Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

Tamko La CHADEMA kuhusu Mabomu ya Gongo la Mboto

with 9 comments

Mhe. Joseph Selasini (MB)

Kupitia Waziri Kivuli wa Ulinzi Na Jeshi La Kujenga Taifa,Joseph Selasini akitoa tanko la Chadema Leo Kuhusu milipuko ya Mabomu Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam.Picha na Mwanakombo Jumaa, MAELEZO

MAAFA YA GONGO LA MBOTO: WAZIRI WA ULINZI NA MKUU WA MAJESHI WAJIBIKE!

TAARIFA KWA UMMA

DODOMA, FEBRUARI 17, 2011

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeeleza kushtushwa na kusikitishwa na taarifa za milipuko ya mabomu katika Ghala la Kuhifadhi Silaha la Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika eneo la Gongo la Mboto, Dar es Salaam jana jioni.

Aidha, kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imewapa pole ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wote wa Tanzania kwa sababu ya maafa haya. Pia Kambi hiyo imezitaka mamlaka zote za umma zinazohusika kuchukua hatua za haraka kuhakikisha wananchi wote walioathirika na maafa haya wanapatiwa huduma zote wanazohitaji katika kipindi hiki cha msiba huu. Hii ni pamoja na kuwapatia huduma za maziko wale wote waliofariki, matibabu kwa waliojeruhiwa na hifadhi kwa wale waliopoteza makazi yao. Aidha, ni muhimu kwa vyombo vya usalama kuhakikisha ulinzi wa mali za wananchi katika maeneo yote yaliyoathirika na ambazo zitakuwa hazina ulinzi baada ya wananchi kukimbia maeneo yao.

Taarifa ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeeleza kwamba tukio hili ni la kushtusha na kusikitisha hasa kwa kuzingatia kwamba haijapita miaka miwili tangu tukio la aina hiyo hiyo litokee katika Ghala ya Silaha ya Kambi nyingine ya JWTZ katika eneo la Mbagala, Dar es Salaam, ambalo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu thelathini na uharibifu mkubwa wa mali za umma na za wananchi binafsi. Aidha, milipuko ya Mbagala ilipelekea Serikali kutumia mabilioni ya fedha za umma kwa ajili ya malipo ya fidia kutokana na vifo, majeruhi na uharibifu wa mali binafsi za wananchi.

Akielezea tukio la milipuko ya Gongo la Mboto, Msemaji wa Ulinzi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mh. Joseph Selasini alisema: “Milipuko ya Gongo la Mboto inaonyesha dhahiri kwamba Serikali ya Awamu ya Nne ya Chama cha Mapinduzi (CCM) haijajifunza lolote kutokana na maafa yaliyotokea Mbagala mwaka juzi. Maana kama Serikali ingejifunza kutokana na maafa hayo ingeshachukua hatua za dharura na za haraka kuhakikisha kwamba maafa ya aina hii hayatokei tena.” Mh. Selasini alizitaja baadhi ya hatua hizo kama ni pamoja na kuhamisha maghala yote ya silaha na mabomu yaliyo karibu na maeneo wanayoishi raia na kuyapeleka katika Kambi za JWTZ zilizoko mbali kabisa na maeneo ya raia. “Haiwezekani kwa Serikali kuendelea kuweka maghala ya silaha katika Kambi za Jeshi zilizo karibu na wananchi na hivyo kuhatarisha maisha yao namna hii”, alisema Mh. Selasini.

Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imewataka Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kujiuzulu mara moja ili kuwajibika kisiasa kutokana na maafa ya Gongo la Mboto na ili kupisha uchunguzi huru na wa kina wa chanzo na/au sababu za milipuko hiyo. Mh. Selasini alisema: “Dr. Hussein Mwinyi alikuwa Waziri wa Ulinzi wakati wa maafa ya Mbagala; na Jenerali Mwamunyange alikuwa Mkuu wa Majeshi. Maafa ya Mbagala yalitokea chini ya dhamana na/au usimamizi wao. Na mara baada ya maafa hayo, Waziri Mwinyi na Jenerali Mwamunyange waliliahidi taifa kwamba maafa ya aina hii hayatatokea tena. Sasa yametokea. Inaelekea, kwa hiyo, kwamba ahadi yao ilikuwa sio ya kweli na/au hawakuhakikisha kwamba inafanyiwa kazi ili iwe ya kweli. Viongozi hawa hawana budi kuwajibika kwa hiari yao wenyewe au kuwajibishwa kama itahitajika.”

Mh. Selasini aliongeza kusema kwamba hadi leo hakuna taarifa yoyote rasmi iliyowahi kutolewa hadharani kwa wananchi na/au kwa wawakilishi wao Bungeni ya chanzo na/au sababu za maafa hayo. “Hadi leo hii wananchi na/au wawakilishi wao Bungeni hawajaambiwa kama kulikuwa na makosa ya makusudi na/au ya uzembe na/au kama hatua zozote za kinidhamu na/au za kisheria zilizochukuliwa dhidi ya mtu yeyote kutokana na kusababisha na/au kuwajibika kwa maafa hayo. Jana maafa mengine ya aina hiyo hiyo yametokea tena na kwa kadri ya taarifa rasmi ya Serikali watu wengi wameuawa na wengi wengine kujeruhiwa na mali nyingi kuharibiwa. Kwa sababu hizo, huu ni wakati muafaka kwa Dr. Mwinyi na Jenerali Mwamunyange kuonyesha uadilifu wao kwa kujiuzulu nafasi zao ili kuwajibika kwa maafa haya.”

Mwisho, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imependekeza iundwe Tume Huru ya Uchunguzi na/au Kamati Teule ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuchunguza kwa kina chanzo, sababu na madhara yote yaliyosababishwa na milipuko ya Gongo la Mboto. “Kwa kuzingatia historia ya uchunguzi wa milipuko iliyotokea Mbagala mwezi Aprili 2009, Tume Huru na/au Kamati Teule ya Bunge lazima itoe taarifa yake hadharani kwa kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, alishauri Mh. Selasini.

Advertisements

Written by zittokabwe

February 17, 2011 at 6:13 PM

9 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. […] This post was mentioned on Twitter by Jahu M.K and Shamsan_Wa_Angel, Zitto Zuberi Kabwe. Zitto Zuberi Kabwe said: Tamko La CHADEMA kuhusu Mabomu ya Gongo la Mboto http://wp.me/pRboX-gu […]

 2. NDIO CHADEMA MTALIPWA NA MUNGU CCM HAWAMJUI MUNGU,IKISHINDIKANA,HAWATOJIUZURU BASI ITISHENI MAANDAMANO HADI WAONDOKE TUME TUMECHOKA HAKUNA CHOCHOTE AMBACHOKINAENDELEA JUU YA HIZO TUME AMBAZO ZINAUNDWA AHSANTE.
  \

  NIHUKA DR

  February 17, 2011 at 10:29 PM

 3. nashauri waziri wa ulinzi ajiuzulu, kwani kilichotokea mbagala ni kile kile kilichotokea gongo la mboto bado hakujifunza ,au alikuwa mpaka roho nyengine za watu zitoke kwa style ile ile ya mbagala halafu waunde tume.zitaundwa tume ngapi Tanzania
  jamani tunateketea

  ali

  February 17, 2011 at 11:24 PM

 4. Nakubaliana na tamko la CHADEMA la kuwataka Waziri wa Ulinzi na Mkuu wa Majeshi wawajibike. At least waonyeshe kwamba wamewakosea Watanzania kwa kutoonyesha kuwa makini kwa tukio hili, ambalo walishatamka kwamba halingetokea tena baada ya lile la Mbagala. Na kabla watu hatujasahau, na wala ripoti ya lile tukio la Mbagala haijatolewa, tayari tukio jingine linaloelezewa kuwa ni baya kuliko lile la Mbagala limetokea! Kwa nini wasionyeshe uungwana wa kuwajibika kwa kujiuzulu nafasi zao? Kutoa pole ya mdomo haitoshi. Kila mmoja anaweza kutoa pole tu. Lakini tunataka iingie kwenye kumbukumbu kwamba hata wao jambo hili limewakera. Wakae pembeni kama ishara ya kuonyesha kukerwa na kujutia kwa nini limetokea jambo hili mara mbili chini ya uongozi wao.

  Masalakulangwa

  February 18, 2011 at 11:50 AM

 5. CHADEMA tunawaona nyie msikate tamaa.Hata wakisema mnatafuta madarka,sisi si wajinga.TUNAONA.Hivi huu uchungu wa nchi ya Tanzania hawa waheshimiwa wa Jembe na Nyundo(CCM) hawawezi kuwa walau waungwana wakasisitiza juu ya kujiudhuru kwa Waziri wa Ulinzi?Hivi tukiwanyima kura 2015 mtaita na huo ni udini? Embu nyie wabunge wa CCM kemeeni maovu, pongezeni mema.Tumechoka na uzandiki huu.

  Fidelis Kulolwa

  February 18, 2011 at 3:53 PM

 6. how come sif they don resign?we need to deliver issues in a constructive way as we understand can be irrespibility and what could be the way to?chadema mpo sahihi lakin bado hamna mbadala

  emmanu elmasonga

  February 20, 2011 at 12:23 AM

 7. Kwa kweli hii hali inasikitisha inaonyesha ni jinsi gani Tanzania imetawaliwa na Chama mama kisicho na maendeleo yoyote zaidi ya kutudanganya eti maisha bora kwa kila mtanzania inawezekana au ndo kwa kuuwa watu na mabomu kweli hii si haki hata kidogo, Ni bora ajiudhuru tu huyo Waziri wa Ulinzi anaonyesha ni jinsi gani ana kwalification za kukabiliana na majanga kama ni hivi kwa kweli elfu mbili na kumi na 5 ni mshike mshike yaan lazima tuwango’e hata kwa damu sio kuanzia chama mpaka uongozi wote unanuka tu.

  Ramso

  February 20, 2011 at 12:41 PM

 8. Huu siyo uungwana kabisa, kama military strategies zimeanza kutumika dhidi ya raia, raia aliyekufa hatujui angezalisha kiasi gani ktk pato la taifa, mimi napendekeza vingozi hawa washitakiwe kwa mauaji ya kukusudia, la sivyo wananchi tutachukua sheria mkononi, inauma sana!

  Papaa Sammy(UDOM)

  March 4, 2011 at 1:06 PM

 9. Huu siyo uungwana hata kidogo, siasa kwenye roho za watu siyo issue, sajasomea upelelezi, ila ninaokabisa kulipuka kwa mabomu Gongo ni mbinu za kijeshi na imepanwa na kutekelezwa effectively, ili iwefunzo, viongozi hawa waachishe kazi na washitakiwe kwa kosa la kuua kwa kukusudia, la sivyo kitamuka!

  Papaa Sammy(UDOM)

  March 4, 2011 at 1:37 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: