Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Hoja niliyotoa Feb 6, 2009 kuhusu CAG na Vyama

with 2 comments

Muswada wa Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2008 (The Political Parties (Amendment) Bill, 2008)

(Kusomwa Mara ya Pili)

(Majadiliano Yanaendelea)

MHE. KABWE  Z. ZITTO:

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia Muswada huu wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa, pamoja na mapendekezo ya mabadiliko mbalimbali, ambayo yameletwa.

Napenda nimfahamishe Mheshimiwa Naibu Spika kwamba, pamoja na schedule of amendments za Mheshimiwa Shellukindo na Mheshimiwa Waziri Marmo na mimi pia nimeleta schedule of amendments nadhani itakuwa inagawiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, la tatu na la mwisho, naipongeza hatua sasa ambayo tumeifikia ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kukagua hesabu za vyama.  Toka Mfumo wa Vyama Vingi umeanza, Wakaguzi wakishazikagua hesabu za Vyama vya Siasa, zinapelekwa kwa Msajili, Msajili anazihifadhi.  Hakuna ukaguzi unaofanywa wa fedha za walipa kodi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kitu ambacho ni kinyume na Katiba, vilevile ni kinyume na Public Finance, lakini ndio kitu ambacho kinasababisha vyama vinapata fedha maeneo ambayo hayajulikani kwa ajili ya uchaguzi.  Wakipata dola, wanatumia nafasi hizo kuweza kuwaridhisha wale ambao wamewachangia fedha.  Kwa hiyo, hatua hii ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, itatusaidia sana kuweza kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za Vyama vya Siasa.

Mdhibiti pia atajua vyanzo wa hizi fedha ni wapi na kwa nini watu wanatumia fedha nyingi sana kwenye uchaguzi.  Chama ambacho kinajulikana kinatumia fedha nyingi sana katika uchaguzi kinajulikana ni chama gani na watu hawaelezi hizo fedha wamezitoa wapi.  Ipo siku tutakuja kuwekewa Serikali hapa na mamluki ambao wana interest tofauti na Taifa letu.   Hatua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, kukagua hesabu za vyama vyote na kutoa taarifa ni ya kupongeza sana.  Sheria ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuum inamtaka taarifa yake iwe submitted Bungeni.  Taarifa hiyo itakuwa submitted Bungeni, Watanzania watajua kodi zao zinatumika namna gani na Vyama vya Siasa.

La pili, kanuni ya ugawaji ruzuku.  Sheria mama, section 17, ibara ya

17(1) na (2) zinaelezea kanuni.  Kanuni hii nilikuwa naomba na Mheshimiwa Waziri wa Nchi, aweze kukubaliana nami, turejeshe umuhimu wa kura ambazo vyama vinapata katika ugawaji wa ruzuku. Sasa hivi tumeweka uwiano sawa sawa, ruzuku inagawiwa kwa mujibu wa idadi ya Wabunge na kwa mujibu wa idadi ya kura za Wabunge.  Nchi ambayo kila chama kimepata na sio kura za Rais ni kura za Wabunge nchi nzima.

Nilikuwa napendekeza kwamba, tutoe weight kubwa zaidi kwenye idadi ya kura ambazo kila chama kimepata ili kuhakikisha ya kwamba, kura zinakuwa na thamani.  Kwa sababu kuna watu ambao wanapiga kura zinapotea kwa sababu hazihesabiwi.  Chama kile kinaendeshwa namna gani na ruzuku inayoendesha vyama hivi leo Serikali ikiiondoa kuna vyama vingine kama chama kinachotawala, sijui kitaendesha namna gani maana wana mlolongo mkubwa wa bureaucracy?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nilikuwa naomba Waziri wa Nchi, akubaliane nami kwamba, tufanye mabadiliko haya ya kukokotoa ruzuku ili kuhakikisha ruzuku hii inakokotolewa kwa mujibu wa kura ambazo vyama vimepata.  La pili, sheria inatamka wazi kwamba, sehemu ya ruzuku ile pia itumike for Parliamentary activities of the Party.

Sasa hili nadhani inabidi Msajili aangalie jinsi ya kuweka regulations, maana Bunge la Tanzania sasa lina Kambi mbili; Kambi ya Upinzani na Kambi ya Chama kinachotawala.  Lakini ile Parliamentary activities kwa fedha za ruzuku, kwa kweli sijaona jinsi gani ambavyo zinaweza kutumika na kusaidia Wabunge katika shughuli zao mbalimbali za Miswada na kadhalika.  Nilikuwa naomba labda hili Msajili anaweza akaliangalia na Waziri katika eneo la regulations.

Naibu Spika, zaidi ya hapo, nilikuwa napenda tupate mabadiliko hayo ya eneo la Wabunge na Madiwani kupoteza nafasi zao, lakini pia eneo la ruzuku.  Nikubaliane kabisa na schedule of amendments, ambayo Mheshimiwa Shellukindo ameileta hapa kwa ajili ya kui-widen ile Council ya Vyama vya Siasa, ili itusaidie kuweza kuwa na National Consensus na kukubaliana mambo gani ambayo tunakubaliana kama Taifa.

Zaidi ya hapo, nakushukuru sana ahsante sana.

NAIBU SPIKA:

Ahsante, nimepokea schedule of amendment iliyoletwa na Mheshimiwa Zitto.  Nawatangazieni hivyo, kwa sababu kutakuwepo na kazi juu ya hizi; msifike watu mkasema ndio ndio kumbe hamjaziona.  Kwa hiyo, tunaendelea na Mheshimiwa Juma Killimbah, Mheshimiwa Shellukindo na Mheshimiwa John Cheyo wajiandae.

Advertisements

Written by zittokabwe

April 21, 2011 at 12:54 PM

Posted in 2008), BUNGE, Zitto Kabwe

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Your report is very informative. Keep it up Mh.Zitto

  vabisay

  April 21, 2011 at 6:36 PM

 2. CHAPA KAZI KAKA,
  KUTOKOMEZA UFISADI NI NJIA YA KUKOMBOA WATANZANIA WALIO WENGI AMBAO NI WANYONGE. TUPO PA1.

  Remmy M. Ngaiza

  May 18, 2011 at 12:35 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: