Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Swali Kwa WAZIRI MKUU-KUHUSU SCANDAL YA STIMULUS PACKAGE

with 2 comments

MHE. KABWE Z. ZITTO:

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu, katika bajeti ya mwaka 2009/2010 Serikali ilileta Bunge mapendekezo ya kutenga zaidi ya shilingi trilioni 1.7 kwa ajili ya kuhuisha uchumi (stimulus package) na Serikali iliahidi hapa Bungeni ya kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali atafanya ukaguzi maalum kwenye eneo hili. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, ametoa taarifa yake. Katika taarifa yake pamoja na kuonyesha kwamba kuna zaidi ya shilingi bilioni 48 ambazo ameshindwa kuzithibitisha kama zilitoka kwa taratibu zinazotakiwa. Lakini pia amesema kwamba Serikali imemnyima taarifa muhimu ikiwemo orodha ya watu na makampuni ambayo yalifaidika na mpango huu. Mheshimiwa Waziri Mkuu unatoa kauli gani kuhusu suala hili?

WAZIRI MKUU:

Mheshimiwa Spika, sijui Mheshimiwa Kabwe maana mimi ndio Waziri Mkuu, ndio ninayeshughulika na masuala ya Serikali kwa upana wake. Kwa bahati mbaya sana hiyo taarifa kwamba aliomba baadhi ya taarifa kutoka Serikali tukamnyima mimi nilikuwa sijazipata na kwa sababu taarifa hizo na mimi nimezipata juzi yaani kwa maana ya ma-book yale na so long ndio nazipitia labda nipe nafasi nikishapata nafasi ya kuipitia then tuta-take up issue seriously kwa sababu hatuna sababu ya kumnyima yeye ndio Mkaguzi wa Hesabu na kwa nini tusiseme  hapana.

SPIKA: Lakini amesema atakupa habari zaidi.

MHE. KABWE Z. ZITTO:

Mheshimiwa Spika, napenda nimpe taarifa Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba nikusomee sehemu ya taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

SPIKA: Mheshimiwa Zitto haitasaidia anasema yeye anaipitia, sasa ukimsomea si unatupotezea muda wetu sisi.

MHE. KABWE Z. ZITTO:

Mheshimiwa Spika, nilikuwa naomba unipe fursa ya kuuliza.

SPIKA: Usimsomee wewe uliza unachotaka kufanya nyongeza amesema yeye hajapata na atakwenda kujisomea huko.

Written by zittokabwe

April 14, 2011 at 3:35 PM

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Wakati mwingine nashindwa kumwelewa huyu mama (Spika) attitude anayoonyesha kwa watoa hoja mbalimbali, hasa kutoka upande wa upinzani. Naona bado ana mwelekeo wa kutaka kulinda interests za chama chake.

  Bundala

  April 14, 2011 at 3:54 PM

  • kwa taarifa yenu hii ni EPA nyingine na watu pesa walichukuwa wakatengeneza mabango ya uchaguzi wakasambaza nchi nzima yaani hawa watu mkiziba huku wanatoboa upande wa pili. nakumbuka mheshimiwa Zito aliwahi tamka kuwa wameshawazibia EPA sasa tuone mapesa ya uchaguzi watapata wapi. Mheshimiwa huko ndo walikotokea mwaka jana hawa watu wana mbinu za ajabu sijuwi mtawafukuza vipi tu. duu mungu tusaidie maana mbinu zao ni hatari

   mawazo dolonyi

   April 14, 2011 at 5:59 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: