Zitto na Demokrasia

Zitto na Demokrasia

TAMKO

with 11 comments

Natoa tamko kuwa habari ya Jamboleo ni ya kutunga yenye lengo la kugawa uongozi wa CHADEMA na kuleta mgogoro.

Kumekuwa na habari kwenye magazeti kitambo sasa zenye kuonyesha mgogoro ndani ya CHADEMA. Napenda kuwajulisha marafiki zangu kuwa hakuna mgogoro wowote. Sihami wala sifukuzwi CHADEMA.

Tuna kazi moja tu, nayo ni kuimarisha chama kuelekea 2015 wakati tukipigania mabadiliko ya Katiba.

Tusiyumbishwe!

Zitto Zuberi Kabwe

Advertisements

Written by zittokabwe

December 7, 2010 at 10:06 AM

Posted in Uncategorized

11 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Great my man!
  Nadhani tatizo kubwa ni kauli tata unazozitoa wakati usio mwafaka kwa kuonesha misimamo tofauti na matarajio ya baadhi ya wanachama wa Chadema.

  Nakuomba uwe na nia moja na uoneshe kwa vitendo jinsi ulivyojidhatiti katika kukijenga chama na kuweka maslahi ya chama mbele.

  Watanzania wengi tunakupenda na tunaona bado una nafasi nzuri ya kufanya makubwa mbeleni. Jitahidi kutoongea mambo ya misimamo yako nje ya vikao hasa inapokuwatofauti na maamuzi ya vikao…. Kikao kikipitisha uamuzi basi wote mfuate maana ndo maamuzi hayo hata kama huyataki na ndo demokrasia ilivyo na haupaswi kusema nje ya kikao maamuzi hayo!!! Ndugu yangu Zitto – huo ni ushauri wangu binafsi.

  Eng. Magafu

  December 7, 2010 at 10:30 AM

 2. […] This post was mentioned on Twitter by Lusajo L.M. and Issa Mwamba Wa'Fatma, Zitto Zuberi Kabwe. Zitto Zuberi Kabwe said: TAMKO: http://wp.me/pRboX-fJ […]

 3. Safi sana Kaka, Tuna Imani na Chama Chetu na tusikubali kabisa kudanganywa na Magazeti ya Serikali ya Ccm, wameshaanza kujikanganya wenyewe, Wameeleza kuwa swala la Umeme litabaki kuwa Historia ndani ya Nchi hii lkn wapi, ndio kwanza wanaanza kutupiana mipira swala la Dowans na Richmond.

  Chapa S. Magotti

  December 7, 2010 at 10:43 AM

 4. Hi;
  Mie nakutakia maisha marefu katika siasa, ila ni vizuri kujiepusha na kauli ambazo zinaonyesha mgawanyiko ndani ya chama to my point of view kauli uliyoitoa kuhusiana na walkout ya CHADEMA ilikuwa haina umuhimu na wala haijengi chama na hata ungenyamzana kulikuwa hakuna negative effects to ur side na kwa chama chako.

  CCM waligawanyika katika bunge lililopita na nyie mkapata chance ya kushambulia sasa inaweza kula kwenu.adui anangalia wapi kuna udhaifu kwanza.
  poa ,kila la kheri

  jamali

  December 7, 2010 at 2:13 PM

 5. Asante Mheshimiwa Zitto kwa kututoa hofu katika hili. Mafisadi watapanga kila mbuni ya kuigawa Chadema, muendelee kuwa Makini, Asante

  Paskal

  December 7, 2010 at 2:59 PM

 6. Hello, tunashukuru kwa TAMKO, ni kweli ilifika mda tulikuwa hatuelewi nini kinacho endelea; Nilipokuwa mtoto mdogo mama aliniasa ” Usimtishie Mtu kitu” kwa sababu adui akisikia atatenda akijua watu watajua umetenda; Kwa mda huu Mungu akupe hekima ya mambo yote.

  Emmanuel Haule

  December 7, 2010 at 8:48 PM

 7. Ahsante Mh. Zitto kwa kauli hiyo, ila nina hoja nyingine kidogo naomba uipe umuhimu wa kipekee kwani naona wewe tu ndiye utakayeweza kutatua kero kuu ya wapiga kura wako kwa sasa,sifahamu email yako ila najua hapa utanisoma halafu utanipa e mail nikuattachie picha na videa uangalie jinsi wananchi wa Kigoma wanotumia reli wanapata shida! Nimeongea na watu wengi na hata station master mwenyewe sikumpata mkuu wa wilaya in all my stay at kgm ingawa nilimtafuta HALI NI MBAYA SANA , TIKETI ZA DODOMA ZINARUSHWA HADI TSH 30000 VS HALALI TSH 14500HIVI. WANAANZA KUKATA TIKETI JUMAPILI SAA 4 NA BAADA YA KUKATA TIKETI KAMA 15 HIVI WANASEMA ZIMEISHA NIMESHUHUDIA MAMA MMOJA ALIYELALA STATION AMBAYE ALIKUWA WA 17 KABLA ZAMU YAKE IKATANGAZWA TIKETI ZIMEISHA! MAMA YULE ALIAMBULIWA KUNGOKA UKUCHA BAADA YA KUKANYAGANA KWENYE FOLENI! KATIKA KUHOJI WARUSHA TIKETI NIKAAMBIWA WANAACHA KWA STATION MASTER SI CHINI YA 5000 KWA KILA MANUNUZI YA TIKETI NA KUUZA KWA WASAFIRI KWA ZIDIO LA SH 10,000 HADI 20000 JUU BEI YA TIKETI HALALI! NIMESHANGAA SANA HALII INAVYOKALIWA KIMYA NA MBUNGE WA KIGOMA NJINI MKUU WA WILAYA NA HATA WA MKOA PAMOJA NA MALALAMIKO KIBAO HADI WANANCHI WAMEJENGA DHANA KUWA WANAKULA PAMOJA!HABARI ZA KAMATI YA BUNGE NA USHAURI WA KUKATA TIKETI SIKU YA SAFARI NIMEZIPATA ILA USHAURI HUO UNATUMIWA VIBAYA NA WANAANZA SAA 4 KWA MAKUSUDI! HAIHITAJI ELIMU YA CHUO KIKUU KUJUA KUWA HATA KAMA WANGEKUWA TAYARI KUKATA TIKETI ZOTE DIRISHANI KUANZIA SAA4 WASINGEWEZA KUTOA TIKETI 1000HIVI( BEHEWA 20 WATU 80 KILA BEHEWA) KWA MASAA 5 AU 6 HIVI MAANA SAFARI NI SAA 11. NAKUOMBA USHULIKIE HARAKA KUNA WATU WANATOKA VIJIJINI WANALALA STATION ILI KUWAHI FOLENI LAKINI KABLA HAWAJAKATA TIKETI WANAAMBIWA ZIMEISHA!

  BURAKEYE

  December 8, 2010 at 7:25 PM

 8. Habari ya tiket za usafili wa tren inatia simanzi kubwa sana na inauma sana. Na hivi mvua zimeanza hata usasfili wa Basi utakuwa shida tena. Mimi niwaombe kaka shughulikieni daraja la malagalasi ili Kigoma iweze kuungwa na mkoa wa Tabora, Usafili ni shida ndugu yangu, Hivi mkishilikiana na akina SIx,pamoja na Prof Kapuya kweli daraja na barabara ya rami inashindikana? Manake hiyo barabara itapita hata kwenye majimbo yao.

  Tulisikia, aliyekuwa mkurugenzi wa Tanrod alishasain mkataba na serikali ya Korea kusini kuhusu kujenga daraja hilo, ujenzi utaanza lini?

  Halafu miye huwa najiuliza hivi mkoa wa Kigoma hasa kigoma mjini huwa hakuna bajeti ya kukarabati barabara za mitaani? manake miaka nenda rudi huo ukarabati wa hata mitaro huwa haufanyiki kwa nini? Nenda Kisangani, mrole, fid, majengo na viunga vingine vya mji hutaona hata barabara moja at least ikiwekewa changalawe au kukarabati mitaro.

  Mbona mikoa mingine ukarabati hufanyika kila mwaka? Bila shaka Wabunge mnaingia kwenye vikao vya halimashauri kwa nini hilo hamliulizi na utekelezaji ukafanyika mara moja? Mpe ujumbe huo na Serukamba, misaada yetu kwenu ni kuona miundo mbinu na shughuli za maendeleo zikifanyika majimboni.

  Nawasilisha,
  hata hivyo nakupa pole kwa changamoto za hapa na pale ndani ya chama na nje ya chama kwa ujumla.Mti ulio imara hata ukitikiswa na upepo hauwezi kuanguka.

  jewe kahigi

  December 9, 2010 at 11:23 PM

 9. zitto kutokana na kusikia habari ya wewe kuenguliwa unaibu kambi yetu ilinichanganya sana, nini kilitokea naomba nijuris

  chacha marwa

  December 11, 2010 at 9:25 AM

 10. The most difficult thing is to find a blog with unique and fresh content but your blog is different. Bravo.

  Faye Conaway

  December 13, 2010 at 8:51 PM

 11. Mh. Zito Ninatamani siku moja kuona nchi hii inakamatwa na kuongozwa na chadema,lakini hatutafikia huko kama hakuna uwezeshwaji wa kukijenga chama kutoka ngazi ya shina. Watanzania wengi wako vijijini lakini aibu kubwa inayotukabili chadema kuna hata majimbo yanayoongozwa na chama chetu lakini ofisi za chama ziko kwenye nyumba za watu,wakereketwa au tumepanga, tafadhali jipangeni tupate angalau ofisi kila makao makuu ya wilaya,baadae kata na hata vijiji. Naamini INAWEZEKANA TUKIAMUA

  Mr Mwita

  December 30, 2010 at 11:01 PM


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: