Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Tamko: Kuhusu Habari ya Gazeti la Sunday Citizen-Tarehe 20-Machi-2011

with 4 comments

Salaam,

Naomba nitumie nafasi hii kufafanua kuhusu habari ya gazeti la Sunday Citizen ya  Tarehe 20-03-2011.

Nyote mnafahamu kwamba mkutano wa pili wa Bunge la kumi ulikutana kwa ajili ya kuchagua wenyeviti wa Kamati za Bunge ili kupata Kamati ya Uongozi ya Bunge.

Mimi niligombea uenyekiti wa kamati ya POAC kamati niliyokuwa nikiongoza toka Bunge la kumi. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kamati za oversight ni kamati za Kambi rasmi ya upinzani Bungeni ambapo CHADEMA ilitimiza masharti yote ya kuwa kambi rasmi ya upinzani Bungeni.

Wabunge wa CCM kwa kushirikiana na CUF, NCCR na UDP waliamua kuikomoa chadema kwa kuinyima kamati hizi na hivyo kufanya tafsiri ya kanuni. Habari ambazo tulizipata ni kwamba kamati ya PAC ingekwenda kwa Cheyo, LAAC kwa Mrema na POAC kwa Hamad Rashid na hivyo chadema kutopata nafasi yeyote na kupunguza nguvu yake kwenye kamati ya uongozi ya Bunge ambayo hupanga ajenda za Bunge.

Mara baada ya kupata majina ya wajumbe 15 wa kamati ya POAC nilianza kampeni na msaidizi wangu kwenye kampeni alikuwa ni Mhe. Regia Mtema. Tuligawana wabunge ili kupata kura 8 ambazo zingehakikisha ushindi. Kati ya kura hizo nane, tatu ni zetu sisi wabunge wa CHADEMA-Mimi, Mhe Matiko na Mhe Mtinda. Kwa hiyo nilikuwa natafuta kura 5 kutoka CCM. Spika alipotangaza majina ya wajumbe jina la Hamad Rashid halikuwemo.

CCM wakaitisha kikao cha caucus yao ili kufanya maamuzi juu wenyeviti wa kamati (walifanya hivyo hivyo wakati Mimi na Dr. Slaa tulipochaguliwa kuwa Wenyeviti mwaka 2008). Kikao chao kikaamua kwamba mwenyekiti awe Hamad Rashid, na kwa kuwa yeye sio mjumbe basi Spika amteue kuwa mjumbe. Kama Spika hatamteua basi Mhe Amina Mwidau wa CUF(Viti Maalum kutokea Tanga) achaguliwe. Wajumbe wa kamati ya POAC kutoka CCM wakapinga ndani ya kikao chao kwamba mimi ninafaa zaidi kuliko huyu Mhe.Amina Mwidau wa CUF (ambaye mie wakati huu nilikuwa simfahamu kabisa).

Wajumbe wote waliopinga uamuzi wa chama ninaambiwa walizomewa na hatimaye kuitwa jina mmoja kutamka kuwa watafuata uamuzi wa chama. Pinda ndiye aliongoza kikao hicho.Spika alipoambiwa abadili orodha yake na kumweka Mhe Hamad Rashid, alikataa kwa hoja kwamba orodha imeshakuwa public na hawezi kuibadili.

Akabakia Mhe Mwidau kama mgombea ambaye CCM wanamtaka. Wajumbe watano ambao walikuwa wamenihakikishia kura walimfuata Waziri Mkuu kumwambia kuwa wao wataenda kinyume na maamuzi ya chama na watanipigia kura.

Usiku kucha wa siku ya kuamkia kupiga kura mimi na Regia tulizunguka kuhakikisha kura zetu zinabakia intact na hata kumshawishi Mbunge wa CUF Mwidau ajitoe. Tukiwa tunajiandaa kwenda kwenye kupiga kura CCM wakaitwa kwa dharura na kuambiwa na Pinda kuwa uamuzi wa jana usiku umefutwa na Rais ameagiza achaguliwe Zitto. Tukaenda kwenye uchaguzi, nikagombea na Mhe Mwidau na nikapata kura 13 dhidi ya 2 za Mwidau. Hiyo ndio background kwa ufupi.

Kwa hiyo, sikumpigia simu Rais kutaka anisaidie. Nimekaa bungeni miaka mitano na nazijua siasa za Bunge. Nilikuwa nimejipanga kiasi ambacho kushindwa kungetokea iwapo tu Chief Whip wa CCM angekuja kusimamia mwenyewe uchaguzi. Ikumbukwe pia mie nimekuwa student leader, najua siasa za kipiganaji. Inawezekana hata huyo mgombea angekuja kwenye mkutano baada ya kura kupigwa!

CCM walibadili msimamo baada ya kutishiwa strong rebellion from their own ranks that they will vote for me. Wabunge 5 wa CCM kati ya 11 kumwambia Pinda kuwa watanipa mimi kura ilikuwa ni ishara tosha kwamba wanaweza kuaibika.

Pia inawezekana kabisa CCM walibadili msimamo asubuhi ili kutaka kudhoofisha hoja ya chadema kwamba mabadiliko ya kanuni yaliwalenga kwa kusema ‘mbona Zitto kashinda’ Hayo ndio maelezo ninayoweza kuwapa ndugu zangu kuhusiana na suala hili. Kama kuna maswali zaidi nitawajibu kwa kadiri ya uwezo wangu.

Zitto Kabwe (MB)

20/03/2011

Advertisements

Written by zittokabwe

March 21, 2011 at 9:49 AM

4 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. I DO APPRECIATE THE WAY YOU DO POLITICS.

  NORBERT A.NONGWA

  March 21, 2011 at 1:53 PM

 2. sioni tatizo kuhusu wewe kuchaguliwa hata kama ulimpigia rais simu shida ipo wapi???

  leopold kimaro

  March 21, 2011 at 9:44 PM

 3. Tunakushukuru baba kwa ufafanuzi wa Habari hiyo ya CITZENS.
  Wakati mwingine inahitaji ujasiri wa kufafanua baadhi ya mambo yanayotolewa na vyombo vyetu vya Habari.

  Fidelis Kulolwa

  March 22, 2011 at 4:23 PM

 4. .Kabla ya mkutano huo wa Bunge Chadema ilieleza kuwa imeamua kuvitenga vyama hivyo kwa kuwa vinashirikiana na CUF ambayo kwa mtazamo wake haina tofauti na CCM. CUF na CCM wameamua kuungana Zanzibar na kuunda Serikali ya Mseto na kwa kuwa sheria ya vyama ya Zanzibar ndiyo inayotumika pia Tanzania Bara Chadema imeona CUF na CCM ni wamoja alieleza Katiba Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa alipokuwa akitoa tamko la Kamati Kuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam mwezi uliopita. .Hoja hiyo jana ilifanya mkutano kuanza kwa moto pale Naibu Spika Job Ndugai alipowasilisha azimio linalotoa tafsiri ya nini maana ya Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni akitaka lipitishwe na Bunge hali ambayo ilitafsiriwa kuwa ni mkakati wa kuivunja nguvu za kisheria Chadema ..Mkutano huo ulitoa tafsiri inayobainisha kuwa kambi rasmi ya upinzani bungeni ni mjumuiko wa wabunge wote wa upinzani bila kujali vyama wanavyotoka hivyo kutoa fursa kwa wabunge hao kuwa na haki ya kuchaguliwa kuongoza kamati tatu za bunge zinazohusika na Hesabu za Serikali..Kamati hizo kwa mujibu wa kanuni za Bunge ni Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa LAAC Kamati ya Hesabu za Serikali PAC na Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma POAC ..Hata hivyo tafsiri iliyoongezwa katika kanuni hizo za Bunge haimwondolei uwezo Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe kuteua wabunge anaowataka pale atakapokuwa akiunda Baraza la Mawaziri Kivuli..Wakati wa mjadala huo baadhi ya wabunge waliugeuza Ukumbi wa Bunge kuwa jukwaa la mipasho na mabishano.

  Mchangiaji

  March 28, 2011 at 7:12 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: