja sio la msingi. Labda kama kuna ajenda ya siri nyuma ya hizo Posho.

    Kitumba ya Nyoka

    June 25, 2011 at 4:24 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: