Maelezo ya Bajeti Kivuli
Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo kuita ni vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini.
| MAPATO |
SHILINGI MILIONI |
||
| A | Mapato ya ndani |
|
11,889,078 |
| i)mapato ya kodi (TRA) |
10,232,539 |
|
|
| ii)Mapato yasiyo ya kodi |
1,163,533 |
|
|
| B | Mapato ya Halmashauri |
493,006 |
|
Mapato haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa ya kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii inaonyesha kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani.
Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti.
Kabwe Zuberi Zitto,Mb
Waziri wa Fedha na Uchumi Kivuli
19.06.2012












Mmesameheka, lakini mara nyengine pateni muda wa kuhariri ili msitoe “mwanya wa mashambulizi”.
HAMISI
June 19, 2012 at 4:56 PM
Jitahidini kuwamakini sana maana hilo nidio na mkumbuke kuwa kibaya huvuma zaidi kuliko kizuri.
Enock
June 19, 2012 at 5:54 PM
wakati mwingine tuoneshe umakini kama chama chetu baba. Ila watanzania ni waelewa na tunaelewa error na fraud usijali kabisa baba.
tari
June 22, 2012 at 5:38 PM